Ripoti: Kati ya 2018 hadi 2022 kulikuwa na Matukio ya Uhalifu 273,862 Nchini Tanzania

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
1696146762648.png

1696146809104.png
Takwimu za Uhalifu Nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka 5 (2018 - 2022) zimeonesha kulikuwa na jumla ya Matukio yaUhalifu 56,228 yaliyoripotiwa ambayo yalihusu Mauaji, Ubakaji, Ulawiti, Wizi wa Watoto, Kutupa Watoto, Unajisi na Usafirishaji Haramu wa Binadamu.

Pia, kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Jeshi la Polisi, katika kipindi hicho, kulikuwa na Ripoti za Matukio 126,295 yaliyohusu Wizi wa Silaha, Unyang;anyi katika Barabara Kuu, Kutumia Silaha, Kutumia Nguvu, Uvunjaji, Wizi wa Magari, Pikipiki, Mifugo, Kuchoma Nyumba na Uhalifu wa Kifedha.

Aidha, jumla ya Matukio 91,339 yaliyohusu Kupatikana na Silaha, Risasi, Mabomu, Dawa za Kulevya zikiwemo Unga, Kemikali, Bangi, Mashamba ya Bangi na Mirungi yaliripotiwa. Mengine ni kukutwa na Nyara za Serikali, Magendo, Rushwa, Gongo, Mitambo ya Pombe Haramu, Uvuvi Haramu, Mazao ya Misitu, Bahari na Wahamiaji Haramu.

Kwa upande wa Makosa ya Uhali wa Kifedha, kulikuwa na Jumla ya Matukio 4,985 yaliyoripotiwa yakihusisha Kupatikana na Noti Bandia, Wizi kwenye Mabenki, Mashirika ya Umma, Vyama vya Ushirika, Serikali za Mitaa, Serikali Kuu na Kughushi Nyaraka

JESHI LA POLISI/NBS
 
Back
Top Bottom