Ridhiwan Kikwete, Watu Wanakusema Vibaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ridhiwan Kikwete, Watu Wanakusema Vibaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OgwaluMapesa, Jul 28, 2010.

 1. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2010
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Katika hili nimeamua kumfunga paka kengere,liwalo na liwe hata kama namgusa mtoto wa mpendwa Rais Jakaya Kikwete,Ridhiwan Kikwete

  Niseme Wazi kiwa mimi kuwa mimi ni shabiki wake damudamu kiasi cha kuwa tayari kumwaga damu yangu kupambana na wale wanaomwonea wivu kwa ulaji anaoupata kutokana na kuzaliwa na kijiko cha dhaabu kwenye nasaba ya kifalme na Mzee kukupigia ''vuvuzela'' ili hapo baadaye naye aule.

  Binafsi sioni ubaya kwa mwana kubebwa na baba au mwana kumpigia mdogo mdogo baba hata kuanza kujaribu kuvaa viatu vyake akiwa hai kama anavyofanya kikwete na Mwanae.

  Sioni ubaya ukizingatia kuwa anachofanya Kikwete kwa Ridhwan ni kama walivyofanya watangulizi wengine kama vile mzee Abeid mwinyi,Hassan Mwinyi,John Malecela,Yusuph Makamba na wengine ambao wemevitengenezea vitegemezi vyao ulaji kwenye siasa.

  Maana huo ni mfumo mzuri tuliokopa kwa wahindi ambao wametutawala kiuchumi nchini.Bila hiyo wale watoto wa wakubwa waliotuhumiwa hata kughushi wangekuwa wameishachukuliwa hatua.Lakini ni nyani gani anaweza kumsulubu ngendere wakati wote wala mahindi?

  Sina nia ya kumtaka Ridhwan asijihusishe na mambo ya siasa wala mengine ya kijamii,lakini kasi ya mtoto huyo wa Rais inatisha na akiendelea hivyo ,gharama zake mambo anayofanya sasa ,zitabebeshwa kwa Rais kikwete tena kwa kuanzia kwenye uchaguzi mkuu ujao.

  Nimeamua kumwambia ukweli kwa sababu kubwa mbili za msingi,Mosi ni kwamba yeye ni mtoto wa Rais aliyoko madarakani na kama atashinda tena kwenye uchaguzi mkuu ujao .basi anaweza kuendelea ingawa safari hii,so rahisi kwake kushinda kama alivyofikiri.

  Kwa Kutambua kwamba Ridhwan ni mtoto wa Rais ,Jamii inamwona kama kioo cha jamii kwa kila jambo alifanyalo.

  Pili NimeMUA Kimwambia yanayozungumzwa hata na makada wenzake wa CCM ,kwani naamini hakuna anaweza kumwambia ukweli mtoto huyo wa Rais kutokana na tabia ya unafiki ya baadhi ya watu wa CCM ya kujikomba na kufikia hata hatua ya kulamba iatu vya wakubwa wa aina ya Ridhwan.

  Nianze kwa kumpongeza kwa kazi kubwa kuhangaika kusaka wadhamini wa mzee wa Nchi nzima haikuwa kazi Nyepesi.Ni heshima na jukumu la pekee kwake na kwa vijana wote wa Taifa hili.

  Pili Nimpongeze pia kwa kufanikisha Kimezengwe uchaguzi mkuu wa klabu ya soka ya Yanga hivi karibuni .Malalamiko yanaoendelea sasa dhidi yake kuhusu uchaguzi huo.

  Nawajua vizuri sana wana yanga jinsi walivyo mahodari kuzungumza kwani baadhi wamefikia hatua ya kuamini kwamba Ridhwan alipata Maelekezo ya baba Yake (Rais Kikwete) ambaye naye ni Mnazi wa Yanga Kuhakikisha wagombea fulani hawapati nafasi Yanga.

  Leo hii uchaguzi huo unalalamikiwa sana na sana baadhi ya wanachama wanatishia kwenda mahakamani na lawama nyingi zinaelekezwa kwa Ridhwan.

  Yanayozungumzwa na kundi la wanayanga wanaopinga mgombea wao kufanyiwa fitna hadi kujitoa ,wanasema eti serikali ilihingilia uchaghuzi na wakati mwingine wanashindwa kumungunya maneno na kusema Ikulu ilihingilia Kati uchaghuzi wao.

  Hii maan yake ni kwamba wamefika hatua ya kuamini Baba (Kikwete) kamtuma mwana kusimika viongozi anaowapenda wakati yawezekana Ridhwan aliyoyafanya hayana hata chembe ya mkono wa Rais Kikwete
  Tatu nimpongeze kwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kuachia ngazi kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (uvccm) Masauni Yusuph Masauni hatimaye kiyi hicho sasa kinakaliwa na rafiki yake wa karibu aliyeemuunga mkono kwenye harakati za kuwania nafasi ya uenyekiti wa UVCCM Beno malisa ,kabla baba yake kuamuru nafasi hiyo iende Zanzibar.

  Ridhwan ni shaidi katika hilo kwani mengi yaliandikwa kwenye vyombo vya habari juhu ya kuhusika kwake na mpango wa iliyomngoa masauni Madarakani.

  Ridhwani mwenyewe amepata kukaririwa na baadhi na baadhi ya vyombo vya habari akikanusha,lakini wapo wanaoamini hasa wajumbe wa Baraza kuu UVVCCM Kutoka Zanzibar kwama alihusika kuwapoka kiti hicho.kama anabisha ajaribu kwenda Zanzibar.

  Binafsi naomba nikupe ushauri wa bure.Ridhwan hebu angalia mifano ya watoto wa viongozi waliopita.wapo ambao hawakijulikana hata kwa majna yao na hili lilitokana na wao kutokuwa mbele kwenye shughuli za Baba zao walipokuwa Marais.

  Ridhwan leo uko mbele ya kila kitu cha baba yako ,utadhani wewe ni Rais mdogo wa Nchi .wapo watu wanaohoji ukwasi wako wa sasa unaokufanya usione umuhimu wa kazi yako uliosomea ya kuvaa jihoo la uwaki naa kubishana na majaji mahakamani kutetea watuhumiwa.

  Nakushauri ,achana na mambo hayo ,Vinginevyo utamponza Baba yako na kama unabisha subiri muda si Mrefu utajua ninacholisema
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  Kwani ametenda wema upi hadi watu wa mseme kwa mema?
  Kila mtu hulipwa kutokana na kazi yake.
  Ukipanda ubaya utavuna ubaya
   
 3. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mbona sifa nyiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiingi wakati bado mapema??????????????? au mnatumana? siwaelewi!!!! hizi sifa za wakati huu .mbona tuna vijana wengi wenye sifa kuliko yeye.au wao hawastahili kusifiwa .huu ushabiki ungehamia kwenye vitu vya msingi .
   
 4. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,056
  Likes Received: 3,980
  Trophy Points: 280
  ukiandika makala ndefu kama hii jaribu kupitia kufanya marekebisho maana umechapia maneno chungu nzima na kupoteza maana ya waraka huu! Hebu fanya hivyo mkuu, heshima mbele
   
 5. Pilato

  Pilato Member

  #5
  Jul 28, 2010
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 60
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  :angry:
  KATIKA HILI NIMEAMUA KUMFUNGA PAKA KENGERE ,LIWALO NA LIWE HATA KAMA NAMGUSA MTOTO MPENDWA WA RAISIO JAKAYA KIKWETE ,RIDWANI KIKWETE

  ''Sina nia ya kumtaka Ridwani hasijihusishe na mambo ya kisiasa wala mengine ya kijamii, lakini kasi ya mtoto huyo wa rais inatisha na ikiendelea hivyo gharama zake mambo anayofanya sasa atabebeshwa kwa rais kikwete tena kwa kuanzia uchaguzi ujao,

  Nimeamua kumwambia ukweli kwa sababu kubwa mbili za msingi ,mosi ni kwamba yeye ni mtoto wa raisi aliye madarakani na kama atashinda tena ataendelea ingawa safari hii si rahisi kushinda kwake kama anavyofikiria .

  Pili ni yanayozungumuzwa na makada wenzake wa ccm kwani naamini hakuna anayeweza kumwambia ukweli mtoto wa rais kutokana na tabia ya unafiki wa baadhi ya watu wa ccm ya kujikomba na kufikia hata hatua ya kulamba viatu vya wakubwa wa aina ya Ridwani ,nampongeza kwa kazi kubwa ya kusaka udhamini wa mzee nnchi nzima ,wapo waliotaka kazi hiyo ndani ya ccm na walikuwa wakinon'gona yeye kupewa mikoba ni kutokana na kutoa mini wana mtandao wake.

  Tatu nimpongeze kwa kufanikisha kimizengwe uchaguzi wa yanga na malalamiko yanayoendelea hivi sasa juu ya uchaguazi huo, na nawajua wanayanga walivyo hodari kwa kuzungumza na hata wengine wamefikia hatua ya kuamini kwamba ni baba yake ndio alimpa maelekezo,kuhakikisha mgombea flani hapiti,leo hii uchaguzi unalalamikiwa sana na baadhi ya wanachama kutishia kwenda mahakamani kupinga mgombea kufanyiwa fitna na Ridwani na HADI KUSEMA serikali kuingilia haki hiyo ya mwanayanga na kushindwa kumun'gunya na kusema ikulu imeingilia kati uchaguazi wao.

  Nne nimpongeze kwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kuachia ngazi kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa uvccm Taifa Masauni Yusuf Masauni na hatmae kiti hicho kukaliwa na rafiki yake Swahiba Beno malisa,
  Ridwani ni shahidi kwa hilo mengi yaliandikwa kwenye vyombo vya habari juu ya kuhusishwa kwake ,lakini wapo wanaoamini hasa wajumbe wa wa Baraza kuu la Uvccm Kutoka Zanzibar kwamba alihusika kuwapora kiti hicho KAMA ANABISHA AJARIBU KWENDA ZANZIBAR,

  Binafsi naomba nikupe ushauri wa bure RIDWANI ,hebu angalia mifano ya watoto wa viongozi waliopita .wapo ambao hawakujulikana hata kwa majina yao na hii ilitokana na wao kutokuwa mbele kwenye shughuli za baba zao walipokuwa marais .

  RIDWANI leo uko mbele ya kila kitu cha baba yako , NAUTADHANI WEWE NI RAIS MDOGO WA NCHI , wapo watu waliohoji ukwasi wako wa sasa na unaokufanya usione umuhimu wa kazi yako uliyosomea ya KUVAA JOHO LA UWAKILI NA KUBISHANA NA MAJAJI MAHAKAMANI KUTETEA WATUHUMIWA

  Nakushauri achana na mambo hayo ,vinginevyo UTAMPONZA BABA YAKO NA KAMA UNABISHA "SUBIRI MUDA SI MREFU UTAJUA NINACHOKISEMA "

  Tanzania Daima,sauti ya watu JULAY,28,2010.

  '' duh ila kwa ubishi wa huyu mtoto naamini hata jali ushauri huu..!!, ila siamini kama ubishi wake utatokana na asili yake ya watu wa jamii yake wafupi ni labda kampani yake ndogo yenye matarajio makubwa huko mbeleni''
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  Unataka wamsemeje kama yeyebinafsi hamna jema alilolitenda?
   
 7. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  kwakweli mkuu umenena jambo la maana sana leo...ujue huyu dogo mie huwa simwelewi kabsaaaa...huu sio utawala wa kifalme kijana wangu ridhwani...baba akitoka inakuja regime nyingine ambayo hata kusikia chembechembe za utawala wa babayako haitotaka...ndiooo..si unaona yaliyojiri baba yako alipochukua ikulu...aliwatupilia mbali regime ya mkapa na watu wake woote hataki hata kuwasikia...sasa sijui wewe mwenzetu nchi akichukua slaa utatataka regime hiyo ikuweke wapi...

  pia naskia wewe ni lawyer..sasa unapata wapi muda wa kuzagaa mitaani wakati kuna kesi nyin gi zinakusubiria uende nazo mahakamani...au ulichukua masters ya siasa na kampeni za chinichini...inasemekana ndicho unachokifanya kiasi kwamba wanayanga wengi wanakulaani sanaaa...Ujue dogo vijana wa nyerere wangefanya unavyofanya wewe sahivi wao ndio wangekuwa maraisi wa nchi hii na tungeshakuwa tumeingia msituni kumwaga damu maana WATANZANIA TUSINGEKUBALI NA HATUKOTAYARI KUSIKIA UTAWALA WA KIFALME/KISULTANI

  dogo skiza..acha KUMTEGEMEA MSHUA KIASI HICHO JUST STAND ON YA OWN FEET..baba anakupa puppy luv..inakwisha hiyo utakuwa na wakati mgumu sana..just make up ur ajira ili uweze kuishi kwa raha bila presha za siasa hapo baadae....NI MAONI TUU DOGO NOTHING PERSONAL
   
 8. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2010
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Huyu jamaa mbona haeleweki, kwani huyo Ridhiwani amefanya nini cha ajabu, mbona tulikuwa nae mlimani alikuwa mtu wa kawaida tu na hayo majisifa aliyompa mbona hatuoni yanatoka wapi, au ndo mambo yale ya Watanzania kupenda kujikomba angalau uambulie makombo, acha bwana, Tanzania hii kuna watu potential zaidi ya Ridhiwani wako, kuna watu wenye IQ kubwa zaidi ya Ridhiwani wako, please shut the nonsense, hata mtu mwenye kumfahamu Ridhiwani atakushangaa sana, where did you get this?
   
 9. MLATIE

  MLATIE Senior Member

  #9
  Jul 28, 2010
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 174
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hii issue ya siasa za kifalme ss imeingia Tanzania mfano Karume,ridhiwani,hussen mwinyi nk yaani kwa vile baba alikua mkubwa basi lazima mtu mmoja toka katika familia na yy afuate hio sio demokrasia nchi hii sio ya ukoo hii ni ya watanzania wote tunataka kiongozi atoke kwa watu sio familia zilezile.huyo mtu anyempa sifa ridhiwani atakua anajigonga tu ila na yy apwew angalau afisa mtendaji
   
 10. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #10
  Jul 28, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mmh una yako wewe sasa kisichoeleweka ninini?
  au ndo wale wale na wewe?
  imeeleweka kaka kwa yeyote mwenye macho na anayeenda kwa semantik na si grammar km mwalimu wa mwandiko wa darasa la 3 inakuwa poa tu ukisoma inaeleweka!!!
  r u leftist ??? i dnt wan knw t.
   
 11. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #11
  Jul 28, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mbona mimi sjaona alipomsifia???naona katoa mabichi km yalivyo!!
  pole masauni mwaya pipo knws wats goin on
  waachie ao watoto wa kisultani but ipo siku wataumbuka!!
   
 12. A

  August_Shao Senior Member

  #12
  Jul 28, 2010
  Joined: Nov 23, 2007
  Messages: 158
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  tungoje naye apate ajali ya siasa
   
 13. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  hivi Nyerere angeendesha hii nchi kwa misingi hii ni nani ambaye sio kutoka ukoo wa Nyerere au kutoka Musoma angetawala hii nchi, hivi kikwete anashindwaje kulijua hilo, hata kama Ridhwan alikuwa yuko safi chuoni, lakini sasa sio tena sasa hii nchi anaikamata kama yeye ndio raisi, anakuja juu mno
   
 14. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Hilo nalo neno, Maana tunakoelekea ni kama vile Tanzania haina watu wenye uwezo wa Kuongoza, au ni nchi ya Kifalme. na pia tupo kama vile hatuoni. Watu wameanza kupeana tu.

  huyu Ridhiwani kasikia baba yake amepata ukuu, basi kajitokeza naye anaanza kupigiwa chapuo. na tusipokuwa makini lazima apande naye awe kiongozi, tena mkubwa katika nchi.

  Siyo fair kabisa kupendeleana wazi wazi, inamaana hawa watu wamekosa kwa kwenda wanaamua kuwatengenezea nafasi nyeti kama hizi!
   
 15. M

  Msharika JF-Expert Member

  #15
  Jul 28, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  HAHAHAAAAAAAAA, Jamani kama huna la kujadili chukua vuvuzela puliza ukichoka pumzika kausingizi lainiiiiiiiiiiiiiiiiiii katakuja ulale. Huyo mtoto hana hata quality ya udiwani. Hakae pembeni. Ni haibu mvulana umekomaa unajisongasonga na wazazi , utajitegemea lini? LOL
   
 16. babylove

  babylove Member

  #16
  Jul 28, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  chifupi!chinene!chinapenda chupi
   
 17. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #17
  Jul 28, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Huyu bwana mdogo anajitahidi kutumia nafasi ya baba yake maana anajua kuwa hakuna nafasi nyingine kama hii.
  ila akumbuke kuwa yana mwisho na mwisho wa mambo kama haya ni aibu.
  Ushauri kwake ni aache kabisa kijiinua kwa jina la babaye. Bora linde tu heshima. Mbona hayo yatakuja tu.
  kama ipo, ipo tu - akilaziomisha na wakati uwezo wake mdogo itakuja kula kwaeke mara tu watanzania watakapoamka kutoka katika usingizi walionao.
   
 18. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #18
  Jul 28, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Du! Aliyekosea labda ni mleta hoja. Anayesemwa wala hana habari anasemwa vipi.
   
 19. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #19
  Jul 28, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ingekuwa mie ndie Ridhwani ningefuatilia mambo yangu ya uwakili nikahakikisha nafungua nami ofisi yangu ya mawakili nijitahidi nichukue kesi za maana ziweze kunilipa na kunipandisha chati kuwa ni wakili bora mwenye kujua kazi yake. Hii ya kwenda kuwa KKKB ( Kula Kulala Kwa Baba) ningeachana nayo kwani nimeshakuwa mtu mzima nafamilia yangu inayo nitegemea.
  Huu ni Ushauri wangu binafsi kwa Ridhwani
   
 20. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #20
  Jul 28, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  .
  Ridhiwan ni nini? Ni kamati gani katika chama kipi cha Siasa? Maana naona mlolongo mwingi kumhusu mtu asie katika medani ya siasa za Tanzania. Naona ingekuwa vyema kuwajadili wale wanaomtuma kuliko kuwekea akili huyo anaetumwa.
   
Loading...