RIPOTI: Gaddafi aliuawa kimakosa

RIPOTI: Gaddafi aliuawa kimakosa

Uongozi unahitaji busara na hekima na wala siyo nguvu. Wote mkiwa na hasira lazima ngumi zipigwe tu hakuna jinsi. Watu wanasema utoke uwachie nchi yao na wewe unang'ang;ania sitoki. Unafikiri kinachofuata nini? Ukiwa kiongozi wewe ndiyo unatakiwa ufikiri zaidi kuliko unaowaongoza. Ni sawa baba na mtoto. Watoto wanasema hatukutambui kuwa baba yetu. Na wewe baba unang'ang'ania nyie ni wanangu. Mwisho wa siku unaanza kupigana na watoto wako lakini baba ukijiondokea. Hawa watoto ipo siku watakutafuta na watakupokea kwa heshima. Ghadafi angeondoka zake, huku mambo yangeenda kombo wangemtafuta tu. Yesu mwenyewe pamoja na kufanya mazuri lakini walimsurubisha. Je, wewe mwanadamu? Hawawezi kukuacha hai.
MTENDA WEMA NENDA ZAKO, USIGONJE SHUKRANI
Walibya walikuwa na option ya kuepuka haya madhara hakukuwa na ulazima wa kutumia nguvu zaidi ili tu kumuondoa Gaddafi,sasa hebu jiulize kipi hasa kilichowalazimu kuingiza nchi kwenye machafuko ni kumkomoa Gaddafi au kuna sababu ya msingi ambayo inaweza kufanya tusiwalaumu walibya kwa haya madhara yaliyopo kutokana na uamuzi wao wa waliyoufanya? Ulevi wa madaraka unajulikana hivyo walibya wangetafuta njia nzuri ya kudeal na hilo lakini walichofanya haukuwa uamuzi sahihi,unafikiri hata Gaddafi angejiondoa mwenyewe ni kipi wangefaidika walibya kwa kujiondoa kwake Gaddafi? Ndio maana nasema wametumia nguvu kubwa na kuingiza kwenye vita hali ya kuwa hakukuwa na ulazima huo. Kuishia kumtupia lawama tu Gadaffi katika uchu wake wa madaraka kwamba yeye ndio wa kulaumiwa ni sawa na kumlaumu mwanamke aliyeuliwa na mumewe kwa sababu ya usaliti.
 
Kama watu hawakutaki unawacha unafanya mambo yako. Ni sawa umeoa mwanamke na umekaa naye miaka 5 kwa upendo halafu mwanamke anakuambia hakutaki anataka kuishi pekee yake. Unakuwa king'ang'anizi anaanza kukudharau na kutoka na mwanaume mwingine. Na wewe bado unamng'ang'ania tu. Hapo lazima utafute gunia mbili za mkaa halafu mwisho wa yote, mwanamke anakufa na wewe unaozea segerea. Ndicho kilichomtokea Ghadafi. Amekufa, watoto wake wamefungwa fungwa gerezani na nchi ipo kwenye hali mbaya ya kiuchumi. UNAWASUMBUKIA WATU WAKATI HAWANA MUDA NA WEWE. ANGEENDA KWENYE NCHI YOYOTE AKAISHI HUKO.

Waliokuwa hawamkubali ni wachache sana, pengine hawafiki hata milioni moja...mabeberu wajanja sana, wakishaona nchi za kiafrika zimekuwa kiuchumi basi ujuwe watakufanyia kila njia uporomoke, hata wakifa wananchi wako sawa tu ilimradi lengo lao litimie.
 
Tatizo ni pale wachache wanapokukataa lakini wengi wanakukubali sana.

