Ripoti ya BoT kaa la Moto. Je, Rais Samia atamng'ata jongoo kwa meno?

KooZito

JF-Expert Member
Dec 14, 2020
396
1,377
Wanabodi, nawasalimu kwa jina la JMT.

Ni hivi, mwaka 2015 katika vikao vya ndani ya CCM na hasa NEC vilipitisha majina 5 ya wagombea ambao ni Magufuli, Membe, January, Asha-Rose na Balozi Amina. Uhakika niliona ni kwamba JK alimtaka Membe aliyekuwa adui wa Lowassa ambaye jina lake lilikatwa.

Ghafla JK alipoingia ukumbini akakuta Emmanuel Nchimbi na Sofia Simba wakiongoza watu kuimba, "tuna Imani na Lowassa" kuashiria kutomuunga Membe.

JK alimuuliza ushauri Mkurugenzi wa TISS Othman Rashid kwamba afanye nini baada ya Mkapa kumwambia amkate Membe kwa kuwa amemkata Lowassa.

Jibu la Othman lilikuwa hivi: "Mh wewe ni Mkwere?", 'ndiyo'. Unamjua jongoo mdudu? JK akasema ndiyo. Othman akamuuliza, "umewahi kumkanyaga jongoo?' Jakaya, "yes" anaendelea, "anatoa harufu mbaya sana"

Othman akamwambia, "sasa fumba macho mkamate jongoo kwa mkono wako na umng'ate kwa meno yako, yaani mtoe Membe kwenye 5 Bora lasivyo chama kinakufia mkononi". Ulikuwa ni uamuzi mgumu sana. Membe akakatwa sawia na kijana January na Utamaduni wa kutowaamini wanawake embe dodo likamdondokea Magufuli badala ya Rose na Amina.

Ndugu zangu. Ziko taarifa kutoka kikao Cha Cabinet kilichopita kwamba ripoti ya taarifa za fedha alizotaka SSH za mwezi January to March ziko tayari na amekabidhiwa. Aliyechungulia ripoti hiyo amekuta jina la VP Mpango akiwa alihusika moja kwa mbili katika ufisadi. Kwamba wote watakaonywea kikombe Cha hasira ya mama ni pamoja na "kipenzi" chake, Philip Mpango. Swali: je, mama atafumba macho amng'ate jongoo? Amweke pembeni Makamu wake Mpango aliyemsifia hadharani kwa uadilifu au ataamua kufunika kombe mwanaharamu apite?

Ripoti hii ni kipimo Cha uadilifu na maamuzi magumu kwa mama Samia. Tusubiri.
#FreedomIsBack
 
Kwanza ripot yenyewe unadhan itasomwa na kuwekwa hadharani mkuu?

Na kwa vile Watanzania hawana utamaduni wa kujiuzulu, huyo Mpango atakuwepo tu anachungulia akisema ''hiiiii bhaghosha!!!'''

Ripoti itaishia huko kabatini na mambo yataendelea kama kawa....hakuna jipya kwa Mama,
 
Leta kwanza ushahidi mezani..Vinginevyo hii nayo itakua tu tetesi.Kiufupi tumwagie hiyo ripoti hapa.
 
Mmeanza majungu yenu baada ya kuona Mpango Isdor ni kizingiti katika kumuingiza Mama Samia chaka?
Mpango siyo kizingiti,
Yeye ndiye alikuwa analazimishwa na mwendazake kupika takwimu za uongo kutangaza makusanyo ya Kodi.
 
Nchi imetoka kwenye transition juzi tu, hawawezi kufanya mzaha kiasi hicho, wapo watakao wajibishwa lakini VP atalindwa.

Japo imani naye itapungua, atabaki kuwa 'ceremonial figure tu'.

Iko hivyo kote duniani, lazima rais uwe na ujasiri wa kuangalia pembeni muda mwingine kwa maslahi mapana ya taifa.
 
Tuwekeeni hapa hata excutive summary yake
Screenshot_20210310-213811.png
kwa sasa
 
Acheni majungu..jengeni umoja wa kitaifa..Msimpake matope mpango..sasa ivi tupo tunajenga nchi atutaki majungu.
 
Wajuaji mko wengi sana Tanzania mnaishi kizembezembe. Ndo maana unaweza kusafiri kilomita 500 nchini ukakutana tu na mapori yasiyoendelezwa.

Kikubwa Jiwe harudi tenaaaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom