Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,870
- 155,833
RIPOTI: ‘GADDAFI ALIUAWA KIMAKOSA’
Raia wa Libya sasa hivi wanaishi maisha ya tabu ukilinganisha na kipindi cha utawala wa Kanali Gaddafi.
LONDON:
Ripoti ya Kamati ya Bunge Uingereza imekosoa hatua ya Uingereza na Ufaransa kuingilia kati na kusaidia kuondolewa madarakani kwa Kanali Muammar Gaddafi nchini Libya mwaka 2011.
Kamati hiyo ya Mambo ya Nje ilisema Uingereza iliongeza chumvi ilipokuwa inaeleza hatari ambazo zingewakumba raia baada ya Serikali ya Gaddafi kuanza kukabiliana na maasi.
Mpango wa kuingia kati kusaidia mwishowe ulitumika kama fursa ya kubadilisha utawala, ripoti hiyo ilisema. Pia, ripoti hiyo inamtuhumu aliyekuwa Waziri Mkuu David Cameron kwa kukosa kuandaa mkakati mahususi kuhusu Libya.
Wabunge hao walisema jambo hilo lilisababisha kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, mgogoro wa wahamiaji, ukiukwaji wa haki za kibinamu na kukua kwa kundi la wapiganaji wa Kiislamu wanaojiita Islamic State Afrika Kaskazini.
Msemaji wa Serikali ya Uingereza ametetea Serikali na kusema muungano wa mataifa ya Kiarabu, Arab League, na Umoja wa Mataifa, wote waliunga mkono hatua hiyo ya kijeshi.
Gaddafi aliuawa na waasi 20 Oktoba, 2011 na kuwaacha raia wa nchi yake wakiteseka baada ya kutetereka kwa uchumi wa nchi hiyo hali inayochangia kuongezeka kwa wakimbizi barani Ulaya.
Habari kutoka Libya zilisema kwamba Gaddafi alifariki dunia baada ya kujeruhiwa kichwani na miguuni alipokuwa akijaribu kutoroka kutoka Sirte.
Habari zaidi zilisema kuwa Gaddafi akiwa kwenye msafara mkubwa wa magari alijaribu kutoroka punde baada ya wanamapinduzi wa Libya kuutwaa mji huo.
Baadaye ndege za kivita za Nato ziliufuata msafara huo na kuudondoshea mabomu na Gaddafi alijeruhiwa kichwani na miguuni.
Kuuawa kwa Gaddafi kulithibitishwa na kamanda wa ngazi za juu wa jeshi la wanamapinduzi, Abdel Majid Mlegta kwa kusema ushahidi wa picha na video ulitolewa hadharani. Gaddafi aliiongoza Libya tangu alipompindua Mfalme Idris I, katika mapinduzi yasiyo ya umwagaji damu, wakati huo akiwa na miaka 27
Alipata umaarufu mkubwa kutokana na nguo alizopenda kuvaa, huku akiongozana na walinzi wa kike. Kiongozi huyo wa Libya, pia anadhaniwa kuwa na mbinu nzuri za kisiasa, kwa kuweza kuirejesha Libya kutokana na kutengwa kidiplomasia duniani.
Alipokuwa kijana alivutiwa na kiongozi mzalendo wa Misri, Gamal Abdel Nasser, alipokuwa akishiriki katika maandamano dhidi ya Israel wakati wa mtafaruku wa Suez mwaka 1956.
DONDOO:
Rais wa zamani wa Marekani, Ronald Reagan alimwita Gaddafi ‘mad dog’ yaani ‘mbwa kichaa’.
Kutoka katika Gazeti la Mwananchi la leo ukurasa wa 32 ukielezea habari za Afrika.