Halafu hao wachache wabebe silaha waanzishe uasi kisha wasaidiwe na NATO, kiufupi inabidi usimame kidete ulinde haki ya wengi, huo ndiyo uongozi ulivyo, hakuna kiongozi anayependwa 100%
 
Issue ya Ghadafi ilikuwa ngumu sana. Marekani aliwatumia ndugu zake yaani wananchi wake kwahiyo hapo ni ngumu kung'amua yupi adui yupi rafiki. Ni sawa na mtu anakuchonganisha wewe na ndugu zako mnaanza kupigana. Ukimuua ndugu yako mmoja kwa nia ya kujitetea hata wengine wanaokuunga mkono wataenda kwa adui. Hili kuepuka ugomvi na ndugu zako ni wewe kukimbia, watasema ni muoga lakini utakuwa umewaokoa.
Hizi nchi za kibeberu wametengeneza mazingira ya wananchi wake kuipenda nchi zao. Angalia movie, muziki na michezo mingine. Kofia, nguo na zingine zina nembo ya USA au majina ya majimbo kama Los Angeles, Newyork City, Miami n.k Huku bongo msanii anaimba nyimbo na kofia imeandika Newyork City (Siwezi kuwalaumu kwasababu mazingira magumu ya kiuchumi huenda yanawafanya hivyo). Kwa nchi kama Marekani huwezi kuwashawishi waingie vitani kwasababu Wanajeshi, polisi na wananchi ni marafiki. Mtu anaandamana na sanamu la Trump likiwa uchi wa mnyama halafu hata hapigwi. Jaribu Bongo uone kitakachokutokea. Polisi na wanajeshi wapo harsh sana kwa wananchi kwahiyo hawa wananchi wakitumiwa na mabeberu ni rahisi sana kuingia kwenye machafuko
Thread closed.
 
Kuna mambo ya kijinga sana yametujaa vichwani waafrika kiasi huwa nashangaa tunawezaje kujenga nyumba isianguke ikiwe hatujui umuhimu wa MSINGI.

1. Ili tuendelee, tunahitaji TAASISI IMARA na sio KIONGOZI IMARA. Gaddaffi hakuwa TAASISI, alikuwa KIONGOZI MBINAFSI asiyekumbuka kuwa siku moja angekufa. Kwa mfano asingeuliwa na aliowaudhi akafa kwa kugongwa na gari la farasi kwa bahati mbaya, Walibya wangelazimika kumfufua?

2. Si kweli kuwa Walibya wote walikuwa wakineemeka na utawala wake. Hakuna mtawala kwa mabavu asiye na wafuasi. Kinachotofautiana na idadi ya hao wafuasi na mirengo yao, maana ndani yao kuna WANAFIKI na WAKWELI. Wanafiki hawanaga ushirika wa kudumu, siku ukianguka wanageuka na kuwa washirika wa aliyekuangusha. Wa kweli hupigana pembeni yako hadi mwisho...Je, kuna dalili ya kundi kubwa kumpigania Gadaffi hadi mwisho?

Ukisoma kitabu cha Things Fall Apart cha Chinua Achebe, utajifunza kitu kuhusu HAKI na USAWA unavyotukwamisha. Lilikuwapo tabaka la watu waliotengwa ndani ya jamii ya Ibo ambalo lenyewe lilikuwa la kwanza kushawishika kujiunga na Wamisionari sababu hawakukubalika na jamii yao. Hawa wanafanana na Walibya walioishi kwenye vile vibanda vilivyochoka kule Benghazi, hawa hata kama ungelikuwa ni wewe...ungeitikia wito wa kumng'oa Gadaffi.

Waafrika tujifunze kuheshimu zile fundamental human rights. Hata ujenge bahari kila mkoa, ukiutweza utu wa mwanadamu, hautaungwa mkono kwa moyo, utaungwa kwa woga na hila.

3. Jambo la tatu lenye kunifikirisha nisipate majibu ni hili la kuwa ukioa sijui na kufanyaje basi utapata pesa bure kutoka kwa Gadaffi. Ikiwa haya ni kweli, ina maana Walibya hawafanyi kazi, maana kazi tunafanya ili tuweze kujikimu. Kuna serikali yenye kuweza kuadvocate maisha ya namna hiyo kwa wananchi wake? Walibya si sehemu ya manusura ya wahamiaji haramu wanaookotwa pwani ya Italia pamoja na Waafrika wengine wa Kaskazini? Je kuna watu wanaokimbilia Libya kutafuta kazi kama ilivyo USA, South Africa na Saudia Arabia?

Kwangu mimi Gadaffi ni FAILURE. Kiongozi asiye na plan ya kuwaandaa wengine kuchukua majukumu yake ni mbinafsi na wa hovyo kabisa. Badala ya kutengeneza uongozi endelevu kwa kuzingatia vipaumbele vya nchi, akajitengeneza kuwa mungu, na sasa ni marehemu.
 
Kama Gaddafi angefanikiwa kuifanya sarafu moja ya umoja wa Africa, nchi ya USA na Umoja wa Ulaya zingekuja kununua madini kwa thamni ya pesa ya Africa.
 
WHAT HAPPENED IN LIBYA .., WHAT IS HAPPENING IN LIBYA NOW ,, AND WHAT WILL HAPPEN IN LIBYA IN FUTURE TIMES.,,, IS LIKE THE TEARS OF THE SUN .,,THAT NEVER DRIED.......
 
Yaani kweli sisi wote hapa tulikuwa tunasubiri report ya kamati ya Bunge ya Uingereza kutambua makosa yaliyofanywa ktk mauaji ya gadhafi?
 
Tatizo ni pale wachache wanapokukataa lakini wengi wanakukubali sana.
Halafu hao wachache wabebe silaha waanzishe uasi kisha wasaidiwe na NATO, kiufupi inabidi usimame kidete ulinde haki ya wengi, huo ndiyo uongozi ulivyo, hakuna kiongozi anayependwa 100%
Ukiwa kiongozi lazima utumie busara, hekima, akili nyingi na nguvu kidogo. Na hapa mabeberu ndiyo wanapotushinda na mwisho wa siku tunabaki kuwalaumu huku majanga yameshatokea. Alipoamua kupambana na watu wachache aliweza kuwashinda? Unapoingia na adui vitani hata kama ni watu 20 lazima ujiulize hawa wanajiamini nini? nani walioko nyuma ya adui yako. Adui anasilaha kali kuliko wewe halafu unasema upigane naye. Lazima ujiulize hawa silaha wametoa wapi? Hiyo vita Ghadafi alishinda? Wewe unafikiri kwanini Marekani haijaivamia Irani au north korea? Kwasababu wanatumia akili nyingi na nguvu kidogo. amepiga hesabu hasara ni nyingi kuliko faida. Watu wanakaa mezani wanajadili faida na hasara zitakazotokea. Wakiona hasara ni nyingi kuliko faida wanapiga chini mpango wa vita. Ni sawa na mtu A anataka apigane na wewe halafu kuna mtu B hakupendi anakuchukia. Huyu mtu B lazima ashirikiane na mtu A kukupiga wewe. Mabeberu wanashinda siku zote kwasababu wanatumia akili nyingi na nguvu kidogo. Shida ya viongozi wa Afrika wanatumia nguvu nyingi akili kidogo ndiyo matokeo yake hayo. Watu wakiandamana kidogo utawaona FFU wanakuja na bunduki, mabomu na magari ya kuwashawasha wakati waandamaji hawana hata fimbo mkononi.
 
RIPOTI: ‘GADDAFI ALIUAWA KIMAKOSA’
Raia wa Libya sasa hivi wanaishi maisha ya tabu ukilinganisha na kipindi cha utawala wa Kanali Gaddafi.

LONDON:
Ripoti ya Kamati ya Bunge Uingereza imekosoa hatua ya Uingereza na Ufaransa kuingilia kati na kusaidia kuondolewa madarakani kwa Kanali Muammar Gaddafi nchini Libya mwaka 2011.

Kamati hiyo ya Mambo ya Nje ilisema Uingereza iliongeza chumvi ilipokuwa inaeleza hatari ambazo zingewakumba raia baada ya Serikali ya Gaddafi kuanza kukabiliana na maasi.

Mpango wa kuingia kati kusaidia mwishowe ulitumika kama fursa ya kubadilisha utawala, ripoti hiyo ilisema. Pia, ripoti hiyo inamtuhumu aliyekuwa Waziri Mkuu David Cameron kwa kukosa kuandaa mkakati mahususi kuhusu Libya.

Wabunge hao walisema jambo hilo lilisababisha kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, mgogoro wa wahamiaji, ukiukwaji wa haki za kibinamu na kukua kwa kundi la wapiganaji wa Kiislamu wanaojiita Islamic State Afrika Kaskazini.
Msemaji wa Serikali ya Uingereza ametetea Serikali na kusema muungano wa mataifa ya Kiarabu, Arab League, na Umoja wa Mataifa, wote waliunga mkono hatua hiyo ya kijeshi.

Gaddafi aliuawa na waasi 20 Oktoba, 2011 na kuwaacha raia wa nchi yake wakiteseka baada ya kutetereka kwa uchumi wa nchi hiyo hali inayochangia kuongezeka kwa wakimbizi barani Ulaya.

Habari kutoka Libya zilisema kwamba Gaddafi alifariki dunia baada ya kujeruhiwa kichwani na miguuni alipokuwa akijaribu kutoroka kutoka Sirte.

Habari zaidi zilisema kuwa Gaddafi akiwa kwenye msafara mkubwa wa magari alijaribu kutoroka punde baada ya wanamapinduzi wa Libya kuutwaa mji huo.

Baadaye ndege za kivita za Nato ziliufuata msafara huo na kuudondoshea mabomu na Gaddafi alijeruhiwa kichwani na miguuni.

Kuuawa kwa Gaddafi kulithibitishwa na kamanda wa ngazi za juu wa jeshi la wanamapinduzi, Abdel Majid Mlegta kwa kusema ushahidi wa picha na video ulitolewa hadharani. Gaddafi aliiongoza Libya tangu alipompindua Mfalme Idris I, katika mapinduzi yasiyo ya umwagaji damu, wakati huo akiwa na miaka 27

Alipata umaarufu mkubwa kutokana na nguo alizopenda kuvaa, huku akiongozana na walinzi wa kike. Kiongozi huyo wa Libya, pia anadhaniwa kuwa na mbinu nzuri za kisiasa, kwa kuweza kuirejesha Libya kutokana na kutengwa kidiplomasia duniani.

Alipokuwa kijana alivutiwa na kiongozi mzalendo wa Misri, Gamal Abdel Nasser, alipokuwa akishiriki katika maandamano dhidi ya Israel wakati wa mtafaruku wa Suez mwaka 1956.

DONDOO:
Rais wa zamani wa Marekani, Ronald Reagan alimwita Gaddafi ‘mad dog’ yaani ‘mbwa kichaa’.
Kutoka katika Gazeti la Mwananchi la leo ukurasa wa 32 ukielezea habari za Afrika.
Hawana lolote wapuuzi tu hawa
 
Waliokuwa hawamkubali ni wachache sana, pengine hawafiki hata milioni moja...mabeberu wajanja sana, wakishaona nchi za kiafrika zimekuwa kiuchumi basi ujuwe watakufanyia kila njia uporomoke, hata wakifa wananchi wako sawa tu ilimradi lengo lao litimie.
Mjanja siku zote ndiyo anashinda. Wewe unapigana na watu wachache hata hujiulizi hawa wachache wamewezaje kuivimbia serikali iliyoko madarakani? Shida ya viongozi wa Afrika wanatumia nguvu nyingi na akili kidogo wakati mabeberu wanatumia akili nyingi na nguvu kidogo. Ushajiuliza kwanini Marekani haikuivamia North Korea? Wamekiri wamemuua Ghadafi kimakosa. Ni nani aliyemuua Ghadafi? je, nani atashitakiwa kwa kumuua Ghadafi? Watu wameshachukua mafuta na wameacha lawama. Hao ndiyo mabeberu. Kasome Capitalism na Neo-colonialism ndiyo utajua hawa watu wanaakili nyingi sana ili uweze kuwashinda lazima na wewe utumie akili nyingi.
 
