RIP John Mjema

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,173
12,936
Katutoka jana.

Habari zaidi zitawajia kuhusu alivyoanza kuchizi hadi kifo chake pamoja na historia ya maisha yake.

RIP John Mjema
 
Katutoka jana.

Habari zaidi zitawajia kuhusu alivyoanza kuchizi hadi kifo chake pamoja na historia ya maisha yake.

RIP John Mjema

Mungu ametoa,Bwana Mungu Ametwaa,Jina lake lihimidiwe?
hivi John Mjema ndio yule ndio msanii wa kizazi kipya cha kina Rich- Monduli?
 
Mungu ametoa,Bwana Mungu Ametwaa,Jina lake lihimidiwe?
hivi John Mjema ndio yule ndio msanii wa kizazi kipya cha kina Rich- Monduli?

Huyu alikuwa na kundi lake la 'Mambo Poa', akiwa na Spider na Marehemu Steve 2K. Nyimbo zake ni pamoja na 'Mimi sio Mwizi, Bomba la Mvua na Wachumba 30'

RIP John.
 
Huyu alikuwa na kundi lake la 'Mambo Poa', akiwa na Spider na Marehemu Steve 2K. Nyimbo zake ni pamoja na 'Mimi sio Mwizi, Bomba la Mvua na Wachumba 30'

RIP John.

Nani alimchoma kisu Steve 2k?
 
Nani alimchoma kisu Steve 2k?

clasmeti na monita wa darasa letu aitwaye castrol Ponela. Jamaa ninavyomjua mie ni kuwa alikuwa mtaratibu na rafiki ila baadae sana akaanza kupiga nondo, nilikutana naye miaka kibao baada ya kumaliza skuli alikuwa dubwahsa haswa ila alikuwa pia na skills za kuchezea chapati (disco) nadhani ndo ikawa stepstone ya kukutana na marehemu Steve 2K (Rip).

Nilikutana na Marehemu Steve ktk studios fulani maeneo ya mwenge akiwa na kina Mjema (Rip) na spider, jamaa alikuwa mcheshi sana, ila one thing akishadhania kwamba hauko sahihi naye basi anakutoa nishai sawia, hivyo pia ule ujasiri wake nadhani hakuutumia vyema ktk ugomvi na Castrol, Tatizo jengine ni kuwa pombe ndizo zilikuwa zinapunguza ule ucheshi wake na kuwa mgovi. Ila mshikaji alikuwa imara kweli na ilibidi promota akatambike kwanza kabla ya kuingia deal na Mambo poa. Walikuwa hawadhulumiki wale (i like that).

Kibaya zaidi ni kuwa tumepoteza wasanii na vijana ambao walikuwa hawana kashfa kama za hawa bongo fleva wa sasa....
 
Katutoka jana.

Habari zaidi zitawajia kuhusu alivyoanza kuchizi hadi kifo chake pamoja na historia ya maisha yake.

RIP John Mjema

duh RIP John Mjema...

i cudnt bliv kuwa jamaa kama huyu cud decide to end up maisha yake kwa kujinyonga..anyways hapa naona kama umeandika alichizika..wat was nyuma ya kuchizika kwake??cud it b mibangi yao?
 
Mwanamuzi wa kizazi kipya ajiua kwa kisu Dar
Na Beatrice Charles

MSANII wa muziki wa miondoko ya Bongo Fleva, John Mjema amejiua kwa kujipiga kisu,polisi wamethibitisha jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Kandihabi alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 12:00 jioni, Mtoni Kijichi eneo la Neluka na kwamba msanii huyo alijichoma na kujichinja sehemu ya shingoni.

Kamanda Kandihabi alisema mmoja wa ndugu wa marehemu ambaye alitoa taarifa kwa polisi, Michael Kassim (20) alisema mjomba wake anadhaniwa kuwa alikuwa ameathirika na ugonjwa wa ukimwi.

?Tulikuwa tikimsikia akisema mara kwa mara kuwa yeye ameathirika,? alisema Kassim.

Akizungumza na gazeti hili katika ofisi za Mwananchi jirani wa marehemu ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema marehemu Mjema alikuwa anaumwa kwa muda mrefu na kwamba alikuwa ameanza kuchanganyikiwa akili, hali ambayo ilimfanya afikie hatua ya kuanza kuvua nguo.

Alisema kabla ya kufariki Mjema alikuwa chini ya uangalizi wa ndugu zake kutokana na majaribio ya kutaka kujiua.

?Alitaka kujiua kipindi cha nyuma, lakini siku ya tukio ndugu zake hawakuwepo nyumbani ndipo yeye akapata nafasi ya kujiua kwa kutumia kisu,? alisema jirani huyo.
 
Mugo"The Great";140177 said:
Mwanamuzi wa kizazi kipya ajiua kwa kisu Dar
Na Beatrice Charles

?Tulikuwa tikimsikia akisema mara kwa mara kuwa yeye ameathirika,? alisema Kassim.

Mjema alikuwa anaumwa kwa muda mrefu na kwamba alikuwa ameanza kuchanganyikiwa akili, hali ambayo ilimfanya afikie hatua ya kuanza kuvua nguo.

Alisema kabla ya kufariki Mjema alikuwa chini ya uangalizi wa ndugu zake kutokana na majaribio ya kutaka kujiua.

Pumzika kwa amani John,

Matukio ya wengi kujimaliza baada ya kujua/kuhisi kuwa wamepata VVU, yanaongezeka.
Hapa kuna tatizo, nafikiri katika system nzima kuanzia kwenye ushauri nasaha hadi kwenye social support/post counseling.

Binasfi haya maneno 'kuathirika' na 'kuishi kwa matumaini' siyapendi na ninaona yana ashiria unyanyapaa.

kitengo cha ustawi wa jamii kiwezeshwe, ilikuwapa nafasi kina John Mjema kuendelea kuishi.
 
apumzike kwa salama

kwa kweli hili ni darasa kwetu na wanaohusika na masula ya ukmwi kuna mapungufu ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi.

kwa kweli hata rais wa nchi alinukuliwa akiwa na mawazo yasio salama alipoenda kupima.
anaeleza kuwa akifikiri ni vp hali itakuwa akionekana na ngoma.

ina maana kila mtu huwa na mawazo mabaya na kujiona ndio kwisha

sasa kazi ifanyike wajihisi kuwa yea wana ngoma na wanaweza kuishi kama kawaida badala ya matumaini
 
Duh,,ndugu zanguni yule mkuu alieimba wachumba telathini
ameamua kukatiza maish yake kwa sabababu ambazo mpaka sasa
aijajulikana,,,ndugu walipoulizwa walidaai aliwaambia alikuwa na matatizo ,na aliathirika,,hapa kidogo tumeshindwa kuelewa...
habarizaiidi,,,soma uhuru ya leo..mungu amlaze mahali pema peponi kakayetu..
 
habari znazosomeka kutoka kwenye gazeti la uhuru..alipata uchizi,,na kumalizia aliathirika ,,hapa kidogo matata
mungu amlaze mahali pema peponi
Amina
 
Wanasema majani ndio yamechangia yote hayo..alichizi akapelekwa milembe aliporudi ndo ngoma ikadata zaidi....Jani nomaa wasanii wa bongo...
Kama wale TMK ipo siku nao watakuja data inaeleweka wazi kuwa hawapandi kwa stage bila kupuliza..mabalaa yake ndo hayo msongo wa mawazo unaamua kupiga mkameme..
 
Daah
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom