Ripoti UNDP 2019: Maendeleo ya Watanzania yamerudi nyuma kwa 25%

Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2019 inaonyesha kwa ujumla maendeleo ya binadamu nchini kwa mwaka 2018 yalirudi nyuma kwa asilimia 24.9, ikilinganishwa na mwaka 2017.

Uchambuzi katika ripoti hiyo umezingatia hali ya kutokuwapo usawa katika mazingira ya kuzaliwa mtoto, katika kipato, katika elimu na katika tofauti kwa wenye mali na wasiokuwa nazo.

Pamoja na hali hiyo, Tanzania bado inaonekana kuwa juu ya makadirio ya jumla katika ukanda wa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara (asilimia 30.5) na kidunia (asilimia 31.1).

Ripoti hiyo ya Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) iliyozinduliwa Desemba 18, mwaka jana ikiwa na jina la “Mtizamo wa Zaidi ya Pato, Zaidi ya Wastani, Zaidi ya Mahitaji ya Leo: Tofauti za Kijamii na Kiuchuni Katika Karne ya 21”, inahusisha nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa (UN).

“Maendeleo yamerudi nyuma kutokana na ukuaji wa uchumi kutokuwa jumuishi katika sekta zinazohusisha maisha ya Watanzania wengi,” alisema Dk Abel Kinyondo wa Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

“Katika miongo miwili iliyopita, uchumi umekuwa ukikua kwa wastani wa asilimia 7, lakini unahusisha sekta zisizokuwa na ajira ya Watanzania wengi. Ndio maana unasikia wanalalamika uchumi unakuwaje wakati hakuna pesa. Matokeo yake tabaka la maskini na tajiri linaongezeka.

“Kwa mfano, kuanzia mwaka 2016 hadi sasa kulikuwa na madai ya nyongeza za mishahara, ajira , kutopandishwa vyeo. Maana yake ni kwamba purchasing power (uwezo wa kifedha) inashuka kwao, kwa hiyo pengo linaongezeka la kutokuwapo na usawa katika maeneo hayo.”

Hata hivyo, Humphrey Moshi wa Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anatofautiana na maoni ya Dk Kinyondo.

“Takwimu zinakinzana na uhalisia unaoendelea katika uwekezaji katika sekta ya elimu, pamoja na huduma mbalimbali za kijamii,” alisema.

Lakini alikubaliana na kuongezeka kwa tofauti katika jamii duniani, akisema inatokana na utandawazi.

“Na hali inaonyesha tofauti hiyo inaweza kuongezeka zaidi katika tofauti za kijamii,” alisema.

Ripoti hiyo pia inaitaja Tanzania kudondoka katika viashiria vya maendeleo ya binadamu kwa mwaka 2018 baada ya kupata alama 0.528 ikilinganishwa na alama 0.519 ilizopata mwaka 2015. Licha ya kuwa juu ya wastani wa kikanda na kidunia. Tanzania imeshika nafasi ya 159 kati ya nchi 189.

“Kwa mwaka 2018, Tanzania ilipata alama 0.528. Hata hivyo baada ya viashiria kutazamwa kwa jicho la usawa, viashiria vilishuka kwa Tanzania hadi asilimia 0.397,” inasema ripoti hiyo.

Ripoti hiyo inasema endapo jamii zikiondoa mwanya katika usawa wa kijinsia katika shughuli za kilimo, huenda uzalishaji ukaongezeka kutoka asilimia 7 hadi asilimia 19, ikizitaja Tanzania, Malawi na Rwanda.

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Ole Ngurumwa alisema maendeleo ya watu yanatakiwa kwenda sambamba na maendeleo ya vitu.

“Maendeleo ni sehemu ya haki za binadamu kwa hiyo ni vyema Serikali ikakumbuka kuweka uwiano sawa katika maendeleo ya watu na vitu,” alisema.

Ripoti hiyo inaonyesha asilimia 85 ya watu waishio mijini nchini ndiyo wanapata huduma za maji safi na salama huku vijijini wakiwa ni takribani asilimia 43 tu.

Takwimu hizo hazijatofautiana kwa kiwango kikubwa na za Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), kwa mujibu wa katibu mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo.

Kitila alisema takwimu za mwaka 2015/2016 zinaonyesha asilimia 47 ya Watanzania ndio wanapata maji safi na salama vijijini.

“Kwa takwimu za NBS za Desemba mwaka jana, kuna asilimia 64.8 vijijini, kazi inafanyika lakini bado tunatakiwa kuongeza kasi zaidi vijijini. Kazi hii inachagizwa na uanzishwaji wa wakala wa huduma za maji vijijini,” alisema Profesa Kitila.

Hata hivyo, Januari mwaka jana, Profesa Kitila alinukuliwa akisema ukosefu wa weledi kwa wahandisi umesababisha kukwama kwa miradi ya maji vijijini.

Matokeo mengine

Kwa mwaka 2018, tofauti ya kipato kwa Watanzania ilikuwa ni asilimia 22.4, juu ya wastani wa asilimia 27.6 ambayo ni makadirio ya nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara, na kidunia ni asilimia 25.

Hali ya kutokuwa na usawa katika umri wa kuishi imepata asilimia 25.3 juu ya malengo ya nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara.

