Ripoti: Uchumi unakua, umasikini unaongezeka

Mkuu umenena mambo mazito sana sijui wanajf na wenyewe watakuwa wavivu kusoma hizi data ulizo shuka nazo hapa! Na kuacha hii mada ipotee kimya kimya bila kucomment. Ushauri wangu kwa mkuu moderator plz iingize hii hoja kwenye Tanzania 2010-2015 mkuu hongera sana...

Nimekubali Chadema wanavichwa big sana god be blessing u, mpe hi kamanda Lema, tunakubali kazi zake, mwambie tunamsubiri akitua UK... Tutajumuika wabongo wengi kujadili naye mambo ya msingi ya arashu, pia naomba nipatie namba yake
 
mkuu post yako nzuri lakini ndefu kweli kweli, sijui kama itapata wasomaji wa kutosha labda uipunguze asilimia 90

ni kweli post nefu ila inaonesha uvivu wako wa kujua mambo

Ndio maana wazungu wengi wa zamani walieneza propaganda kwao ukitaka kumficha mwafrika mwandikie
 
ulicho nena hapo uko sawa wasawia mkuu, ukiwa na serikali yenye mfumo mzuri kwa mahitaji ya wananchi wake hakika ni lazima utashinda vita ya umasikini wa kila mtu mmoja mmoja, naomba niwape data kidogo kwa mama mmoja wa nchini kenya kama ifuatavyo.

Miaka nane iliyopita, Mama Njoki – kama ambavyo Njuguna anajulikana zaidi kutokana na jina la mmoja wa watoto wake watano – anasema alikuwa mke wa nyumbani katika Wilaya ya Kiambu Katikati mwa Kenya. Mume wake ni mhasibu, ambaye anaingiza kiasi cha kutosha kama kipato cha kaya.

Leo hii, anamiliki mradi wa maziwa kutokana na kuwa na ng'ombe wa maziwa 15 aina ya Friesian na Jersey, na hivyo kuzalisha maziwa kila siku kwa ajili ya kituo cha maziwa cha karibu katika kijiji chake cha Ndumberi. Mafanikio yake yalichangiwa na mfuko wa kuweka akiba na kukopa ambao ulimruhusu kujenga biashara yake.

Mama mwenye umri wa miaka 58 anafuga ng'ombe wake wa maziwa ambao wanazalisha zaidi kidogo ya lita 100 kila siku, katika kipande kidogo cha ardhi yenye ukubwa wa mita za mraba elfu moja. Katika kipande kidogo cha ardhi kinachosalia kuna mbuzi wachache na kuku.

"Nilichonacho leo hii kinawezekana kwa mke wa nyumbani yoyote yule ambaye anaingiza angalau shilingi za Kenya 100 Kenya (dola 1.25) kwa siku kwa ajili ya bajeti ya chakula cha familia. Anachohitaji kufanya ni kuokoa sarafu chache kutokana na bajeti ya chakula na kuiweka katika vikundi cha kuweka akiba, ili apate angalau shilingi 200 ifikapo mwishoni mwa mwezi," anasema Mama Njoki.

Mtaji unafungua fursa

Anarudia tena ushauri ambao yeye mwenyewe aliukubali miaka nane iliyopita kutoka kwa ofisa wa taasisi ya kutoa mikopo midogo ijulikanayo kama Pamoja Women Development Program (PAWDEP), alipojiunga na wanawake wengine 39 katika kijiji chao na kuanzisha kikundi kijulikanacho kama Consolata Self Help Group.

"Tulisajili kikundi hicho kama shirika lililojikita katika jamii, na kukihusisha mara moja na taasisi ya kutoa mikopo midogo, ili tuwe na jukwaa la benki kwa ajili ya kuweka akiba," anasema Mama Njoki.

Kila mwanachama wa kikundi cha Consolata anaweka sawa na dola 2.50 katika mfuko kila mwezi. Wanachama wanaowakilisha wazo zuri la kibiashara wanaweza kukopa fedha kutokana na akiba waliyoweka kwa riba ya asilimia tano; mkopo huo unalipwa mwishoni mwa miezi mitatu.

Mikopo ya wanachama ni asilimia 60 tu ya mtaji ambao wamewekeza katika kikundi cha kuweka akiba, na kiasi kinachobaki kinasaidia kulipia madeni kama wakishindwa kulipia mikopo.

Mikopo ya wanachama inatolewa mara mbili na nusu ikilinganishwa na mtaji unowekezwa kwenye kikundi; kwa mfano, mwanachama ambaye amekusanya dola 100 katika akiba anaweza kupata mkopo wa dola 250. Kwa njia hii asilimia 40 ya mkopo unahakikishwa dhidi ya fedha ambazo mkopaji anaingiza katika mpango huo kama atashindwa kurejesha.

"Tuliwahamasisha kuendelea kufanya majaribio kwa kukopa mara kwa mara na kuwekeza katika biashara ndogo ndogo," anasema Rachel Wanyoike, mshauri wa mikopo midogo midogo ambaye kwa sasa anafanya kazi kama Mkuu wa Rasilimali Watu katika PAWDEP. "Wakati huo huo, tuna kiasi kikubwa cha maofisa mikopo ambao wanaendelea kuwafunza jinsi ya kuwekeza fedha kwa njia ambayo itasaidia kulipia mikopo yao kwa mafanikio."

Mkopo wa kwanza wa Mama Njoki, mwaka 2003, ulikuwa wa dola 250 ambao aliutumia kuanzisha ufugaji wa ndani na kufuga ng'ombe wake mmoja. Baba mkwe wake alimpatia ng'ombe alipoolewa, lakini kwa miaka amekuwa akifuga ng'ombe mmoja tu. Mkopo ulitumiwa kuondokana na mfumo wa ufugaji wa jadi na kuanza kufuga ng'ombe ndani, na kula majani yaliyoletwa kutoka mahali pengine – na Mama Njoki pia aliwalisha taka kutoka kiwanda cha karibu cha bia.

"Baada ya kupatiwa mafunzo ya mikopo midogo, nilikubali kuwa wanyama wanahitaji uwekezaji ambao unakua," alisema.

Aliweza kulipia mkopo wa kwanza kutokana na fedha anazopata kutokana na kuuza maziwa halafu akakopa tena dola 625 kununua ng'ombe wa pili. Uuzaji wa maziwa ulilipia deni, na kiasi cha mikopo mikubwa kutoka kikundi cha Consolata ilijenga biashara kwa kasi kubwa.

"Hadi mwisho wa mwaka 2009, Mama Njoki alikuwa ameshaongeza idadi ya ng'ombe wa maziwa na kufikia 14, ambao tulidhani walitosha kuwa dhamana ya mkopo wake binafsi," alisema Wanyoike.

Kwa kuwa na dhamana hii, Njuguna alipata mkopo binafsi wa dola 12,500 kutoka PAWDEP, ambao unalipwa kwa miaka mitatu, ambapo anamfanya kuchanganya ufugaji wa mifugo mbalimbali – amenunua mashamba matatu katika eneo la mjini la Ruiri, nje kidogo mwa mji wa Nairobi.

"Tunatarajia kukamilisha kulipia mkopo mapema mwaka kesho. Na kwa kuwa na viwanja hivyo, tutakuwa na furaha kutoa hadi au zaidi ya shilingi milioni tano (dola 37,500) kuwezesha kuendeleza viwanja vyake," alisema mshauri wa mikopo midogo.

Wanachama wengine wa kikundi cha Consolata wamepata maendeleo ya kasi, kwa kuanzisha biashara ndogo ndogo au kilimo.

"Kila mmoja wetu angalau anamiliki ardhi. Wengi wetu tumewekeza katika ardhi, wakati wengine wameanzisha biashara," anasema Mama Njoki.

Pamoja na kwamba Njuguna alianza kwa mkopo wa dola 250, Wanyoike anashauri kuwa kukopa kiasi kidogo cha fedha kunaweza kusaidia kuvutia wafanyabiashara wa kike kuwa na msingi bora.

Kutathmini muktadha

PAWDEP kwa sasa inafanya kazi na miradi ya kuweka akiba ambayo jumla ya wanachama wake wanafikia 48,000 ambao ni wanawake kutoka majimbo ya Kati, Mashariki, Bonde la Ufa na Nairobi. Kuna taasisi kama hizo nchini Kenya, zinazosaidia wanawake na vijana kukuza upatikanaji wa mikopo.

Ripoti ya mwaka 2010 iliyochapishwa na shirika la misaada la kimataifa la ActionAid - "Fertile Ground: How Governments and Donors Can Halve Hunger" – iliyojikita katika takwimu zilizokusanywa nchini Kenya, Uganda na Malawi inapendekeza kuwa aina hii ya msaada kwa wakulima wadogo wanawake ingepunguza nusu ya njaa katika bara la Afrika ifikapo mwaka 2015.

Mama Njoki alikuwa na bahati ya kuwa na mume anayemuunga mkono. "Katika kundi lao kuna idadi kubwa ya wanawake ambao wanaingiliwa mara kwa mara na waume zao. Baadhi yao wamelazimika kununua viwanja kwa siri na sasa wanaviendeleza bila waume zao kujua," anasema Wanyoike.

Wanaume wenye hasira, anasema Wanyoike, zaidi ya mara moja wamewahi kuvamia ofisi za PAWDEP wakidai wanawake wao wapatiwe akiba walizojiwekea.

Ushauri wa kuweka akiba kidogo kidogo kutokana na bajeti ya kaya ambayo inaweza kutumiwa na wengine kuchukua mikopo ni jambo zuri, lakini Esther Njuguna pia alipata rasilimali nyingine ambazo mamilioni ya wanawake wengi ambao ni uti wa mgongo wa kilimo barani Afrika wanaweza kuwa na ndoto ya kufanya hivyo.

Alimiliki ng'ombe wake, na aliweza kukodisha ardhi ya kupanda chakula cha mifugo ili kulisha mifugo yake. Kijiji cha Ndumberi kina kituo cha kusindika maziwa ambacho kilimpatia Mama Njoki faida na kuwa na soko la wazi la mazao yake ya mifugo.

Wanawake wengi wa Afrika wangefaidika na mikopo ambayo kwa sasa inapatikana kwa shida kutokana na sheria na mila na desturi za kumiliki ardhi, mahusiano ya nyumbani; wanaume na wanawake wa vijijini wanakabiliwa na matatizo ya miundombinu duni ambayo inawanyima maji, masoko, au hata ushauri mzuri na teknolojia za kilimo.

Wakati mikopo midogo haiwezi kutengana na sababu nyingine, inachangia kwa kiasi kikubwa katika kufanya rasilimali nyingi kupatikana kwa watu wa vijijini. (END/2011)
 
Mkuu kilewo hongera zako kwa kutoa komment ya kueleweka,

Hii imekaa vizuri kwa kiongozi kama wewe kujakuchangia moja kwa moja bila kuficha jina lako, ni jinsi gani inaonyesha CDM imejaliwa vichwa vya kuchambua mambo na kufuatili ya ndani na ya nje hongereni sana CDM kuwa na kizazi cha kuchambua maswala nyeti ya kitafa keep it up KILEWO
 
Hii mada ni nzuri ingependeza sana kama ingewekwa kwenye gazeti ila policy makers waifanyie kazi
 
Kama kawaida wabongo tunapenda vitu vya mkato. We don't want to read much. Tunapenda vitu vya juu juu. Probably ndio maana tunasaini mikataba mibovu b'se we dont care to read the small details.

Acha mbwembwe EMT, unafikiri watu wanakwenda kazini au internet Cafe kusoma Jamii Forum tu, NO. Hii ni sehemu tu kupata taarifa au burudani. Kwa hiyo huwezi kusoma thread moja kwa saa nzima. Huo utakuwa ni wizi mkubwa wa muda wa kazi kwani sasa hivi ni muda wa kazi labda kama upo likizo au huna kazi. Sasa hao wanosaini mikataba unafikiri ni wazembe wa kusoma? Kwa taarifa yako wanasoma vizuri hii mikataba kwa lengo la kutafuta upenyo wa kuiba kupitia hiyo mikataba. Wanajua wanchofanya na ni wasomi wazuri kabisa ambao wanatumia huo udhaifu wa hukumu yako kukuibia wewe na nchi yetu. Amka tafadhari
 
UNDP inatoa taarifa juu ya "The concentrated poverty". Yaani umaskini wa kutisha, kwa bahati mbaya Tanzania ni moja ya nchi zilizo chini ya mstari mwekundu wa umaskini ambao wao wanaita "below poverty level" au absolutely poverty". Huu ni umaskini unaozidi kawaida ya umaskini, waweza kuita umaskini sana, au umaskini zaidi, ama umaskini mno, lakini yote hayo yanaashiria neno moja tu nalo ni kwamba umaskini unaoikabili nchi yetu ni sawa kabisa na ugonjwa wa ukimwi kwa maana ya kwamba umaskini wetu sasa hautibiki.

KATIKA kuufafanua umaskini, mtu aweza kuuweka ama kuugawanya katika mafungu mawili, umaskini wa nchi (au taifa) na umaskini wa watu au "mass poverty" yaani walio wengi katika ujumla wao. Enzi za mkoloni nchi yetu ilikuwa na umaskini wa watu tu yaani "individuals" lakini haikuwa na umaskini wa dola kama uliopo sasa ambapo takribani asilimia 50 ya bajeti ya serikali inatoka kwa wahisani.

Katika uhalisi wa mambo nchi yetu ni ombaomba, hata waliyodai Mkapa alirudisha heshima ya Tanzania kimataifa sijui wanatumia vigezo gani kwani katika ukweli wa maisha hakuna omba omba yeyote aliyepata kuheshimika. Heshima ya Tanzania italetwa kwa kujitegemea na kujitosheleza, kwanza kwa chakula na baadaye kwa mahitaji mengine, yaliyo muhimu kwa taifa. Enzi za mkoloni Tanganyika ilikuwa nchi ya kwanza kwa uzalishaji wa mkonge ambapo ilitoa asilimia 28 ya mahitaji ya dunia ukiacha mazao mengine kama nyonyo, karanga, pamba na ngozi, na kahawa.

Kwa mapato hayo serikali ya mkoloni haikuwa lofa iliweza kujenga mabarabara, njia za mawasiliano, na kutoa elimu bora kwa hao waliobahatika kusoma. Kwa maneno mengine walau serikali iliweza kujitegemea, lakini sasa kila kitu kiko nyang'anyang'a na hoi bin taabani. Hakuna mradi wowote wa kitaifa ambao ungeweza kutoa ajira ya maelfu kama ukoloni, hakuna watu wabunifu ndani ya hiyo kada ya watawala badala yake umahili wao uko kwenye kudhibiti wapinzani na kuendesha mizengwe ya kuwawezesha kubaki madarakani. Wao watawala, ushindi wanaouona muhimu ni ule tu wa uchaguzi mkuu. Ule ukweli kwamba wao baada ya kuwashinda wapinzani, nao wameshindwa na umaskini hawaujali wala hawaoni aibu.

Inapotokea kwamba dola imekuwa maskini hadi kuendeshwa kwa misaada toka nje ya nchi na watu (wananchi) nao wakawa maskini hadi kufikia kiwango cha kushindwa kufanya lolote na kubaki kama walemavu kungojea kudra za Mungu basi hapo kuna tatizo mara mbili yaani tatizo la umaskini na tatizo la watu wenyewe. Lakini papo hapo viongozi wakuu wa serikali wanapokuwa ni matajiri kuliko serikali yao, basi hapo ndipo kinapoinuka kitendawili cha uongozi bora.

Mawaziri walio matajiri, wakuu wa mikoa walio tajiri, makatibu wakuu walio tajiri, na wabunge walio tajiri, je, wamefanya biashara gani madarakani hadi wakaupata utajiri walio nao? Kisha je wameulipia kodi ya mapato? Maana inaonyesha kwa utajiri wao basi wanavyo vyanzo vya uhakika vya mapato na kwa kuwa katika nchi yetu kuna sera ya kutoza kodi ya mapato (wakati mwingine hata kabla ya mtu hajapata) basi na wao watoe mchanganuo wao kuthibitisha kwamba nao ni raia wema wanaoilipa serikali mapato sawa na sheria za nchi zinavyoagiza!!

Kitendawili hiki ni kigumu kuteguliwa ingawa jibu lake liko wazi, kitendawili chenyewe ni kwamba hapa kuna nchi yenye rasilimali za kila namna lakini bado nchi hiyo ni maskini ya kupindukia duniani, nchi hiyo ilipotawaliwa na Wakoloni haikuwa maskini kama ilivyotawaliwa na watawala waliopo sasa, wakati nchi ni maskini, na watu ni maskini mno. Viongozi ni matajiri wa kupindukia. Je kuna mchezo gani umechezwa kuyaleta haya? Jibu wanalo wenyewe watawala, wanajua jinsi walivyofanya hata kuupata utajiri walio nao sasa isipokuwa wanajifanya hawajui wafanye nini ili kuondoa umaskini kwa nchi yao na watu wao, kwa kuwa akili yao imeishia kujitajirisha wao na siyo nchi. Vijana wapatao laki nne wanamaliza elimu ya msingi kila mwaka lakini uongozi uliopo madarakani haujui ufanye nini au uwapeleke wapi,hivyo baada ya kutoka darasani wanaishia "vijiweni".

Viwanda vingi vimekufa, na mashirika ya umma mengi yameanguka waliokuwa wafanyakazi nao inabidi waungane kwenye vijiwe na vijana wao wanaotoka darasani hadi vijiweni. Kutokana kukosekana sera ya uhakika ya kilimo, kilimo kimebaki duni toka enzi za Mwalimu Nyerere hadi sasa na kwa uduni huo.Kilimo kimejiunga kwenye siasa na kutengenezewa majina mazuri ya kisiasa kama ''KILIMO KWANZA'' wakati uhalisia sio huo. Tumebaki kudanganyana tu ili mradi siku iende. Hakuna elimu ya kuwaelimisha wananchi hasa vijana wajue umuhimu wa kilimo. Mikopo ya Kikwete inatolewa kwa wafanyabiashara badala ya wakulima, na wafanyabiashara wenyewe sio wahitaji halisi wa mikopo hiyo kwania tayari walishakuwa na mitaji ya kutosha. Wakulima wanaachwa kama walivyo, vijana wanaona kilimo kama hakiwezekani kwani hakiwaondoi katika dimbwi la umasikini wa kutupwa. Wakulima hawapendelewi wala hawajengewi mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao kama wanavyofanyiwa wafanyabiashara, hivyo vijana wanaona ni bora kufanya biashara ili wajiingize kwenye mazingira mazuri kuliko kiliko kulimo. Kizazi kipya cha vijana wanakimbia kilimo vijijini na kuja mjini kubahatisha maisha mapya. Wale vijana wanaozaliwa mijini, wao wanakimbilia majuu (wanazamia meli), kizazi cha kale cha wakulima kinazeeka na kudhoofu na hakuna wa kuziba pengo, hivyo usemi wa kwamba Tanzania ni nchi ya wakulima na wafanyakazi umebaki kauli za maandishi tu, lakini katika uhalisi wa mambo Tanzania haina wakulima ndiyo maana ni nchi inayoumwa njaa kila mwaka. Pia Tanzania si nchi ya wafanyakazi maana hakuna kazi nyingi za kufanya kwa sababu hakuna viwanda wala makampuni au mashirika ya kutoa ajira.

Yale yaliyokuwepo yameuawa na watawala waliopo madarakani. Sasa inabidi wote wenye kutazama mambo katika umakini wajiulize nchi ambayo imepukutisha maelfu ya askari wake toka jeshini baada ya kulazimishwa na sera za IMF za kuwa na jeshi dogo, na hivyo kuwalazimisha askari hao kujiunga na walalahoi wengine vijiweni, nchi ambayo imeua mfumo wake wa elimu na kuwafanya vijana wake wasipate elimu ya kuwasaidia kuishi badala yake vijana wake wakawa na elimu ya nadharia ambayo baada ya mtu kumaliza shule (kutoka darasani) anashindwa kuitumia (to apply) aidha hapo kijijini au mjini, mwisho anaishia kijiweni kuvuta bangi au kulamba unga. Ndio vijana hawa wanalaghaiwa na wafanyabiashara wakubwa kujiingiza katika biashara haramu.

Nchi ambayo inashindwa kuzalisha kizazi kipya cha wakulima na waliopo inawaacha wawe wachovu zaidi kwa kuvuruga mfumo wa masoko ya mazao yao na kuwasababishia umaskini usiomithilika, nchi ambayo haina mpango wowote wa kuongeza ajira kwa maelfu ya wananchi wake, nchi ambayo imeua mfumo wa utoaji haki na kusababisha magereza kufurika wafungwa na mahabusu, nchi ambayo haina mikakati yoyote ya kuwatumia wafungwa kuzalisha mali ili kujikimu wawapo magerezani badala ya kutegemea pesa kutoka serikalini, na mahakama zake kuwa na mafuriko ya kesi za jinai. Je nchi ya namna hiyo ina uhakika gani wa kudumisha amani yake wakati inayaacha mabomu yanayongojea wakati wake ufike yalipuke?

Kwa hakika nchi yetu ni mfano wa mtu anayetembea sambamba na gema ambaye kuna uwezekano wa kutumbukia wakati wowote. Hata hivyo ieleweke wazi kwamba tatizo la umaskini ni matokeo tu ya uzembe wa watawala, endapo nchi itapata utawala ulio makini na ulio dhamiria kuondoa tatizo hili, umaskini wa Tanzania unaweza kufutika baada ya muda mfupi na Tanzania ikawa miongoni mwa nchi tajiri na zenye uchumi imara au "economic giant" katika dunia hii.

Mtu hawezi kuamini akielezwa kwamba umaskini wa Tanzania ni sera ya makusudi kabisa ambayo lengo lake kuu ni kudhibiti wananchi na kuwawezesha watawala kuendelea kudumu madarakani hadi siku ya kufa. Watawala wa nchi hii wanajua wazi kwamba wakiwaondoa watu wao katika dimbwi la umasikini hawawezi kutawalika na pia hawawezi kuburuzwa, kwa hiyo umaskini ni silaha yao nzuri ya kuendelea kutawala.

Fikiria kama Watanzania wangekuwa na elimu, shibe, na utajiri, ni wazi kwamba asingekuweko mgombea yeyote wa ubunge, urais, au udiwani wa kuhonga watu soda, pilau, khanga au pombe za kienyeji. Pasingekuweko na mtu wa kuuza shahada yake ya kupigia kura kwa Tshs: 2,000. Hapo ndipo yangekuweko mashindano ya sera na programu za kuendeleza nchi, majimbo, maeneo, au mitaa.

