Hamduni
Senior Member
- Apr 25, 2020
- 155
- 108
Katibu wa NEC Itakadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi amesema Tanzania tunahitaji uwekezaji bandarini kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania, ameyasema hayo alipotembelea vyombo vya habari vya Africa Media Group Limted; Magic Fm na Channel Ten Plus mapema leo tarehe 20 Julai, 2023
Katika ziara hio Ndugu Mjema ametoa ufafanuzi kuhusu suala la uwekezaji wa bandari kati ya Tanzanina na Dubai na amewatoa hofu Watanzania kuwa uwekezaji wa Bandari unaotarajiwa kufanywa na Kampuni ya DP World utaipaisha Tanzania kwenda nchi zIlizoendelea katika kipindi cha miaka kumi ijayo.
Aidha Mjema amesema suala la uwekezaji sio geni katika bandari ya Dar es Salaam kwani ilikuepo kampuni moja inaitwa TICTS lakini haikuweza kuwapa Watanzania wanachostahili na ndio maana wanatafuta kampuni yenye uwezo zaidi.
"Uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam sio jambo geni, pale kulikua na kampuni inaitwa TICTS lakini bado kama nchi hatujaweza kupata tunachotaka ndio maana tunataka kuleta kampuni yenye uwezo mkubwa zaidi" alisema Mjema
Pia Ndugu Mjema amesema kuwa uwekezaji wa Bandari unaotarajiwa kufanywa na Kampuni ya DP World kwenye Bandari ya Dar es salaam utatoa fursa za kuhaulisha ujuzi kwa watanzania, kutoa ajira pamoja kuongeza pato la taifa.
Mwisho Mjema amewaasa wananchi kuendelea kuiunga mkono Serikali inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani anayo nia ya dhati ya kufanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kuboresha maisha ya Watanzania.