Ridhiwan Kikwete, Watu Wanakusema Vibaya

Hivi Ridhwani angekuwa mwanasiasa wa CHADEMA tungesema haya tunayoyasema juu yake? Je Ridhwani hana haki kisheria kuingia kwenye siasa kwa sababu tu baba yake ni mkuu wa nchi?
 
.
Ridhiwan ni nini? Ni kamati gani katika chama kipi cha Siasa? Maana naona mlolongo mwingi kumhusu mtu asie katika medani ya siasa za Tanzania. Naona ingekuwa vyema kuwajadili wale wanaomtuma kuliko kuwekea akili huyo anaetumwa.

Kiby,
Hebu matfute Francis Mponjoli Kifukwe(YANGA) na yule Masauni Masauni(UVCCM) ndio utamjua mwana wa sultani....Mtemi Kikwete II
 
Katika hili nimeamua kumfunga paka kengere,liwalo na liwe hata kama namgusa mtoto wa mpendwa Rais Jakaya Kikwete,Ridhiwan Kikwete

Niseme Wazi kiwa mimi kuwa mimi ni shabiki wake damudamu kiasi cha kuwa tayari kumwaga damu yangu kupambana na wale wanaomwonea wivu kwa ulaji anaoupata kutokana na kuzaliwa na kijiko cha dhaabu kwenye nasaba ya kifalme na Mzee kukupigia ''vuvuzela'' ili hapo baadaye naye aule.

Binafsi sioni ubaya kwa mwana kubebwa na baba au mwana kumpigia mdogo mdogo baba hata kuanza kujaribu kuvaa viatu vyake akiwa hai kama anavyofanya kikwete na Mwanae.

Sioni ubaya ukizingatia kuwa anachofanya Kikwete kwa Ridhwan ni kama walivyofanya watangulizi wengine kama vile mzee Abeid mwinyi,Hassan Mwinyi,John Malecela,Yusuph Makamba na wengine ambao wemevitengenezea vitegemezi vyao ulaji kwenye siasa.

Maana huo ni mfumo mzuri tuliokopa kwa wahindi ambao wametutawala kiuchumi nchini.Bila hiyo wale watoto wa wakubwa waliotuhumiwa hata kughushi wangekuwa wameishachukuliwa hatua.Lakini ni nyani gani anaweza kumsulubu ngendere wakati wote wala mahindi?

Sina nia ya kumtaka Ridhwan asijihusishe na mambo ya siasa wala mengine ya kijamii,lakini kasi ya mtoto huyo wa Rais inatisha na akiendelea hivyo ,gharama zake mambo anayofanya sasa ,zitabebeshwa kwa Rais kikwete tena kwa kuanzia kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Nimeamua kumwambia ukweli kwa sababu kubwa mbili za msingi,Mosi ni kwamba yeye ni mtoto wa Rais aliyoko madarakani na kama atashinda tena kwenye uchaguzi mkuu ujao .basi anaweza kuendelea ingawa safari hii,so rahisi kwake kushinda kama alivyofikiri.

Kwa Kutambua kwamba Ridhwan ni mtoto wa Rais ,Jamii inamwona kama kioo cha jamii kwa kila jambo alifanyalo.

Pili NimeMUA Kimwambia yanayozungumzwa hata na makada wenzake wa CCM ,kwani naamini hakuna anaweza kumwambia ukweli mtoto huyo wa Rais kutokana na tabia ya unafiki ya baadhi ya watu wa CCM ya kujikomba na kufikia hata hatua ya kulamba iatu vya wakubwa wa aina ya Ridhwan.

Nianze kwa kumpongeza kwa kazi kubwa kuhangaika kusaka wadhamini wa mzee wa Nchi nzima haikuwa kazi Nyepesi.Ni heshima na jukumu la pekee kwake na kwa vijana wote wa Taifa hili.

Pili Nimpongeze pia kwa kufanikisha Kimezengwe uchaguzi mkuu wa klabu ya soka ya Yanga hivi karibuni .Malalamiko yanaoendelea sasa dhidi yake kuhusu uchaguzi huo.

Nawajua vizuri sana wana yanga jinsi walivyo mahodari kuzungumza kwani baadhi wamefikia hatua ya kuamini kwamba Ridhwan alipata Maelekezo ya baba Yake (Rais Kikwete) ambaye naye ni Mnazi wa Yanga Kuhakikisha wagombea fulani hawapati nafasi Yanga.

Leo hii uchaguzi huo unalalamikiwa sana na sana baadhi ya wanachama wanatishia kwenda mahakamani na lawama nyingi zinaelekezwa kwa Ridhwan.