Kwa ajili hiyo umaskini kama ulivyo katika nchi hii ni kikwazo cha mengi, ni kikwazo dhidi ya demokrasia, ni kikwazo dhidi ya utawala bora kutokana na ukweli kwamba wezi wa mali za umma na walaji rushwa na mafisadi ndio wenye tabia za kuwanunua wapiga kura walio hoi kwa njaa na umaskini wa kupindukia. Pia umaskini ni kikwazo dhidi ya mabadiliko yoyote.

Sasa kwa bahati mbaya tatizo la umaskini haliwezi kuondoshwa na utawala unaoona kwamba kuwatawala watu masikini ni raha zaidi kuliko kuwatawala watu walioridhika kimaisha, wakoloni walijitahidi kuwagawa wananchi ili wabaki hawaelewani kati ya walionacho na wasionacho, waliosoma na wasiosoma ili wapate kinga ya kuwafanya waendelee kutawala bila shida. Wao walihakikisha wananchi wanaowatawala wanabaki wajinga. Wagonjwa, na maskini ili wasiwe na ubavu wa kuwaondoa madarakani. Cha kushangaza ni kwamba takribani miaka 48 (2009-1961) tangu tupate uhuru wetu kutoka kwa Mwingereza watawala wetu bado wanaendeleza mbinu za wakoloni za kutawala za kutufanya tuwe wajinga, masikini na tunaosumbuliwa na magonjwa kila wakati.

Kwa mfano Maasi ya Maji Maji 1905-1907 yalifanya Mjerumani kuyaelewa makabila ya kusini kwamba ni ya watu jeuri na wagumu kutawalika endapo wataachiwa kutulia pasipo kuvurugwa na njaa, umaskini au magonjwa alichokifanya ni kutokupeleka maendeleo makubwa kama vile reli, shule, na mahospitali makubwa. Serikali ya TANU pia ilifuata nyayo za Mjerumani, ilijua wazi kwamba watu wa kusini, Wangoni, Wapangwa, wamatengo, Wamakua, Wamwera, Wanyasa, Wamakonde, Wayao, na Warufiji kwa asili yao ni watu jeuri na wagumu kuburuzwa endapo wataachiwa wawe na uimara wowote ule aidha uimara wa kiuchumi, au uimara wa kielimu au uimara wa kuwa na mshikamano, hivyo basi sera ya ''gawanya utawale'' ikabidi iendelezwe na juu ya hiyo iongezwe sera ya kuwafanya wawe maskini zaidi na pia kuwatenga ama kuwabomolea misingi yote ya maendeleo kwani kama wangekuwa na maendeleo walau nusu tu ya yale yaliyoko kaskazini ingekuwa vigumu kutawalika. Kwa hiyo kwa makusudi kabisa reli ya TAZARA ambayo kimsingi ingekuwa kama ilivyo reli ya kati kwa mikoa ya kusini ikapitishwa porini badala ya kupita Rufiji, Mtwara,Lindi, Songea hadi Itungi Port (Kyela) na kuingia Zambia. Reli ilikwepeshwa maeneo hayo ili tu kuzuia kasi ya maendeleo ya kusini na pia kuzuia kukua kwa uchumi wa kusini.

Kusini ambayo ina rasilimali nyingi na utajiri mwingi kuliko kaskazini na pengine maeneo mengine yote ya nchi hii sasa imekuwa chemi chemi ya kutoa Wamachinga kwa sababu tu watoto wake wamenyimwa elimu. Rasilimali zake zinaoza na huenda siku za usoni watapewa wageni kama ilivyotokea kwa SongoSongo na machimbo ya Alexandrite huko Tunduru.
Baadhi ya wasomi wachache wa kusini walipewa nyadhifa katika serikali ili ziwe kama takrima na uchawi wa kuloga akili zao wasijejali tena maendeleo ya kusini wala kuwahurumia ndugu zao ambao wanahitaji ukombozi kwa njia ya maendeleo.
Umasikini wa Tanzania ni wa Kujitakia
Africar T Kagema

UNDP inatoa taarifa juu ya "The concentrated poverty". Yaani umaskini wa kutisha, kwa bahati mbaya Tanzania ni moja ya nchi zilizo chini ya mstari mwekundu wa umaskini ambao wao wanaita "below poverty level" au absolutely poverty". Huu ni umaskini unaozidi kawaida ya umaskini, waweza kuita umaskini sana, au umaskini zaidi, ama umaskini mno, lakini yote hayo yanaashiria neno moja tu nalo ni kwamba umaskini unaoikabili nchi yetu ni sawa kabisa na ugonjwa wa ukimwi kwa maana ya kwamba umaskini wetu sasa hautibiki.

KATIKA kuufafanua umaskini, mtu aweza kuuweka ama kuugawanya katika mafungu mawili, umaskini wa nchi (au taifa) na umaskini wa watu au "mass poverty" yaani walio wengi katika ujumla wao. Enzi za mkoloni nchi yetu ilikuwa na umaskini wa watu tu yaani "individuals" lakini haikuwa na umaskini wa dola kama uliopo sasa ambapo takribani asilimia 50 ya bajeti ya serikali inatoka kwa wahisani.

Katika uhalisi wa mambo nchi yetu ni ombaomba, hata wanaodai Mkapa amerudisha heshima ya Tanzania kimataifa sijui wanatumia vigezo gani kwani katika ukweli wa maisha hakuna omba omba yeyote aliyepata kuheshimika. Heshima ya Tanzania italetwa kwa kujitegemea na kujitosheleza, kwanza kwa chakula na baadaye kwa mahitaji mengine, yaliyo muhimu kwa taifa. Enzi za mkoloni Tanganyika ilikuwa nchi ya kwanza kwa uzalishaji wa mkonge ambapo ilitoa asilimia 28 ya mahitaji ya dunia ukiacha mazao mengine kama nyonyo, karanga, pamba na ngozi, na kahawa.

Kwa mapato hayo serikali ya mkoloni haikuwa lofa iliweza kujenga mabarabara, njia za mawasiliano, na kutoa elimu bora kwa hao waliobahatika kusoma. Kwa maneno mengine walau serikali iliweza kujitegemea, lakini sasa kila kitu kiko nyang'anyang'a na hoi bin taabani. Hakuna mradi wowote wa kitaifa ambao ungeweza kutoa ajira ya maelfu kama ukoloni, hakuna watu wabunifu ndani ya hiyo kada ya watawala badala yake umahili wao uko kwenye kudhibiti wapinzani na kuendesha mizengwe ya kuwawezesha kubaki madarakani. Wao watawala, ushindi wanaouona muhimu ni ule tu wa uchaguzi mkuu. Ule ukweli kwamba wao baada ya kuwashinda wapinzani, nao wameshindwa na umaskini hawaujali wala hawaoni aibu.

Inapotokea kwamba dola imekuwa maskini hadi kuendeshwa kwa misaada toka nje ya nchi na watu (wananchi) nao wakawa maskini hadi kufikia kiwango cha kushindwa kufanya lolote na kubaki kama walemavu kungojea kudra za Mungu basi hapo kuna tatizo mara mbili yaani tatizo la umaskini na tatizo la watu wenyewe. Lakini papo hapo viongozi wakuu wa serikali wanapokuwa ni matajiri kuliko serikali yao, basi hapo ndipo kinapoinuka kitendawili cha uongozi bora.

Mawaziri walio matajiri, wakuu wa mikoa walio tajiri, makatibu wakuu walio tajiri, na wabunge walio tajiri, je, wamefanya biashara gani madarakani hadi wakaupata utajiri walio nao? Kisha je wameulipia kodi ya mapato? Maana inaonyesha kwa utajiri wao basi wanavyo vyanzo vya uhakika vya mapato na kwa kuwa katika nchi yetu kuna sera ya kutoza kodi ya mapato (wakati mwingine hata kabla ya mtu hajapata) basi na wao watoe mchanganuo wao kuthibitisha kwamba nao ni raia wema wanaoilipa serikali mapato sawa na sheria za nchi zinavyoagiza!!

Kitendawili hiki ni kigumu kuteguliwa ingawa jibu lake liko wazi, kitendawili chenyewe ni kwamba hapa kuna nchi yenye rasilimali za kila namna lakini bado nchi hiyo ni maskini ya kupindukia duniani, nchi hiyo ilipotawaliwa na Wakoloni haikuwa maskini kama ilivyotawaliwa na watawala waliopo sasa, wakati nchi ni maskini, na watu ni maskini mno. Viongozi ni matajiri wa kupindukia. Je kuna mchezo gani umechezwa kuyaleta haya? Jibu wanalo wenyewe watawala, wanajua jinsi walivyofanya hata kuupata utajiri walio nao sasa isipokuwa wanajifanya hawajui wafanye nini ili kuondoa umaskini kwa nchi yao na watu wao, kwa kuwa akili yao imeishia kujitajirisha wao na siyo nchi. Vijana wapatao laki nne wanamaliza elimu ya msingi kila mwaka lakini uongozi uliopo madarakani haujui ufanye nini au uwapeleke wapi,hivyo baada ya kutoka darasani wanaishia "vijiweni".

Viwanda vingi vimekufa, na mashirika ya umma mengi yameanguka waliokuwa wafanyakazi nao inabidi waungane kwenye vijiwe na vijana wao wanaotoka darasani hadi vijiweni. Kutokana kukosekana sera ya uhakika ya kilimo, kilimo kimebaki duni toka enzi za Mwalimu Nyerere hadi sasa na kwa uduni huo.Kilimo kimejiunga kwenye siasa na kutengenezewa majina mazuri ya kisiasa kama ''KILIMO KWANZA'' wakati uhalisia sio huo. Tumebaki kudanganyana tu ili mradi siku iende. Hakuna elimu ya kuwaelimisha wananchi hasa vijana wajue umuhimu wa kilimo. Mikopo ya Kikwete inatolewa kwa wafanyabiashara badala ya wakulima, na wafanyabiashara wenyewe sio wahitaji halisi wa mikopo hiyo kwania tayari walishakuwa na mitaji ya kutosha. Wakulima wanaachwa kama walivyo, vijana wanaona kilimo kama hakiwezekani kwani hakiwaondoi katika dimbwi la umasikini wa kutupwa. Wakulima hawapendelewi wala hawajengewi mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao kama wanavyofanyiwa wafanyabiashara, hivyo vijana wanaona ni bora kufanya biashara ili wajiingize kwenye mazingira mazuri kuliko kiliko kulimo. Kizazi kipya cha vijana wanakimbia kilimo vijijini na kuja mjini kubahatisha maisha mapya. Wale vijana wanaozaliwa mijini, wao wanakimbilia majuu (wanazamia meli), kizazi cha kale cha wakulima kinazeeka na kudhoofu na hakuna wa kuziba pengo, hivyo usemi wa kwamba Tanzania ni nchi ya wakulima na wafanyakazi umebaki kauli za maandishi tu, lakini katika uhalisi wa mambo Tanzania haina wakulima ndiyo maana ni nchi inayoumwa njaa kila mwaka. Pia Tanzania si nchi ya wafanyakazi maana hakuna kazi nyingi za kufanya kwa sababu hakuna viwanda wala makampuni au mashirika ya kutoa ajira.

Yale yaliyokuwepo yameuawa na watawala waliopo madarakani. Sasa inabidi wote wenye kutazama mambo katika umakini wajiulize nchi ambayo imepukutisha maelfu ya askari wake toka jeshini baada ya kulazimishwa na sera za IMF za kuwa na jeshi dogo, na hivyo kuwalazimisha askari hao kujiunga na walalahoi wengine vijiweni, nchi ambayo imeua mfumo wake wa elimu na kuwafanya vijana wake wasipate elimu ya kuwasaidia kuishi badala yake vijana wake wakawa na elimu ya nadharia ambayo baada ya mtu kumaliza shule (kutoka darasani) anashindwa kuitumia (to apply) aidha hapo kijijini au mjini, mwisho anaishia kijiweni kuvuta bangi au kulamba unga. Ndio vijana hawa wanalaghaiwa na wafanyabiashara wakubwa kujiingiza katika biashara haramu.

Nchi ambayo inashindwa kuzalisha kizazi kipya cha wakulima na waliopo inawaacha wawe wachovu zaidi kwa kuvuruga mfumo wa masoko ya mazao yao na kuwasababishia umaskini usiomithilika, nchi ambayo haina mpango wowote wa kuongeza ajira kwa maelfu ya wananchi wake, nchi ambayo imeua mfumo wa utoaji haki na kusababisha magereza kufurika wafungwa na mahabusu, nchi ambayo haina mikakati yoyote ya kuwatumia wafungwa kuzalisha mali ili kujikimu wawapo magerezani badala ya kutegemea pesa kutoka serikalini, na mahakama zake kuwa na mafuriko ya kesi za jinai. Je nchi ya namna hiyo ina uhakika gani wa kudumisha amani yake wakati inayaacha mabomu yanayongojea wakati wake ufike yalipuke?

Kwa hakika nchi yetu ni mfano wa mtu anayetembea sambamba na gema ambaye kuna uwezekano wa kutumbukia wakati wowote. Hata hivyo ieleweke wazi kwamba tatizo la umaskini ni matokeo tu ya uzembe wa watawala, endapo nchi itapata utawala ulio makini na ulio dhamiria kuondoa tatizo hili, umaskini wa Tanzania unaweza kufutika baada ya muda mfupi na Tanzania ikawa miongoni mwa nchi tajiri na zenye uchumi imara au "economic giant" katika dunia hii.

Mtu hawezi kuamini akielezwa kwamba umaskini wa Tanzania ni sera ya makusudi kabisa ambayo lengo lake kuu ni kudhibiti wananchi na kuwawezesha watawala kuendelea kudumu madarakani hadi siku ya kufa. Watawala wa nchi hii wanajua wazi kwamba wakiwaondoa watu wao katika dimbwi la umasikini hawawezi kutawalika na pia hawawezi kuburuzwa, kwa hiyo umaskini ni silaha yao nzuri ya kuendelea kutawala.

Fikiria kama Watanzania wangekuwa na elimu, shibe, na utajiri, ni wazi kwamba asingekuweko mgombea yeyote wa ubunge, urais, au udiwani wa kuhonga watu soda, pilau, khanga au pombe za kienyeji. Pasingekuweko na mtu wa kuuza shahada yake ya kupigia kura kwa Tshs: 2,000. Hapo ndipo yangekuweko mashindano ya sera na programu za kuendeleza nchi, majimbo, maeneo, au mitaa.

Kwa ajili hiyo umaskini kama ulivyo katika nchi hii ni kikwazo cha mengi, ni kikwazo dhidi ya demokrasia, ni kikwazo dhidi ya utawala bora kutokana na ukweli kwamba wezi wa mali za umma na walaji rushwa na mafisadi ndio wenye tabia za kuwanunua wapiga kura walio hoi kwa njaa na umaskini wa kupindukia. Pia umaskini ni kikwazo dhidi ya mabadiliko yoyote.

Sasa kwa bahati mbaya tatizo la umaskini haliwezi kuondoshwa na utawala unaoona kwamba kuwatawala watu masikini ni raha zaidi kuliko kuwatawala watu walioridhika kimaisha, wakoloni walijitahidi kuwagawa wananchi ili wabaki hawaelewani kati ya walionacho na wasionacho, waliosoma na wasiosoma ili wapate kinga ya kuwafanya waendelee kutawala bila shida. Wao walihakikisha wananchi wanaowatawala wanabaki wajinga. Wagonjwa, na maskini ili wasiwe na ubavu wa kuwaondoa madarakani. Cha kushangaza ni kwamba takribani miaka 48 (2009-1961) tangu tupate uhuru wetu kutoka kwa Mwingereza watawala wetu bado wanaendeleza mbinu za wakoloni za kutawala za kutufanya tuwe wajinga, masikini na tunaosumbuliwa na magonjwa kila wakati.

Kwa mfano Maasi ya Maji Maji 1905-1907 yalifanya Mjerumani kuyaelewa makabila ya kusini kwamba ni ya watu jeuri na wagumu kutawalika endapo wataachiwa kutulia pasipo kuvurugwa na njaa, umaskini au magonjwa alichokifanya ni kutokupeleka maendeleo makubwa kama vile reli, shule, na mahospitali makubwa. Serikali ya TANU pia ilifuata nyayo za Mjerumani, ilijua wazi kwamba watu wa kusini, Wangoni, Wapangwa, wamatengo, Wamakua, Wamwera, Wanyasa, Wamakonde, Wayao, na Warufiji kwa asili yao ni watu jeuri na wagumu kuburuzwa endapo wataachiwa wawe na uimara wowote ule aidha uimara wa kiuchumi, au uimara wa kielimu au uimara wa kuwa na mshikamano, hivyo basi sera ya ''gawanya utawale'' ikabidi iendelezwe na juu ya hiyo iongezwe sera ya kuwafanya wawe maskini zaidi na pia kuwatenga ama kuwabomolea misingi yote ya maendeleo kwani kama wangekuwa na maendeleo walau nusu tu ya yale yaliyoko kaskazini ingekuwa vigumu kutawalika. Kwa hiyo kwa makusudi kabisa reli ya TAZARA ambayo kimsingi ingekuwa kama ilivyo reli ya kati kwa mikoa ya kusini ikapitishwa porini badala ya kupita Rufiji, Mtwara,Lindi, Songea hadi Itungi Port (Kyela) na kuingia Zambia. Reli ilikwepeshwa maeneo hayo ili tu kuzuia kasi ya maendeleo ya kusini na pia kuzuia kukua kwa uchumi wa kusini.

Kusini ambayo ina rasilimali nyingi na utajiri mwingi kuliko kaskazini na pengine maeneo mengine yote ya nchi hii sasa imekuwa chemi chemi ya kutoa Wamachinga kwa sababu tu watoto wake wamenyimwa elimu. Rasilimali zake zinaoza na huenda siku za usoni watapewa wageni kama ilivyotokea kwa SongoSongo na machimbo ya Alexandrite huko Tunduru.
Baadhi ya wasomi wachache wa kusini walipewa nyadhifa katika serikali ili ziwe kama takrima na uchawi wa kuloga akili zao wasijejali tena maendeleo ya kusini wala kuwahurumia ndugu zao ambao wanahitaji ukombozi kwa njia ya maendeleo.

Tanzania itaweza kujikomboa yenyewe kama itakuwa na viongozi wenye dhamira ya kweli ya kumkomboa mtanzania wa kawaida, ila kama tanzania ya sasa itaendelea kuwa na viongozi wenye uchu wa madaraka na kujilimbikizia mali nina uhakika miaka mingine saba ijayo tanzania itageuka kuwa na vita kali kati ya masikini na tajiri, na hii italigharimu taifa kwa miaka mingine kumi na 15 kuwa kwenye hali yake ya kawaida ya sasa.
nahii itakuwa ni fundisho kwa watawala kujua wananchi wake wapo wapi na wanataka kwenda wapi, nilazima kila mtawala aijue tanzania ya sasa badala ya kuongoza kwa mazoea, hata CHADEMA wakishika dola kesho wnapaswa kuzingatia mambo hayo, na nilazima chadema ianze kujenga mtandao mpya wa serikli yake mean watumishi wenye utashi wa kuhudumia wananchi kwa haraka, hii itaondoa mfumo wa kujiona miungu watu kama ilivyo sasa.
 
TUNAAMBIWA nchi yetu ni moja ya nchi 38 masikini sana duniani [LDCs] ikishika nafasi ya 10 toka mwisho; lakini tunaambiwa hapo hapo kwamba nchi yetu ni moja ya nchi zenye utajiri mkubwa wa raslimali duniani; hususan madini ya dhahabu na mengineyo.
Watanzania ni masikini wa kutupa, na sasa ni masikini zaidi kuliko siku ya Uhuru [Desemba 9, 1961]. Wakati huo huo, viongozi wake wanathubutu kusimama juu ya paa kuita kwa nguvu zote wawekezaji [waporaji] kutoka nje kuja kupora kilichomo, chini ya mikataba mibovu ya uwekezaji. Ni upofu gani huo?
Moja ya sheria mbovu zenye kuruhusu uporaji wa raslimali za Taifa zilizotungwa na Bunge linalodai kutetea maslahi ya wananchi [wakati ukweli ni kinyume chake], ni Sheria ya Madini ya 1998 ambayo imekuwa ni kichaka cha wageni wachache wasio waaminifu katika migodi yetu.
 
Wana Jf
Kwa wale ambao hamjapata sikiliza Radio Kiswahili Ujerumani ya Jumapili ya tarehe 15/05/2011,mjaribu kuisikiliza kwani inaonekana Tanzania Umasikini wetu ni wa kujitakia ili tuweze kuendelea kupokea misaada kutoka nchi masikini

Akihojiwa na Radio Ujerumani Mama Zhakia Meghigi alidokeza kuwa baadhi ya nchi ikiwepo Tanzania zipo hapo ktk nchi masikini 48 Dunian eti kwa sababu zinahitaji kuendelea kupata misaada kutoka kwa wahisani
Hivi wana jf hili tutaendanalo mpaka lini?

Sikiliza hapa Wavuti wamejaribu kurecord kilicho ongelewa Category: 1 - Wavuti
 
Kweli kabisa! Tumejitakia kama Taifa! Kinachotakiwa ni kutubu mbele ya Mungu.full stop!
 
ndugu zangu tunawahitaji watu kama hao ili wafanye kazi ya kuwahubiria watumishi wa umma na viongozi kwa ujumla!. lakini yeye hatakiwi awe kiongozi wa kisiasa, ili kumuokoa asije akajifunza yaleyale nae akaishia kulaaniwa.
 
Watu hutaja sababu mbalimbali za umaskini ambazo nyingi huwa ni propaganda tu. Mimi nimejiridhisha kwamba sababu ya umaskni katika jamii/nchi yeyote ile Duniani ni:-
1. JAMII HUSIKA KUTOFUATA SHERIA ZILIZOPO.

Hakuna sababu nyingine zaidi ya hiyo!!!
 
Nakubaliana nawe, Watz tumezoea kutofuata sheria zilizopo; mfano hai viongozi wa CDM kwa sababu wanazozijua wao kwa makusudi wamekwepa kulipa kodi katika mamlaka za kiserikali. Kutolipa kodi ni kudhoofisha jitihada za serikali iliyopo madarakani kuwatumia raia wake.
 
...too MYOPIC, unfortunately.

It is the fact!
Its the reality!
You might call it MYOPIC but people and countries decided to overcome it are now in different World compared to those doing the opposite like your Tanzania!!
 
Watu hutaja sababu mbalimbali za umaskini ambazo nyingi huwa ni propaganda tu. Mimi nimejiridhisha kwamba sababu ya umaskni katika jamii/nchi yeyote ile Duniani ni:-
1. JAMII HUSIKA KUTOFUATA SHERIA ZILIZOPO.

Hakuna sababu nyingine zaidi ya hiyo!!!

Kwa nini hawafuati sheria zilizopo?
 
Back
Top Bottom