Ripoti - Dodoma hapafai kuzalia..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ripoti - Dodoma hapafai kuzalia.....

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Dec 26, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Gazeti la habari leo linatutaarifu ya kuwa Hospitali kuu ya Dodoma haina sifa za kuzalia watoto mbali ya kuwa imekuwa ikiendelea kutoa hiyo huduma...............
   
 2. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2010
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  loh, Mungu wangu wee! jamani wahusika waoneeni huruma akina mama na watoto
   
 3. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  tupe sababu
   
 4. MKURABITA

  MKURABITA JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 311
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mkuu, hii ni habari muhimu sana kwetu, siku nyingine kumbuka kuweka link ili tusome zaidi, nimejaribu kufuatilia Habari Leo sijaona namna ya kupata habari zilizopita.
   
 5. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Waandishi wetu bana!labda tujue hospitali inahitaji nini ili iweze kuzalisha.kama wakunga wa jadi wanazalisha iweje regional hospital ishindwe?
   
 6. Miss X

  Miss X Member

  #6
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 98
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Dodoma hapafai kuzalia-Ripoti
  Imeandikwa na Anastazia Anyimike; Tarehe: 26th December 2010 @ 11:18 Imesomwa na watu: 172; Jumla ya maoni: 0


  LICHA ya kuwa na hadhi ya Hospitali ya Mkoa, wataalamu wameielezea kuwa ina mapungufu mengi, kiasi cha kutofaa kutoa huduma nyingi zikiwamo za kuzalisha na hata upasuaji.


  Hayo yamebainika baada ya uchunguzi uliofanywa na jopo la wataalamu 11, wakiwamo tisa kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na wawili kutoka Mkoa wa Dodoma ambao walifanya ukaguzi wa vituo vya kutolea huduma za afya mkoani humo.

  Hata hivyo, kutokana na kukosekana kwa mbadala, uongozi wa hospitali hiyo umetakiwa kufanya marekebisho katika vyumba vya kujifungulia na chumba cha upasuaji kwa wazazi hasa baada ya kuthibitika kwamba, havifai kutumika katika utoaji wa huduma hiyo.

  Akizungumza na HABARILEO Jumapili, Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi, Dk Ibrahim Maduhu alisema kuwa, katika hospitali hiyo wameona kuwa vyumba vya kujifungulia, kile cha upasuaji kwa wazazi na `X-ray' havifai kutumika.

  "Tulichokuwa tunafanya ni kuangalia mambo mengi, jinsi wanavyotoa huduma, wataalamu, usajili, dawa, usafi na utunzaji wa taka, lakini katika hospitali ya mkoa hali ni mbaya katika vyumba vya kujifungua, upasuaji na X-ray kwa kweli havifai kabisa kutumika na tumewataka warekebishe hili."

  Alisema katika Wilaya ya Kondoa kati ya vituo saba walivyokaguliwa viwili vimetakiwa kufanya marekebisho ikiwamo hospitali ya wilaya ambayo haina wataalamu huku vituo vitano vikifungwa kutokana na sababu mbalimbali.

  Zingine zilizotakiwa kufanya marekebisho ni kutoka manispaa ya Dodoma ni St. Gemma Gagani Health Centre (watumishi na vifaa), Zahanati ya Makole (utupaji wa taka hatari na mikataba) na Kituo cha Afya Kijiji cha Matumaini (wataalamu) na Zahanati ya Kondoa (wataalamu).

  Maduhu alisema katika ukaguzi huo wamefungia vituo vya kutolea huduma za afya 16 na vingine sita kutakiwa kurekebisha ikiwa ni vituo 22 katika manispaa ya Dodoma na Kondoa.

  "Vituo sita tulivyovifungia kwa kutokuwa na usajili, vingine vimekiuka taratibu za usajili kwani watu waliovisajili hawapo na kinachofanyika ni kutumia cheti cha mhusika tu, utaratibu ni kuwa aliyesajili anatakiwa kuhakikisha anakitembelea kituo hicho mara mbili kwa wiki."

  "Pia kuna vituo vinane tulivyovifungia kutokana na kutokuwa na wataalamu, hawa watu wanafanya biashara, lakini wanaleta mzaha na maisha ya watu, kusema ukweli hatutawavumilia watu kama hawa," alisema.

  Maduhu alisema sababu zingine za kuvifungua baadhi ya vituo ni pamoja na kuwa na mazingira hatarishi, kutokuwa na daktari msimamizi na kujengwa kwenye makazi ya watu.
  Alisema, pia kuna vituo vilivyofungwa baada ya vilivyokutwa na dawa za serikali, zilizomaliza muda wake na ambazo hazijasajiliwa.

  "Dawa za serikali zinatumika katika hospitali za serikali na za dini ambazo zinatoa huduma bila faida kwa sababu zinatolewa ruzuku, lakini tunapozikuta kwenye kituo kisichostahili bila maelezo ya wapi wamezitoa ina maana ni dawa zilizoibwa kwenye hospitali zetu, tulichokifanya ni kuzichukua na kurejesha kwa Mganga Mkuu, zile zilizopitwa na wakati na zisizosajiliwa unafanyika utaratibu wa kuziharibu na pia kuwachukulia hatua za kisheria," alisema.

  Maduhu alizitaja vituo vilivyofungwa na sababu kwenye mabano kuwa ni zahanati ya Central, zahanati ya Majengo, Kliniki ya meno ya Dk Kidyalla, Zahanati ya JRL na zahanati ya DN (Wataalamu; Mazingira hatarishi), UMATI-Chamwino (usajili, dawa zisizosajiliwa, dawa zilizomaliza muda), zahanati ya Tumaini na hospitali ya Elina (usajili na dawa za serikali), zahanati ya Chang'ombe (usajili) wakati zahanari ya Nhendeule na kliniki ya meno ya Red Cross Dental havipo.

  Alisema, kwa upande wa Kondoa ni Tumaini PRINMAT na Sha-Majala (usajili), zahanati za Chemchem na Kondoa (havipo) na zahanati ya Blessed (hakuna msimamizi na wataalamu).

  "Nawataka wanaoendesha huduma za afya kufuata taratibu za usajili ya mwaka 1977, kwani kinyume cha hapo wanaweza kushitakiwa na kupata adhabu ya kifungo au faini au vyote kwa pamoja.

  "Kwa wale ambao hawajafuata taratibu wafunge mara moja kabla ya sheria kuchukua mkondo wake na pia uongozi wa idara ya afya wa wilaya, hususani timu ya uendeshaji ya afya ya wilaya ufanye usimamizi na ukaguzi wa mara kwa mara ili kudhibiti ubora wa huduma za afya," alisema.
   
Loading...