Yanayozungumzwa na kundi la wanayanga wanaopinga mgombea wao kufanyiwa fitna hadi kujitoa ,wanasema eti serikali ilihingilia uchaghuzi na wakati mwingine wanashindwa kumungunya maneno na kusema Ikulu ilihingilia Kati uchaghuzi wao.

Hii maan yake ni kwamba wamefika hatua ya kuamini Baba (Kikwete) kamtuma mwana kusimika viongozi anaowapenda wakati yawezekana Ridhwan aliyoyafanya hayana hata chembe ya mkono wa Rais Kikwete
Tatu nimpongeze kwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kuachia ngazi kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (uvccm) Masauni Yusuph Masauni hatimaye kiyi hicho sasa kinakaliwa na rafiki yake wa karibu aliyeemuunga mkono kwenye harakati za kuwania nafasi ya uenyekiti wa UVCCM Beno malisa ,kabla baba yake kuamuru nafasi hiyo iende Zanzibar.

Ridhwan ni shaidi katika hilo kwani mengi yaliandikwa kwenye vyombo vya habari juhu ya kuhusika kwake na mpango wa iliyomngoa masauni Madarakani.

Ridhwani mwenyewe amepata kukaririwa na baadhi na baadhi ya vyombo vya habari akikanusha,lakini wapo wanaoamini hasa wajumbe wa Baraza kuu UVVCCM Kutoka Zanzibar kwama alihusika kuwapoka kiti hicho.kama anabisha ajaribu kwenda Zanzibar.

Binafsi naomba nikupe ushauri wa bure.Ridhwan hebu angalia mifano ya watoto wa viongozi waliopita.wapo ambao hawakijulikana hata kwa majna yao na hili lilitokana na wao kutokuwa mbele kwenye shughuli za Baba zao walipokuwa Marais.

Ridhwan leo uko mbele ya kila kitu cha baba yako ,utadhani wewe ni Rais mdogo wa Nchi .wapo watu wanaohoji ukwasi wako wa sasa unaokufanya usione umuhimu wa kazi yako uliosomea ya kuvaa jihoo la uwaki naa kubishana na majaji mahakamani kutetea watuhumiwa.

Nakushauri ,achana na mambo hayo ,Vinginevyo utamponza Baba yako na kama unabisha subiri muda si Mrefu utajua ninacholisema

Full of rubish na umbea. Mod peleka hii takataka kwenye umbea hapa si mahali pake.
 
Huyu bwamdogo mmeamua kufanya celeb wakt sioni la maana toka kwake. Ana nini la kumfanya tumwongelee jamani, ana impact gani katika umasikini wa waTz? anasaidia nini ktk kupambana na usisadi!
 
Nyie huyu dogo manamuonaje? Mi naona hana ishu wala haja ya kujadiliwa hapa haipo! Ignore
 
kwa ushauri wangu angeenda kufanya kazi za kujitolea hata iwe vietnam nk akajifunza jinsi ya kuishi na watu na kuitumia elimu yake, baadae akirudi atakuwa mtu bora zaidi mwenye mawazo kujenga na kujitegemea.
 
Yote yataandikwa ila kwa ujumla wake ni kwamba watu wanataka kuwe na Social Mobility, nikimaanisha watu wa lower class nao wawe na chance ya kwenda middle na middle to higher and vice versa.

Ni muhimu kurekebisha hali hii, wanaokimbilia uongozi ni wale wale wa familia za juu kisiasa, kibiashara na kidini. Fursa sawa kwa wote na haki sawa kwa wote tafadhali!
 
Ingekuwa mie ndie Ridhwani ningefuatilia mambo yangu ya uwakili nikahakikisha nafungua nami ofisi yangu ya mawakili nijitahidi nichukue kesi za maana ziweze kunilipa na kunipandisha chati kuwa ni wakili bora mwenye kujua kazi yake. Hii ya kwenda kuwa KKKB ( Kula Kulala Kwa Baba) ningeachana nayo kwani nimeshakuwa mtu mzima nafamilia yangu inayo nitegemea.
Huu ni Ushauri wangu binafsi kwa Ridhwani

Ushauri mzuri sana huo Mkuu.

Naamini angetengeneza hela ya ajabu. Na angejenga jina kubwa sana kwake na firm yake. Ila kwa kupoteza muda kwenye mambo yasiyo na tija, Baba yake akimaliza muda wake, yeye atabaki akitafuta nani wa kumkomoa bila kujua kuwa nguvu za betri aliyokuwa kiitumia zimekwisha zamani.

"No matter how tall your father is, you have to take care of your own growth."
 
Ingekuwa mie ndie Ridhwani ningefuatilia mambo yangu ya uwakili nikahakikisha nafungua nami ofisi yangu ya mawakili nijitahidi nichukue kesi za maana ziweze kunilipa na kunipandisha chati kuwa ni wakili bora mwenye kujua kazi yake. Hii ya kwenda kuwa KKKB ( Kula Kulala Kwa Baba) ningeachana nayo kwani nimeshakuwa mtu mzima nafamilia yangu inayo nitegemea.
Huu ni Ushauri wangu binafsi kwa Ridhwani

Uwakili unahitaji juhudi binafsi la sivyo wateja watakukimbia. Sasa kwa haya yanayosemwa hapa JF, yaonekana kijana anawinda passive movement. Siyo mtu wa kufanya juhudi.na hisia zangu ni kwamba, alizoea tangu sekondari mpaka chuoni.

Kwa upande wangu naona mapungufu yako kwake na kwetu wa-TZ pale tunapohangaika kumpemdezesha hata mtu aliye uchi. Huko kote, UV-CCM na hata hapo Yanga SC, kweli huyu mtu alitoa pointi zilizowashawishi mpaka wakafuata yake? Au ni ile tukimuona tu tunapisha njia bila sababu.

Huyu hana wadhifa wowote nchi hii kwa nini awe na watu wenye akili timamu wakimfuata-fuata na kumsifu? Huyu aambiwe ajikaze na asitegemee nguvu ya baba.
Siasa hubadilika. Mbona watoto wa wanasiasa mashuhuri afrika hii wametumia nguvu zao? Angalia watoto wa Lumumba na Nkuruma! Hawa walikuwa na majina kuliko Kikwete mbali sana, sasa kwa nini mtu mwingine, mzembe tu, atusumbue?
 
Mwisho wa huyo dogo ni 1015. Hatutaki serikali za kisultan. Hatutaki. Wewe dogo ridhiwani baba yako akiondoka madarakani ndo mwisho wako. Nakushauri rudi kafanye shughuli zako za kiuwakili. amasivyo umekwisha huko ulipo.
 
Nyie huyu dogo manamuonaje? Mi naona hana ishu wala haja ya kujadiliwa hapa haipo! Ignore

Nadhani ni kwa sababu watu wanamuona anakuwa nuisance.

Jirani yangu hapa anasema anahisi anadekezwa na mzazi maana anaonekana kutumika na kusifiwa ktk majukwaa ya siasa. Sasa kwa kijana anayefahamu huko nyuma hakuwahi kusifiwa hata kuwa wa kwanza ktk mtihani, hilo linaleta ulevi.

Huko Morogoro nasikia ndo anajulikana kwa kuwekeza. Vituo vya mafuta na ujenzi wa magorofa wote unafanyika kwa jina lake hata sehemu zilizozuiliwa, ruhusa inatolewa. Tunajua hana kazi na hana kipato cha aina hiyo. Ina maana ni miradi ya baba.

Bahati mbaya yake itakuwa kama network ya baba itapotea ktk siasa kama ilivyo kwa Moi wa Kenya. Lakini kwa mtindo huu wa sasa atasifika bila kufungua mdomo.

Tuachane naye.
 
Unataka wamsemeje kama yeyebinafsi hamna jema alilolitenda?

He is a spoiled child; anafikiri urais wa baba yake ni wake pia!! Hopefully he will live to regret. Mtoto wa Saddam Hussein alikuwa na tabia kama ya Ridhwani na mambo yake yalikwisha vibaya.
 
He is a spoiled child; anafikiri urais wa baba yake ni wake pia!! Hopefully he will live to regret. Mtoto wa Saddam Hussein alikuwa na tabia kama ya Ridhwani na mambo yake yalikwisha vibaya.

Mfano mzuri sana! Huyu ndo Oudai saddam Hussein wetu kwa miaka hii maana naye alifikia hatua ya kuchapa viboko wachezaji wa timu ya taifa ya futiboli.
 
Hekima huanzia nyumbani.
kama mzazi akishindwa kudhibiti familia yake basi hatoweza asilani kudhibiti anaowaongoza nje ya nyumba yake.
 
Ingekuwa ni Kipindi cha Mwalimu Nyerere, Na Ridhiwani akawa mwanae, Nadhani hata hiyo form ya kuombea kuchangiwa asingejua inafanana je.

Nyerere angetambua mapema kwamba kichwa cha kijana ni kibovu na asingependa kujichafulia jina lake kwa kumzungusha mitaani mtoto wa jinsi hiyo.

Watoto wa familia za jinsi hii huwa wanaanguka vibaya sana..Beno pamoja na baba yake kustaafu ukuu wa magereza bado mzee huyo kapewa madaraka makubwa ndani ya system ili mradi ni kubebana kila kukicha.!

Hatuwaombei mabaya bali tuna jaribu kuwakumbusha kwamba, mchezo wa kubebana bebana unaweza kuwasababishia madhara makubwa huko tuendako.
Watu wamechoka na maisha, MSILISAHAU HILO.
 
Back
Top Bottom