Akizungumza jana, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile alisema bado hajaisoma ripoti hiyo hivyo alisema ataizungumzia baadaye.
Mkurugenzi wa UNDP Tanzania awajibishwe kwa kuupotosha umma wa watanzania pia Tanzania ivunje uhusiano na UNDP mpaka hapo itakapoomba radhi.
Maisha ya watanzania kwa sasa ni mazuri zaidi na biashara zao zimekua zaidi kuliko wakati wowote yangu Uhuru.
 
Kitachofuatia ni kanusho la nguvu lenye tashwishi zote
 
Dar es Salaam. Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2019 inaonyesha kwa ujumla maendeleo ya binadamu nchini kwa mwaka 2018 yalirudi nyuma kwa asilimia 24.9, ikilinganishwa na mwaka 2017.
Uchambuzi katika ripoti hiyo umezingatia hali ya kutokuwapo usawa katika mazingira ya kuzaliwa mtoto, katika kipato, katika elimu na katika tofauti kwa wenye mali na wasiokuwa nazo.
 
Hii habari CCM na Maguguli wao hawatafurahishwa nayo na kama kawaida itaonekana ni mbinu ya mabeberu kutaka kubeza na kubagaza juhudi kubwa za serikali yenye mafanikio kuliko zote zilizowahi kuwepo Tanzania aka serikali ya awamu ya 5 chini ya mzalendo-mambo leo JPM
 
wanaona wenyewe vitambi vinaongezeka peke yao wanajua wote tunamaisha kama yao,,,
Asilimia ya wengi watumishi wa serikali wametokea kwenye familia zenye uwezo hasa kwenye ngazi za juu,,,
Kwa mtoto wa mkulima endelea kulima shamba ndiyo kipaji chenu mlicho pewa na Mungu,,,
Wenye pesa ndiyo watakula national cake na masikini atakula ugali kwa maharage

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2019 inaonyesha

“Takwimu zinakinzana na uhalisia unaoendelea katika uwekezaji katika sekta ya elimu, pamoja na huduma mbalimbali za kijamii,”

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Ole Ngurumwa alisema maendeleo ya watu yanatakiwa kwenda sambamba na maendeleo ya vitu.

“Maendeleo ni sehemu ya haki za binadamu kwa hiyo ni vyema Serikali ikakumbuka kuweka uwiano sawa katika maendeleo ya watu na vitu,” alisema.
Mimi nakubaliana na hoja za THRDC kuwa maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu na sio maendeleo ya vitu.

P
 
Huyu yuuenidiipii hamjui stone? amuulize zito msaliti tulishaambiwa anapigwa kichwani alafu kazi inaendelea polisi wanajua msaliti hufanywaje
 
Chini ya utawala wa Jiwe lazima yarudi nyuma. Huyu mtu hata basics za uchumi tu hana.

Mwache azidi kuongeza juhudi za kuhamishia Simba Chato. Wenzake wenye kampuni za utalii wanawambia wazungu simba wa Chato ni "tamed"
 
Mimi nakubaliana na hoja za THRDC kuwa maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu na sio maendeleo ya vitu.

P
Siku zote watu hutumia vitu na vitu haviwezi kuwatumia watu. Lazima watu wawe na elimu ambayo ndiyo chanzo cha maendeleo yao kisha wataendeleza vitu ambavyo vitawarahihishia kusonga mbele kwenye maendeleo. Kwa kuwa hatujaendelea kielimu viongozi wetu wanautumia udhaifu wetu kwa kufanya manunuzi ya vitu vipya huku sisi tukishangilia kwa mtindo wa kipya kinyemi bila kujua kuwa shida zetu zipo palepale au zinaongezeka.
 
Mimi nakubaliana na hoja za THRDC kuwa maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu na sio maendeleo ya vitu.

P
Dah, kumbe hata wewe unalifahamu hilo. Well-done....!!!!
 
Inawezekana ni kweli, maana kwenye circle yangu...zamani kidogo tulikuwa tunacheza mchezo wa kuwekeana pesa, unaweka 2m monthly....lakini sasa hali tete....imeshuka mpaka laki 5...na bado kunadalili ya kushuka zaidi round ikiisha.
Maana biashara haziendi...Mungu atusaidie.
Kwa sasa hali ya oesa ni ngumu, utajua hilo kwa jinsi watu wanavyoomba pesa.

Hata wale ambao hawakuwa na tabia hiyo.

Ukisoma ripoti ya BOT ya October 2019, inasema mapato ya exports za kilimo kwa mwaka mmoja ulioishia August 2019 yamepungua kwa 55%, kwa kiasi kikubwa kutokana na serikali kuingilia biashara ya korosho, zao linaloingiza mapato kuliko yote.

Kwenye biashara na utalii, serikali ina tamaa ya kodi, kiasi kwamba inapanga kodi kubwa sana ambazo zinaikosesha mapato. Wapanga kodi wanakuwa kama hawajui Arthur Laffer's curve kwamba unaweza kuongeza mapato kwa kupunguza kodi.

Kika kitu kinaendeshwa kisiasa, wataalam wanapewa amri kutoka juu za wanasiasa, utaalamu hausikilizwi.

Lazima maisha yawe magumu kwa wengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkurugenzi wa UNDP Tanzania awajibishwe kwa kuupotosha umma wa watanzania pia Tanzania ivunje uhusiano na UNDP mpaka hapo itakapoomba radhi.
Maisha ya watanzania kwa sasa ni mazuri zaidi na biashara zao zimekua zaidi kuliko wakati wowote yangu Uhuru.
Hajui kwamba nchi hii in donor country
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom