babu M
JF-Expert Member
- Mar 4, 2010
- 5,221
- 3,167
Mimi nitafurahi sana kuona Mtanzania mwenzangu akiwekeza zaidi ya investor kutoka nje.Home shopping Centre
Si heri hiyo pesa aizungushe nchini kuliko kuwapa ma Bank ya wazungu wazitumie?Hiyo hela ya kujenga kiwanda inatoka wapi?Tujue hilo kwanza.
Hahahaha. ...ama kweliMtoa mada ni muongo nimeona taarifa ya habari channel ten mh mbunge ametembelea ujenzi unaoendelea jimboni kwake, kiwanda ni cha twyphord
Duh. ..Hongera kwa mwekezaji!
Dola milioni 56 sio mchezo!
Twyford bathrooms ni kampuni maarufu sana ya iliyopo UK na ipo chini ya Geberit Group ya Europe.
Twyford ceramics Ltd ya hapa Tanzania bidhaa zao sasa hivi wana import kutoka China. Sidhani kama kuna huusiano wowote na Twyford ya UK ambayo walishakana bidhaa zao hazitoki China.
Hata hivyo good move. .Wakurupukaji wengi humu.
Twyford ni generic tile makers wa uchina. Unahitaji kupita kkoo nusu saa tu kulijua hilo. Ni mwendelezo wa generic tile makers kama goodone etc. Ofcourse ni vikampuni vidogo visivyo na majina duniani na hata huko uchina vinakotoka.
Kutokana na hilo target yao kuu ni vinchi vyetu vidogo visivyo na purchasing power ya kununua expensive tiles and ceramics. Kutokana na soko kukua ni vema wao kufanya uzalishaji nchini. Kumbuka tiles nzito na volumetric.
Mtoa pesa sio ridhiwani,yeye ni muwezeshaji kama wanunge wote walivyo.
Acha blah blahhuwa sifanyi miradi ya kitoto wewe,mashine ya pampers unaweza hata kuifunga chumbani ukalala nayo
Nimependa kuona kwamba Ridhiwani hajabweteka kwa sababu ya jina kubwa la Baba. He wants to leave behind something tangible. Safi sana.Interesting great minds of Tanzania are sons and daughters of ruling class.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ameanza harakati za kujenga kiwanda cha 'Tiles' katika jimbo lake ambacho kinaweza kuja kutoa ajira kwa watu zaidi ya elfu sita nchini.
Ridhiwan Kikwete amesema kazi yake ni kutafsiri malengo mema aliyonayo Rais John Pombe Magufuli ya kujenga Tanzania ya viwanda kwa vitendo na kudai lengo kubwa la kujenga kiwanda hicho ni pamoja na kutoa ajira kwa vijana na wakina mama.
"Kitakapokamilika Kiwanda cha Tiles Twyford- Chalinze kinataraji kuajiri wafanyakazi rasmi 2000+ na Wasio Rasmi 4000+ na hii kazi ninayofanya ni kutafsiri malengo mema aliyonayo Rais na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa vitendo. Malengo makubwa ni kutoa ajira kwa vijana na wakina mama. Mungu anatusimamia tutafikia malengo tuliyojipangia" alisema Ridhiwan Kikwete.
Mbali na hilo Mh Ridhiwan Kikwete amedai kiwanda hicho kikikamilika malighafi zake za uendeshaji wa kiwanda hicho zitakuwa zikitoka Iringa, Kilimanjaro, Vikindu, Pugu, Morogoro na Tanga na kusema zaidi ya asilimia 90 ya malighafi zitakuwa zikitoka hapa hapa Tanzania.
"Malighafi Zitatoka Iringa, Kilimanjaro, Vikindu,Pugu, Morogoro, na Tanga. Yaani 90 percent inatoka Tanzania. kwa sasa akili, mwili na nguvu iko Chalinze. Inatakiwa nianze na Chalinze ndiyo nitabadili Tanzania kwa watu kuiga mfano wangu" alisisitiza Mh. Ridhiwan Kikwete
Source:Eatv News
Kila Mbunge akiacha siasa na kufikiria na kufanya maendeleo, hivyo kila jimbo likawa na kiwanda, tutakuwa na viwanda vingapi baada ya miaka 6. Halafu 2020 tukarudi kwenye siasaHongera kwa mwekezaji!
Dola milioni 56 sio mchezo!