Ridhiwan, Lowassa waelezea utajiri wao

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2011
Messages
27,508
Points
2,000

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2011
27,508 2,000
Waziri Mkuu aliyejiuzuru Mh.Edward Lowasa ameendelea kutapatapa katika medani za siasa. Safari hii amejitetea kuwa hana utajiri wa kutisha kama maadui wake wanavyomchafua, badala yake ana utajiri wa ''kutisha'' wa watu wenye mapenzi nae

Source: Tanzania Daima

Kutoka gazeti la Mwananchi:

Ridhiwan, Lowassa waelezea utajiri wao

Jumatatu, Novemba26 2012 | Mwananchi

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwan wamezungumzia tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa kwao kwamba wanamiliki rasilimali zenye thamani ya mabilioni ya shilingi.

Lowassa kwa upande wake amekuwa akidaiwa kuwa tajiri anayemiliki kampuni kubwa za kibiashara na kumekuwa na taarifa kwamba ana ukwasi ambao vyanzo vyake vinatia shaka na siyo rahisi kuvitolea maelezo.

Kwa upande wake Ridhiwan naye amekuwa akidaiwa kuwa na utajiri mkubwa na amekuwa akihusishwa na biashara za kampuni za kusafirisha mafuta ambayo hupelekwa kwenye migodi, umiliki wa hoteli na majengo kadhaa ya kifahari.

Wote wawili wamekuwa wakidaiwa kwamba baadhi ya mali zao wamekuwa wakiziendesha chini ya kivuli cha wafanyabiashara wengine wakubwa nchini ili kukwepa kuhojiwa walikotoa utajiri huo, taarifa ambazo hata hivyo imekuwa vigumu kuzithibitisha.

Hata hivyo jana kwa nyakati na mazingira tofauti, Lowassa na Ridhiwan walijitokeza hadharani na kukanusha madai kwamba wao ni matajiri wa kupindukia.

Lowassa kwa upande wake akiwa mjini Mbeya alisema yeye siyo tajiri kama ambavyo imekuwa ikidaiwa lakini wakati huohuo akasema "sijafilisika".

"Wengi wanasema kuwa mimi ni tajiri siyo kweli, lakini sijafilisika kutokana na kuchangia makanisa kwani nina marafiki wengi ambao wananisaidia katika kuchangia makanisa nao pia hawajafilisika,"alisema Lowassa.

Lowasa alitoa kauli hiyo alipokuwa akiendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa hosteli ya wanachuo wanawake ambao ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Theofilo Kisanji cha mkoani Mbeya, kinachomilikiwa na Kanisa la Moraviani Tanzania, Jimbo la Kusini Magharibi.

Kiongozi huyo ambaye alichangia kaisi cha Sh25 milioni, alisema kila mtu ana wajibu wa kuchangia elimu na kwamba mwanamke anapaswa kutazamwa kwa karibu zaidi kwani ndiye anayebeba jukumu kubwa la kutunza familia.

Kwa upande wake Ridhiwan alisema: "Ikiwa mimi ni tajiri wa kiasi kinachosemwa, basi mimi ninamzidi Bakhressa (Said Salim, mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki), maana nimepewa kila hoteli hapa mjini, kampuni za mafuta na kila biashara kubwa inayoanzishwa hapa mjini ni ya Ridhiwan".

Said Salim Bakhressa ni mfanyabiashara ambaye anatajwa kuwa tajiri kuliko wote nchini na anashika nafasi ya pili katika nchi za Afrika Mashariki na Kati, huku akiwa miongoni mwa wafanyabiashara 10 wanaonyemelea kuingia katika nafasi za juu za utajiri Afrika.

Hata hivyo Ridhiwan ambaye hivi karibuni alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), aliongeza: "Ninaweza kuwa nafanya biashara moja au mbili, lakini siwezi kuwa mmiliki kiasi chote hicho cha mali.

Mtoto huyo wa Rais Kikwete alikuwa akijibu tuhuma kwamba magari yake kumi ya kusafirisha mafuta yamekamatwa na kuzuiwa katika mpaka wa Kenya na Tanzania, Namanga mkoani Arusha kutokana na kukwepa kodi, taarifa ambayo aliikanusha.

Maelezo ya Ridhiwan
Maelezo ya Ridhiwan yamekua wakati kukiwa na taarifa kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), inayashikilia malori mapya 10 ya kubebea mafuta yanayodaiwa kuwa ni yake, yanayodaiwa kuingizwa nchini.


Hata hivyo Ridhiwan alikanusha kuhusika na biashara ya mafuta akisema: "Ili kuwa na utajiri unaotajwa kwangu lazima niwe nimekopa benki au nimeiba, sasa wale wanaonituhumu wasema nimekopa benki gani na kama nimeiba basi wajitokeze watu kulalamika kuhusu wizi nilioufanya".

Mtoto huyo wa Rais Kikwete, alisema kumekuwa na kile alichokiita uzushi wa ajabu na kwamba hajui wanaozusha mambo hayo wana malengo gani. "Wameanza kusema kwamba nauza dawa za kulevya jambo ambalo siyo kweli, mie sifanyi biashara za aina hiyo, kama kuna jambo jingine tuunguze lakini hilo ni uzushi tu,"alisisitiza.

Habari zilizopatikana jana, zilidai malori hayo mapya yanashikiliwa na TRA kituo cha mpakani cha Namanga kwa madai ya kuwapo "utata" wa malipo ya ushuru wa forodha.

Taarifa za kuzuiwa kwa malori hayo zilianza kuzagaa nchini wiki mbili zilizopita kupitia mitandao ya kijamii ukiwamo mtandao maarufu wa Jamii Forums (JF).

Kulingana na taarifa hizo, watu walioshuhudia magari hayo walidai yalikuwa zaidi ya 70 yakitokea Kenya kutengenezwa bodi huku wengine wakidai yalikuwa ni mapya.

Baadaye taarifa hiyo ilibadilika na kusema kwamba magari hayo yalikuwa 20 na kwamba ni malori 10 tu ndiyo yaliyolipiwa ushuru na kuingia nchini, lakini malori mengine 10 yalikuwa yakiendelea kushikiliwa kutokana na ukwepaji wa kodi.

"Ni kweli hayo magari ni ya huyo bwana mkubwa na yalikuwa 20, lakini 10 yalilipwa ushuru halali"alidai ofisa mmoja wa TRA kituo cha Namanga.

Ridhiwan alisema kuthibitisha kwamba tuhuma hizo ni za uwongo haiwezekani mtu anayetajwa kuwa tajiri kama yeye ashindwe kulipia ushuru wa malori kumi.

"Uwongo mwingine huo, kama kweli ningekuwa nina utajiri wote huo, nishindwe kulipia ushuru wa malori kumi tu! Ndo maana nasema ni uwongo tena wa kutunga,"alisema.


Kaimu Meneja wa TRA Arusha, Theresia Mponeja alipulizwa na gazeti hili wiki iliyopita alikanusha kuzuiwa kwa malori hayo na kwamba hakuna taarifa hizo.

Lowassa na elimu

Katika hafla ya jana mjini Mbeya, Lowassa aliendelea kuipigia chapuo elimu akisema: "Ni vizuri vijana wetu wakazingatia elimu kwani bila elimu watashindwa kuhimili ushindani wa ajira katika Jumuiya ya Afrika Mashariki."

"Msipozingatia elimu mtabakia kuwa wachota maji na wakata kuni daima. Ni vizuri vijana wetu mkafahamu kwamba bila ya elimu hamtaweza kufika kokote,"alisema kiongozi huyo.

Aliwaasa wanafunzi wa kike kusoma kwa bidii ili kuweza kuboresha maisha yao na kuisaidia jamii, huku akitaka wajiepushe vishawishi ambavyo vimekuwa kikwazo katika masomo yao.

"Hata vitabu vitakatifu vya Mungu elimu imepewa umuhimu mkubwa, Biblia inasema mshike sana elimu na usimwache aende zake kwani huko ndiko uliko uzima wenu, kwa wenzetu Waislamu Quran inasema itafuteni elimu kwa bidii hata Uchina, maana ni kwamba itafute elimu hiyo hata kama utaipata mbali kiasi gani,'' alisisitiza Lowassa.


Akitoa taarifa ya chuo hicho, Kiongozi wa Kanisa la Moravian Tanzania, Askofu Alinikisa Cheyo alisema ujenzi wa hosteli hiyo ulianza 2011 na unatarajiwa kuwa na vyumba 87 vitakavyotoa fursa kwa wanachuo 348.

Alisema katika awamu ya kwanza ya ujenzi huo, kanisa liliomba mkopo kutoka mamlaka ya elimu Tanzania na kukubali kupewa Sh500 milioni na kwamba awamu hiyo iliyoanza Julai 2011, iligharimu Sh580 milioni.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Crispin Meela aliyemwakilisha mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, alisema Serikali inaunga mkono juhudi za sekta binafsi hususan madhehebu ya kidini katika kuchangia elimu.

Alisema kuwa kwa mujibu wa takwimu, madhehu ya dini yanaongoza kwa kuwa vyuo vikuu vingi. Chuo kikuu hicho cha Theofilo Kisanji kilianzishwa 2004, ingawaje kulikuwa na chuo cha Theolojia tangu miaka ya 1960.My Take:
Mzee (Lowassa) ni kama umegongwa muhuri wa moto wa ''ufisadi'' ikiwemo kuwaficha watanzania juu ya ufisadi wa Richmond, hakika muhuri huo wa moto hautafutika
 

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2011
Messages
27,508
Points
2,000

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2011
27,508 2,000
huyu mzee ngojwa lake lina msubua nilishikana nae mkono juzi mkono wake unatetemeka kama kapigwa shoti ya umeme ajifie tu maana kashaua wengi..
Huko kwenye gonjwa ni mbali sana, hata speech zake zimedoda sana.....umepata kuisikia speech yake ya Arusha, ni kama Mwenyekiti wa tawi Chadema
 

CRN

Member
Joined
Oct 24, 2012
Messages
60
Points
0

CRN

Member
Joined Oct 24, 2012
60 0
Mhalifu siku zote ni mtu wa kujistukia,EL hata nafsi yake huwa inamsuta pindi anapotoa speech,hajiamini hata kidogo,Wamasai ndiyo wamezoea speech zake,HAPO VIPI...........HAPO POA,Kazi kwelikweli.
 

Kageuka

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2012
Messages
241
Points
0

Kageuka

JF-Expert Member
Joined Jun 22, 2012
241 0
Waziri Mkuu aliyejiuzuru Mh.Edward Lowasa ameendelea kutapatapa katika medani za siasa. Safari hii amejitetea kuwa hana utajiri wa kutisha kama maadui wake wanavyomchafua, badala yake ana utajiri wa ''kutisha'' wa watu wenye mapenzi nae

Source: Tanzania Daima

My Take: Mzee ni kama umegongwa muhuri wa moto wa ''ufisadi'' ikiwemo kuwaficha watanzania juu ya ufisadi wa Richmond, hakika muhuri huo wa moto hautafutika
Ni kweli anao watu lakini ni wale walioko mfukoni mwake, watu aina ya Malisa, Bashe, Sadifa, Shigela, Millya na wengine wanaolipwa mapesa ya kula au kwenda kuhonga wengine. Manta kwa asemeje? Yaani aseme akina Bashe si watu? Ndiyo anao watu japo wapo mfukoni mwake na wengine wako naye ili kujipatia pesa.
 