Kuna mambo ya kijinga sana yametujaa vichwani waafrika kiasi huwa nashangaa tunawezaje kujenga nyumba isianguke ikiwe hatujui umuhimu wa MSINGI.

1. Ili tuendelee, tunahitaji TAASISI IMARA na sio KIONGOZI IMARA. Gaddaffi hakuwa TAASISI, alikuwa KIONGOZI MBINAFSI asiyekumbuka kuwa siku moja angekufa. Kwa mfano asingeuliwa na aliowaudhi akafa kwa kugongwa na gari la farasi kwa bahati mbaya, Walibya wangelazimika kumfufua?

2. Si kweli kuwa Walibya wote walikuwa wakineemeka na utawala wake. Hakuna mtawala kwa mabavu asiye na wafuasi. Kinachotofautiana na idadi ya hao wafuasi na mirengo yao, maana ndani yao kuna WANAFIKI na WAKWELI. Wanafiki hawanaga ushirika wa kudumu, siku ukianguka wanageuka na kuwa washirika wa aliyekuangusha. Wa kweli hupigana pembeni yako hadi mwisho...Je, kuna dalili ya kundi kubwa kumpigania Gadaffi hadi mwisho?

Ukisoma kitabu cha Things Fall Apart cha Chinua Achebe, utajifunza kitu kuhusu HAKI na USAWA unavyotukwamisha. Lilikuwapo tabaka la watu waliotengwa ndani ya jamii ya Ibo ambalo lenyewe lilikuwa la kwanza kushawishika kujiunga na Wamisionari sababu hawakukubalika na jamii yao. Hawa wanafanana na Walibya walioishi kwenye vile vibanda vilivyochoka kule Benghazi, hawa hata kama ungelikuwa ni wewe...ungeitikia wito wa kumng'oa Gadaffi.

Waafrika tujifunze kuheshimu zile fundamental human rights. Hata ujenge bahari kila mkoa, ukiutweza utu wa mwanadamu, hautaungwa mkono kwa moyo, utaungwa kwa woga na hila.

3. Jambo la tatu lenye kunifikirisha nisipate majibu ni hili la kuwa ukioa sijui na kufanyaje basi utapata pesa bure kutoka kwa Gadaffi. Ikiwa haya ni kweli, ina maana Walibya hawafanyi kazi, maana kazi tunafanya ili tuweze kujikimu. Kuna serikali yenye kuweza kuadvocate maisha ya namna hiyo kwa wananchi wake? Walibya si sehemu ya manusura ya wahamiaji haramu wanaookotwa pwani ya Italia pamoja na Waafrika wengine wa Kaskazini? Je kuna watu wanaokimbilia Libya kutafuta kazi kama ilivyo USA, South Africa na Saudia Arabia?

Kwangu mimi Gadaffi ni FAILURE. Kiongozi asiye na plan ya kuwaandaa wengine kuchukua majukumu yake ni mbinafsi na wa hovyo kabisa. Badala ya kutengeneza uongozi endelevu kwa kuzingatia vipaumbele vya nchi, akajitengeneza kuwa mungu, na sasa ni marehemu.
HAPo umenena! Ili nchi iwe na maendeleo endelevu inahitaji taasisi imara na sio kumtegemea binadamu.
 
Issue ya Ghadafi ilikuwa ngumu sana. Marekani aliwatumia ndugu zake yaani wananchi wake kwahiyo hapo ni ngumu kung'amua yupi adui yupi rafiki. Ni sawa na mtu anakuchonganisha wewe na ndugu zako mnaanza kupigana. Ukimuua ndugu yako mmoja kwa nia ya kujitetea hata wengine wanaokuunga mkono wataenda kwa adui. Hili kuepuka ugomvi na ndugu zako ni wewe kukimbia, watasema ni muoga lakini utakuwa umewaokoa.
Hizi nchi za kibeberu wametengeneza mazingira ya wananchi wake kuipenda nchi zao. Angalia movie, muziki na michezo mingine. Kofia, nguo na zingine zina nembo ya USA au majina ya majimbo kama Los Angeles, Newyork City, Miami n.k Huku bongo msanii anaimba nyimbo na kofia imeandika Newyork City (Siwezi kuwalaumu kwasababu mazingira magumu ya kiuchumi huenda yanawafanya hivyo). Kwa nchi kama Marekani huwezi kuwashawishi waingie vitani kwasababu Wanajeshi, polisi na wananchi ni marafiki. Mtu anaandamana na sanamu la Trump likiwa uchi wa mnyama halafu hata hapigwi. Jaribu Bongo uone kitakachokutokea. Polisi na wanajeshi wapo harsh sana kwa wananchi kwahiyo hawa wananchi wakitumiwa na mabeberu ni rahisi sana kuingia kwenye machafuko
Ume elezea mengi sana mkuu ila point inarejelea pale pale asee yakwamba maamuzi yao hayakua sahihi na kwa nnnwalifanya waloyafanya uonevu na kutetea maslahi yao kwanjia zakishenzi
 
Leo hii tuona Marekani ambayo inawezeka kuipiga Iran ila inashindwa kukurupuka kufanya hivyo kwa sababu ya wanajua kutakuwa na madhara makubwa endapo wataamua kufanya hivyo kwa maana hiyo lazima watafute njia ambayo haitaweza kuleta majanga,
Swali la msingi ni kwamba je ni uamuzi sahihi kuingiza nchi nzima kwenye kwa sababu ya mtu mmoja kung'ang'ania madaraka? Sawa kiongozi kang'ang'ania ndio kosa lake je ndio tuseme kumtoa kiongozi huyo ni muhimu kiasi cha kuingiza nchi kwenye vita visivyojulikana vitaisha lini? Leo hii tuona Marekani ambayo inawezeka kuipiga Iran ila inashindwa kukurupuka kufanya hivyo kwa sababu ya wanajua kutakuwa na madhara makubwa endapo wataamua kufanya hivyo kwa maana hiyo lazima watafute njia ambayo haitaweza kuleta majanga,sasa ndugu zetu wamechafua nchi yao sasa haikaliki kabisa kisa tu kumuondoa mtu aliyekuwa anang'ang'ania madaraka.
Mkuu yaani huko juu koote na chini yake nimekubaliana na ww ila hcho kipengele chako nlokikopi hapa ndio sijakubaliana na ww mkuu

Kama Kweli US anakhofia hicho pale IRAN Angefanya juu chini akamaliza mgogoro wa SYRIA

Angefanya juu chini Akaumaliza Mgogoro Wa YEMEN

Angefanya juu chini akaumaliza huu mgogoro unaoendelea pale LIBYA Badala yake anajua kuna serikali inayotambulika kimataifa ila jamaa anaenda kumuunga mkono KHAFTAR

Nikwambie 2 US Anacho Ogopa IRAN nihasara zitakazo tokana na ile vita Halina Ubishi kwamba IRAN Anaweza akapigwa tena vibaya na sana ila IRAN Nae atalipiza majibu kwa ukali sanaaaa

Hvyo ss US Anajiuliza ana anzaje kuingia vitani na MUAJEMI Hizo zakusema cjui anakhof nn cjui nn ni habari 2 vijiweni vyakahawa ila ukweli Ndio Huu MKUU
 
Ume elezea mengi sana mkuu ila point inarejelea pale pale asee yakwamba maamuzi yao hayakua sahihi na kwa nnnwalifanya waloyafanya uonevu na kutetea maslahi yao kwanjia zakishenzi
Ghadafi ameuwawa. Je, aliyemuua Ghadafi ni nani? Na nani atashitakiwa kwa mauaji ya Ghadafi?
 
Gaddafi kauliwa kimkakati...

He was a very strong leader, a leader with missions and visions not only to libya but to whole of Africa...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom