Ridhiwani JK, ona na hawa!!

Siku hizi Mh. Rais anaiogopa kauli mbiu yake ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania kama ukoma.

Ni kipindi kirefu sasa sijamsikia akitamka kauli hii, sijui safari hii atakuja na kauli mbiu gani???
KAULI MBIU YA MWAKA HUU;
Tanzania bila ukimwi inawezekana,
Malaria haikubaliki.
 
sijaelewa kwa nini unaadress issue hii kwa ridhiwani. Who is he?
 
Ndio wanafanya ziara za mawaziri soon kuwaeleza watanzania mafanikio kama hayo jamani msiwalaumu....
 
na mimi najiuliza hili swali,,,kwani uyu bwana kikwete jr ni nani hasa katika hili la kutudharirisha wanafunzi wa taifa la badae?
inaniuma sana hii hali,ilhali watu/mafisadi wanatafuna nchi,watu wanaweza jichanga bil 50 kwa kampeni,mlahaba wa madini,mashirika ya uma kuuzwa kiholela.
kuna wau jehanamu itawatapika jamani...maisha gani haya sasa???!!
 
MENE MENE TEKELI NA PERES....sijui kama nimepatia, ila anguko la ufalme huu litakuwa kuu kuliko mnavyodhani. Gharama ya kuingiza watoto wote kwenye siasa za uzandiki kama hizi si ndogo. Ikitokea mapinduzi, ndo kizazi kizima kitaisha...inanikumbusha Bushelvic Revolution kule Russia, ambapo Czar na familia yake walifyekwa wote. Na hata waliosalimika hawathubutu kutumia jina la ukoo ule wa kifalme, maana watmalizwa. Siwaombei mabaya, ila kuna watu wameizunguka hii familia na hawairuhusu ipate mahali pa kuwaza kwa maslahi yao. Mke yuko busy kwenye siasa, baba, watoto, nani wa kuwashauri? Mwisho watajikuta wote wamo katika kila kashfa...na endepo anguko lao litatoke ( na si mbali) basi litakuwa kuu. Hapo ndipo mtashuhudia familia nzima ikisimama kwenye mahakama kwa aibu kuu. Ni maneno yanyoudhi, ila haihitaji PHD kuona mwisho wa ufalme huu. JK yabidi atafakari......washauri wake ndio wanamuingiza king, hawaonekani wao, ila yeye na familia. La UVCCM ni dokezo ya haya

naam umenena
red color=kitabu cha Daniel katika biblia,ili kudhibitisha anguko la ufalme wa dhulma na utesaji wa raia wake...

kuuza sura huku??
 
Ngoshwe ahsante kwa kutukumbusha kwamba badala ya Ridhiwani kukomalia kuibui ubaya wa masauni angalie pia upande wa mafanikio wa baba yake kwa kujenga shule nyingi za nyasi na zisizo na madarasa na waalimu
 
nilishangaa niliposikia huyu jamaa yupo kwenye sakata la masauni,ilhali baba yake ndio kamchagua...ina maana baba hakusoma wasifu wa masauni kwa undani mpaka mtoto aje kuuibua?????????mhhhhhhhhh ila kiongozi wetu ni mvivu wa kusoma jamani...hata kufuatilia wasifu wa mtu anayemchagua kwa kazi kubwa namna hiyo pia imempa shida???
 
nilishangaa niliposikia huyu jamaa yupo kwenye sakata la masauni,ilhali baba yake ndio kamchagua...ina maana baba hakusoma wasifu wa masauni kwa undani mpaka mtoto aje kuuibua?????????mhhhhhhhhh ila kiongozi wetu ni mvivu wa kusoma jamani...hata kufuatilia wasifu wa mtu anayemchagua kwa kazi kubwa namna hiyo pia imempa shida???
Natamani ningejua ratiba ya kila siku ya Mh.rais. Hivi hawa ma rais walivyo na majukumu mengi yanayowasubiri mezani,mimi huwa naona labda inabidi wawe na wasaidizi wa maana na waangalifu sana. Sijui anasoma makaratasi mangapi kwa siku,ukichukulia kuwa watu wa kawaida wanashindwa hata kusoma gazeti moja kila siku. Kama raisi huwa naona anapelekewa magazeti zaidi ya 12,sijui kuna mikataba ya Barrick,makesi etc lakini bado watu wengine nao wamo wanataka kwenda huko,mmmmh matokeo yake mnaonekana wavivu!
 
Hayo ndio maisha bora kwa kila mtanzania. Watanzania ufahamu wetu umefungwa. Mungu atusaidie. Amen
 
Back
Top Bottom