Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 26,060
- 23,943
Ripoti ya awali ya ufuatiliaji wa sakata la mabinti waliokutwa wakiishi katika nyumba moja Jijini Dodoma kwa madai ya kupatiwa mafunzo ya dini ya Kiislamu, imebainisha kuwa baadhi yao walikatisha masomo, kubadilisha majina na kituo walichokuwa wakiishi sambamba na kutokuwa na leseni ya usajili.
Kutokana na ripoti hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ameelekeza watoto hao 132 kukabidhiwa kwa wakuu wa wilaya walizotoka na kuendelea na masomo huku hatua mbalimbali za kisheria zikiendelea kuchukuliwa.
SOURCE: Azamtv