Ridhiwani Kikwete agawa pikipiki kwa watendaji na vifaa tiba jimboni kwake Chalinze

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,896
22,666
Alhamisi jimboni Chalinze. Nimegawa pikipiki kwa watendaji wa kata 6 za Halmashauri yetu ya Chalinze, kutembelea kiwanda cha Uzalishaji wa marumaru cha Keda, na kupokea vifaa tiba kwa ajili ya Vituo vya Afya viwili Kata za Kibindu na Msata na Zahanati vijiji 11.

Wakati tunakwbidhi pikipiki, tumewakumbusha Watendaji kutumia vifaa hivi kuzingatia makusudio ya kutolewa kwake. Wakawasikilize wananchi na kutoa ufumbuzi wa changamoto zao.

Tukikabidhi vifaa tiba tumewahimiza kuvitunza na kuvitumia kwa makusudio yake. Kazi kubwa inaelekezwa Kituo cha Afya Miono ambapo kazi ya ujenzi wa miundo mbinu inapaswa kuwa kipaumbele. Kwa upande wa kiwanda tumewashukuru wawekezaji kwa kutambua mchango wa Rais Samia Suluhu.

#KaziInaendelea

USSR
IMG-20230217-WA0004.jpg
IMG-20230217-WA0002.jpg
IMG-20230217-WA0003.jpg
IMG-20230217-WA0001.jpg
 
Hongera the end justifies the means.

Ila pesa imetoka kwenye mfuko wa Jimbo, wadau au yeye mwenyewe ametoa kama msaada? Sababu tunaposema amegawa huenda na wengine wakaanza kuuliza mbona kwetu mbunge wetu hagawi kitu; Kumbe sio kazi yake au hana means.
 
Back
Top Bottom