Ridhiwani Kikwete Kujenga Kiwanda Cha "Tiles" Chalinze

Fukara

JF-Expert Member
Dec 28, 2013
1,625
928
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ameanza harakati za kujenga kiwanda cha 'Tiles' katika jimbo lake ambacho kinaweza kuja kutoa ajira kwa watu zaidi ya elfu sita nchini.

Ridhiwan Kikwete amesema kazi yake ni kutafsiri malengo mema aliyonayo Rais John Pombe Magufuli ya kujenga Tanzania ya viwanda kwa vitendo na kudai lengo kubwa la kujenga kiwanda hicho ni pamoja na kutoa ajira kwa vijana na wakina mama.

"Kitakapokamilika Kiwanda cha Tiles Twyford- Chalinze kinataraji kuajiri wafanyakazi rasmi 2000+ na Wasio Rasmi 4000+ na hii kazi ninayofanya ni kutafsiri malengo mema aliyonayo Rais na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa vitendo. Malengo makubwa ni kutoa ajira kwa vijana na wakina mama. Mungu anatusimamia tutafikia malengo tuliyojipangia" alisema Ridhiwan Kikwete.

Mbali na hilo Mh Ridhiwan Kikwete amedai kiwanda hicho kikikamilika malighafi zake za uendeshaji wa kiwanda hicho zitakuwa zikitoka Iringa, Kilimanjaro, Vikindu, Pugu, Morogoro na Tanga na kusema zaidi ya asilimia 90 ya malighafi zitakuwa zikitoka hapa hapa Tanzania.

"Malighafi Zitatoka Iringa, Kilimanjaro, Vikindu,Pugu, Morogoro, na Tanga. Yaani 90 percent inatoka Tanzania. kwa sasa akili, mwili na nguvu iko Chalinze. Inatakiwa nianze na Chalinze ndiyo nitabadili Tanzania kwa watu kuiga mfano wangu" alisisitiza Mh. Ridhiwan Kikwete

Source:Eatv News
 
Safi mwana CCM mwenzangu kijana, congrats..!! Call you later Riz..!!
 
Ni hatua nzuri kwake.......

Lakini awe tu makini na anayetaka walioishi kama malaika waishi kama mashetani............

Yasimkute na Dangote &com.....

Nitafurahia mpango wake kukamilika maana ni furaha kwa watu tusio na Mawazo ya kimasikini............
 
UZURI WA VIJANA WETU CCM WANAUBUNIFU WENYE WEREDI
sio wale wengine kazi kujizo ya kutukanana
Katika mijitu mijinga hakika wewe ni mjinga,yaani kila wakati unawaza uitikadi wa chama.Hakika wewe ni mburula.

NB:Hongera R.Kikwete kwa jitihada zako niimani yangu ajira zitakazotolewa ni kwa ajili ya watanzania na bidhaa zitakazo zalishwa ni kwa mstakabari wa watanzania.Mungu akutangulie ufanikishe lengo lako.
 
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ameanza harakati za kujenga kiwanda cha 'Tiles' katika jimbo lake ambacho kinaweza kuja kutoa ajira kwa watu zaidi ya elfu sita nchini.

Ridhiwan Kikwete amesema kazi yake ni kutafsiri malengo mema aliyonayo Rais John Pombe Magufuli ya kujenga Tanzania ya viwanda kwa vitendo na kudai lengo kubwa la kujenga kiwanda hicho ni pamoja na kutoa ajira kwa vijana na wakina mama.

"Kitakapokamilika Kiwanda cha Tiles Twyford- Chalinze kinataraji kuajiri wafanyakazi rasmi 2000+ na Wasio Rasmi 4000+ na hii kazi ninayofanya ni kutafsiri malengo mema aliyonayo Rais na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa vitendo. Malengo makubwa ni kutoa ajira kwa vijana na wakina mama. Mungu anatusimamia tutafikia malengo tuliyojipangia" alisema Ridhiwan Kikwete.

Mbali na hilo Mh Ridhiwan Kikwete amedai kiwanda hicho kikikamilika malighafi zake za uendeshaji wa kiwanda hicho zitakuwa zikitoka Iringa, Kilimanjaro, Vikindu, Pugu, Morogoro na Tanga na kusema zaidi ya asilimia 90 ya malighafi zitakuwa zikitoka hapa hapa Tanzania.

"Malighafi Zitatoka Iringa, Kilimanjaro, Vikindu,Pugu, Morogoro, na Tanga. Yaani 90 percent inatoka Tanzania. kwa sasa akili, mwili na nguvu iko Chalinze. Inatakiwa nianze na Chalinze ndiyo nitabadili Tanzania kwa watu kuiga mfano wangu" alisisitiza Mh. Ridhiwan Kikwete

Source:Eatv News
Sasa sisi inatuhusu nini?
 
Mtoa mada ni muongo nimeona taarifa ya habari channel ten mh mbunge ametembelea ujenzi unaoendelea jimboni kwake, kiwanda ni cha twyphord
 
Back
Top Bottom