Kwayu

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2007
Messages
489
Points
195

Kwayu

JF-Expert Member
Joined Nov 8, 2007
489 195
Hatuwezi kumpa mtu kimeo uraisi. akitufia hajamaliza hata mwaka? Hatutaki hasara ya kufanya uchaguzi mara mbili ndani ya miaka mitano
 

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined
Jun 4, 2011
Messages
6,728
Points
2,000

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined Jun 4, 2011
6,728 2,000
Kwa kweli juzi ndo ilikuwa Mara yangu ya kwanza Kumuona Huyu Mamvi kwa karibu kabisa tangu mwaka 1999 akiwa mkuu wa Bodi ya Shule Ya secondari ya Molinge Sokoine, Jamaa kwanza kazeeka sana tena sana, na anatetemeka vibaya,

Kilicho niacha hoi ni hotuba yake, Membe kumbe alikuwa akimsema huyu jamaa, kuongea jukwaani si kipaji chake kabisa, yeye ni pesa tu ndo inamfanya awe maalufu, Mwanzo mwisho ilikuwa Hapo vipi, hapo vipi, hapo vipi, hapo vipi,
 

Fpam

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Messages
290
Points
0

Fpam

JF-Expert Member
Joined Apr 28, 2011
290 0
tunakoelekea hata mimi litanijia wazo la kugombea urais maana sasa kila mtu anautaka huo URAHISI hadi kigwangala
 

Kageuka

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2012
Messages
241
Points
0

Kageuka

JF-Expert Member
Joined Jun 22, 2012
241 0
Kwa sera zake za ''Hapo vipi-Hapo poa''.....huyu Urais atauona tu kwenye TV,
Mkuu kwenye tv unawezaje kuuona urais? Hivi urais ni kitu tangible, mi nadhani unaweza kumwona Rais kwenye tv lakini si urais. Usijali lkn hoja yako inaeleweka huyu Baba Pamela Siyoi Sumari alishapoteza sifa za kufikiriwa na watu makini kama anafaa kuwa Rais, watu makini akina Nyerere walishaona Baba Pamela ni kimeo, nashauri awe Rais wa Saccoss, NgO yoyote Kama shida ni kuitana Rais
 

Eberhard

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2010
Messages
1,049
Points
1,500

Eberhard

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2010
1,049 1,500
Hakika huyu ndiye Rais ajaye
Kama kuna mtu anastahili kupewa urais CCM ni Lowassa tu. Hakuna na Mbembe wala mnafiki sitta. Wasiwasi wangu kuwa si unafahamu Lowassa ana wale mapacha wake( Siku hizi wanawaita mapacha watatu) Hivyo usishangae akamuweka Yule mzee wa vijisenti kuwa waziri mkuu na yule pacha mwignie (Rostam) kuwa waziri wa fedha. Kwa namna yeyote hile Lowassa haweza kumuacha Vijisenti. Vijisenti ana tuhuma amabazo hata mtoto mchanga anaweza kuzidhibitisha. Hata hivyo ataendendeleza siasa za visasi ambazo kwa sasa hatuziitaji. Tunahitaji maendeleo. Tumerudishwa nyuma sana. Tumenyonywa sana tena na watu wachache. Kwa hivyo ninaweza kusema Lowassa siyo sahihi. Rais sahihi wa kuwafikisha wa kuwaongoza watanzania kwa sasa atatoka chadema. Kwa upande wangu natuma karata zangu kwa slaa au profesa Safari. Zito naye hafai, ni mnafiki na asiyeeleweka kama sita, membe na magufuri.
 

naninibaraka

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2011
Messages
912
Points
1,000

naninibaraka

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2011
912 1,000
huyo Membe mumeo unayempigia debe ndio kimeo,ukiwezeshwa tu na hao mabwana zako unabaki kutokwa na povu hovyo,tunahitaj kiongozi mchapa kazi tumechoka na sanaa za bongo,hatutaki wanafiki na wapiga ramli,jk hakuna la mana zaidi ya sanaa,7 yrs Membe aliyokaa foreign affairs kafanya nini cha watz kumkumbuka?
 

Forum statistics

Threads 1,389,294
Members 527,903
Posts 34,022,436
Top