Ridhiwani JK, ona na hawa!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ridhiwani JK, ona na hawa!!

Discussion in 'Celebrities Forum' started by ngoshwe, May 8, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  HII NDIO TOFAUTI YETU:  RIDHIWANI, sijajua vigezo vilivyotumiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (The Tanzania Education Authority) kuwapata wahamasishaji wa kuchangia mfuko wa kununulia vifaa kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum (students with disabilities) na hata pia mazingira ya kuandalia matangazo haya ambayo yanaonyesha hali halisi ya utofauti wa maisha katika familia za watanzania (ukiwa katika ofisi ambayo ina kila dalili ya neema na vitendea kazi).

  Labda pengine katika hali njema kama hapo ulipo, ebu jaribu pia kutupa jicho lako binafsi huko chini ili kuona tofauti ya matabaka tunayojaribu kuyatengeneza katika nchi hii ambayo ina zaidi ya miaka arobaini ya kujitawala, ebu waone pia hawa ambao ni watanzania kwa kuzaliwa na wamekuwa wakiitumaini Serikali hii hii ambayo inawawezesha wengine kuwa na hali bora hata ya kuweza kuonekana katika mazingira ya gharama: ZUNGUMZA NASI KWA MZINGIRA HALISI YA KITANZANIA ILI IMAANISHE KWELI TUPO PAMOJA NA "KWA PAMOJA IWEZEKANE KWA KILA MMOJA WETU KUFURAHIA MATUNDA YA UHURU WETU KWA MAANA YA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA!!":

  [​IMG]
  Wanafunzi wa shule ya Msingi Kinole, katika halmashauri ya wilaya ya Morogoro, wakiwa wamekaa chini kutokana na uhaba mkubwa wa madawati unaoikabili shule hiyo

  [​IMG]

  Mwalimu, Albert Juakali wa shule ya msingi Iboma iliyopo kijiji cha Udinde Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya akifundisha wanafunzi wa darasa la kwanza chini ya Mti wa Mbuyu

  [​IMG]
  [​IMG]

  [​IMG]
  [​IMG]
  Shule ya Msingi Juhudi - Kigoma Vijijini, Tanzania
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Naskia kichefuchefu...CCM hawana haya kweli...!!
   
 3. Mkereketwa

  Mkereketwa JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2010
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli usemi wa maisha bora kwa kila mtanzania is a fantasy not a reality!!!!!
   
 4. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  [​IMG]ana uwezo mkubwa wa kutafuna huyu, heheeeee, yaani nimecheka mpaka basi
   
 5. p

  pori Member

  #5
  May 20, 2010
  Joined: Mar 12, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wadau, kwa kweli hiyo avator ya mkereketwa imenichekesha kupita kiasi. stress zangu kidogo zimepungua kwa kucheka. ama kweli laugher is the best medicine on earth!
   
 6. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sasa, Mamlaka ya Elimu ya Juu (or whatever its called) ina maana gani kumtumia R J Kikwete kwenye hili tangazo? Hata kama wana nia njema, WHO IS RIDHIWANI KIKWETE???

  Sasa yale mambo ya maana ya kutumia wasanii wenye influence katika jamii ndio wanaweka watoto wa viongozi.

  Nonsense!
   
 7. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Ni mtoto wa mfalme, ni kijana ambaye ana influence kuliko vijana wote, msomi kuliko vijana wote, ana kazi nzuri na anayefuata nyayo za Baba

  Ikumbukwe ma architectures wa haya mambo wanajikomba kwa mzee na kwakuwa Nchi ishakuwa ya kifalme dogo lazima aingie kwenye siasa ili one day aje kukalia kiti cha mzee by the way wametoka kwenye familia ya kichief - Tz kila kitu kinawezekana ili mradi tu uwe connected
   
 8. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  I like your sarcasm P Son.

  Halafu ndio nini kuongea na yale mawireless headsets na madudu mengine? Ndio usomi? Au ndio uchapakazi au? Lakini labda waliokuwa wanashoot hilo tangazo hawakumshauri mwenzao vizuri, wangeshoot walau kwenye mazingira ya shule moja wapo aliyochangia na mmoja wa hao watoto.

  Still, I am not impressed. I am pissed!
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kichefuchefu tupu
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  May 21, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  sijui tutafika?
   
 11. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #11
  May 21, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hebu wandugu mjiulize yale mapesa walikuwa wakichangushana ili kukomba jimbo la moshi si wangesaidia watoto hawa?
  Au nakosea wandugu? Hebu tukubaliane basi
   
 12. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Hivi Tsh 6 bilion zingeweza kusaidia shule ngapi za aina hii?
   
 13. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #13
  May 21, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Wizi mtupu.....
   
 14. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #14
  May 21, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Hata Wachaga ndugu zangu wamekuwa waswahili!
   
 15. M

  Myamba Senior Member

  #15
  May 21, 2010
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Shida ya nchi hii ndugu yangu ni namna ya kuchagua priorities. Wao wanachojua na kukipenda ni kuchukua maelfu ya shilingi kama imprest za safari za mikoani na ughaibuni wakati wananchi wakiwa na hali duni za maisha.

  Tatizo jingine ni kuwa sisi wananchi tunadanganyika na kusahau kwa haraka sana, na kama tungekuwa makini, CCM haingekuwepo madarakani leo!
   
 16. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #16
  May 21, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ongezea ana madaraka kuliko baadhi ya Mawaziri!
   
 17. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #17
  May 21, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  BAdo nimelala,nikiamka nitatumbukiza kitu kwenyewe!
   
 18. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #18
  May 21, 2010
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mawe 005.JPG
  Hiyo ni shule ya Msingi mojawapo huko Sikonge, Tabora. Eneo hili ni maarufu kwa uaribifu wa mazingira kupitia kilima cha tumbaku. kupitia uaribifu wao Halmashauri (W) Sikonge inapata mamilioni ya ruzuku kutoka kwa wanunuzi wa tumbaku huku wakulima wakibaki na madeni ya pembejeo.
   

  Attached Files:

 19. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #19
  May 21, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Siku hizi Mh. Rais anaiogopa kauli mbiu yake ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania kama ukoma.

  Ni kipindi kirefu sasa sijamsikia akitamka kauli hii, sijui safari hii atakuja na kauli mbiu gani???
   
 20. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #20
  May 21, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  MENE MENE TEKELI NA PERES....sijui kama nimepatia, ila anguko la ufalme huu litakuwa kuu kuliko mnavyodhani. Gharama ya kuingiza watoto wote kwenye siasa za uzandiki kama hizi si ndogo. Ikitokea mapinduzi, ndo kizazi kizima kitaisha...inanikumbusha Bushelvic Revolution kule Russia, ambapo Czar na familia yake walifyekwa wote. Na hata waliosalimika hawathubutu kutumia jina la ukoo ule wa kifalme, maana watmalizwa. Siwaombei mabaya, ila kuna watu wameizunguka hii familia na hawairuhusu ipate mahali pa kuwaza kwa maslahi yao. Mke yuko busy kwenye siasa, baba, watoto, nani wa kuwashauri? Mwisho watajikuta wote wamo katika kila kashfa...na endepo anguko lao litatoke ( na si mbali) basi litakuwa kuu. Hapo ndipo mtashuhudia familia nzima ikisimama kwenye mahakama kwa aibu kuu. Ni maneno yanyoudhi, ila haihitaji PHD kuona mwisho wa ufalme huu. JK yabidi atafakari......washauri wake ndio wanamuingiza king, hawaonekani wao, ila yeye na familia. La UVCCM ni dokezo ya haya
   
Loading...