RIP Mwalimu

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,013

Mwenyezi Mungu angekupa uhai zaidi basi ungegundua kwamba nchi yetu si maskini kabisa tuna utajiri mkubwa sana wa rasilimali ambazo kama zingetumika vizuri nchi yetu ingekuwa mbali sana kimaendeleo. Na pia baada ya kusikia na kufahamu ufisadi mkubwa uliofanywa na Viongozi mbali mbali toka CCM basi ungebadili kauli yako na kusema Kiongozi bora wa Tanzania ni lazima atoke nje ya CCM maana hao wote waliotoka CCM wameendeleza ufisadi mkubwa na kuongeza kwa kiwango kikubwa gharama za maisha ya ya kila siku kwa Watanzania. Mwenyezi Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi~AMEN.
 
Last edited by a moderator:
1999?
Sina hakika kama RIP yako ina mashiko. It's too late
 
1999?
Sina hakika kama RIP yako ina mashiko. It's too late

Dah! Kwani kuna muda maalum wa kumtakia marehemu apumzike kwa amani na ukishapita hairuhusiwi tena kumuombea hivyo? Kama upo muda huo umeandikwa kwenye kitabu gani kitukufu? Quran au Biblia?
 
Nilidhani Mwezi huu ni kumbukumbu ya SOKOINE; Sikujua pia ya JK Nyerere

Au ndio watu wameanza na vilembwe vyao vya kutokuwa Makini na kushusha hadhi ya Jamii Forum?
 
Mkuu uko sahihi kabisa.
Watanzania wameathirika na mawazo hasi, which means hawawezi kufikiri positively bila kum quote Mwalimu.
Ningeelewa kama angesema mwalimu angekuwa hai asingekuwa mwanachama wa ccm kutokana na msimamo wake kutoendana na ccm ya sasa.

Nilidhani Mwezi huu ni kumbukumbu ya SOKOINE; Sikujua pia ya JK Nyerere

Au ndio watu wameanza na vilembwe vyao vya kutokuwa Makini na kushusha hadhi ya Jamii Forum?
 
Mwenyezi Mungu angekupa uhai zaidi basi ungegundua kwamba nchi yetu si maskini kabisa tuna utajiri mkubwa sana wa rasilimali ambazo kama zingetumika vizuri nchi yetu ingekuwa mbali sana kimaendeleo.
Mkuu nadhani alijua yote haya na alikuwa na busara ya kutokumaliza mali asili za wajukuu zetu mpaka tutakapopata akili kuyachimba na kutunufaisha.., sio kwamba hakujua bali alijua zaidi kwamba bila busara tunaweza tukawa shamba la bibi kama hivi sasa

Na pia baada ya kusikia na kufahamu ufisadi mkubwa uliofanywa na Viongozi mbali mbali toka CCM basi ungebadili kauli yako na kusema Kiongozi bora wa Tanzania ni lazima atoke nje ya CCM maana hao wote waliotoka CCM wameendeleza ufisadi mkubwa na kuongeza kwa kiwango kikubwa gharama za maisha ya ya kila siku kwa Watanzania
Kwa busara na diplomatically asingeweza kusema hayo maneno mbele ya kadamnasi ile alisema the same thing in not so many words... "kwamba chagueni kiongozi bora.., na kama hayupo ndani ya CCM wananchi watamtafuta nje ya CCM"
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nyerere ndio chanzo cha matatizo yote haya tuliyinayo, mfumo alioutengeza, umekuwa mgumu sa na kuuondoa, sijui kwanini mnakuwa mnamrejea kila wakati wakati huu tunaotaka mabadiliko, embu fikiria, asingeiingilia uchaguzi 1995 tungekuwa wapi sasa, kama asingeanzisha mfumo wa chama kimoja leo tungekuwa wapi?
 
Mfumo aliuoacha Mwalimu ambaye aling'atuka toka madarakani mwaka 1985 miaka 27 iliyopita. Wamekuja akina Mwinyi, Mkapa na Kikwete na katika miaka 27 wameshindwa kabisa kuubadilisha mfumo uliowekwa na Mwalimu pamoja na wote hao kuachana na siasa za Ujamaa na kujitegemea lakini bado wa kupewa lawama ni Mwalimu tu!!!! Hata miaka mia ijayo nchi yetu ikiwa bado iko katika hali mbaya wachukuaji wameshachukua rasilimali zote bado kuna watu watamlamu Mwalimu tu!!!! Kazi kweli kweli!!!!
 
Nilidhani Mwezi huu ni kumbukumbu ya SOKOINE; Sikujua pia ya JK Nyerere

Au ndio watu wameanza na vilembwe vyao vya kutokuwa Makini na kushusha hadhi ya Jamii Forum?
nnguu07
Sokoine alifariki April 14. Birthday ya Mwalimu ni April 13.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hii kauli ya kusema kiongozi bora lazima atoke ccm ilitoka baada au kabla ya kusema 'ccm si mama yangu?'
 
Hii kauli ya kusema kiongozi bora lazima atoke ccm ilitoka baada au kabla ya kusema 'ccm si mama yangu?'
Raia Fulani,
Aliisema hiyo 1995. Wakati huo kwa kweli upinzani haukuwa na uongozi makini. Lakini katika muktadha huo huo aliongeza angalizo hili: CCM wakishindwa kutoa uongozi unaofaa, wananchi watautafuta kwingineko. That is the clincher! Hii ya kuwa CCM si mama yake aliwaambia viongozi waliotumwa kwake na Mwinyi wakitaka aache kufanya vikao na wapinzani (Mrema)
 
hii hotuba inafaa kuwekwa kwenye fuso za matangazo za chadema na kutembezwa nchi nzima ili kutoa elimu ya uraia pamoja na kuelezwa ni kwa nini ccm imefikia mwisho.
 
nnguu07
Sokoine alifariki April 14. Birthday ya Mwalimu ni April 13.

nnguu07
Sokoine alifariki April 14. Birthday ya Mwalimu ni April 13.

Mkuu Jasusi ahsante sana kwa hili bandiko lakini sidhani kama tunahitaji kusikiliza/kuyajadili maneno ya busara ya Mwalimu pale ambapo kuna maadhimisho ya namna moja au nyingine kuhusiana na Mwalimu. Maneno ya Mwalimu yamejaa busara na hekima nyingi yanastahili kusikilizwa wakati wowote ule kuwe na maadhimisho yanayomuhusu Mwalimu au hata kama hakuna maadhimisho. Kwa mara nyingine ahsante sana na uwe na Jumapili njema.
 
Hotuba safi sana (short and clear)

...Ndiyo maana bado Watanzania wengi tunazienzi hotuba za Mwalimu kwa sababu zina hekima na busara ya hali ya juu na pamoja na kuwa alizitoa miaka mingi iliyopita lakini nyingi bado ziko valid hata leo hii....Sijui kama wapo Watanzania wanaozienzi hotuba za Mwinyi, Mkapa au Kikwete.
 
Tena kuna moja aliyosema "IKULU NI MAHALA PATAKATIFU, MIMI SIKUCHAGULIWA NA WANANCHI WA TZ KUJA KUBAGEUZA KUWA PANGO LA WALANGUZI"
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom