Ridhiwan Kikwete aendelea kukagua miradi ya maendeleo Chalinze

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
RIDHIWAN KIKWETE AENDELEA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO CHALINZE.

Chalinze, Pwani.

Mbunge wa Chalinze ndugu Ridhiwanii Kikwete ameendelea na ziara yake ya Kijiji Kwa Kijiji katika jimbo la Chalinze Kwa lengo la kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye shughuli za maendeleo pamoja na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali, wananchi na ofisi ya Mbunge katika ngazi za vijiji.

Ndugu Ridhiwani amebainisha ya kuwa “Maendeleo ya maeneo yetu yanategemea utayari na utashi wetu, sisi ndio wanufaika wa kwanza wa kila jambo na kila Mradi hivyo ushiriki wetu Kwenye miradi hii utaongeza chachu na kutoa hamasa Kwa serikali kuona kuwa sisi wananchi tuko tayari kushirikiana Kwa pamoja Kwa ajili ya Maendeleo”

“Maendeleo hayana itikadi, hayabagui ila matunda yake ni manufaa ya jamii yetu sote na vizazi vyetu hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha tunajenga Chalinze ambayo tunatamani kuiona Miaka michache ijayo na jambo hili linawezekana tukiamua kutokea kwenye kaya zetu, vijiji vyetu, kata zetu hadi ngazi ya jimbo”....... Ridhiwani Kikwete

Ziara ya ndugu Ridhiwani katika Kijiji cha Mnindi kimekuwa ni chachu ya ujenzi wa Chalinze yenye Umoja Kwa kuunganisha wananchi na kuwajengea morali ya kushiriki Kwenye shughuli za maendeleo.

#SamiaNaTanzania
#RizNaChalinze
#KaziIendelee2030

IMG-20210815-WA0036.jpg

IMG-20210815-WA0037.jpg

IMG-20210815-WA0038.jpg
 
Anapiga chuma. Wambie wakajifunze kwa mwenzao wa Uganda. Ni comnando na Majeshi yako chini yake, sijui nchi.
 
Anapiga chuma. Wambie wakajifunze kwa mwenzao wa Uganda. Ni comnando na Majeshi yako chini yake, sijui nchi.
Vongozi wengi hata watoto wa Malkia cha kwanza hupelekwa jeshini wanapowaandaa kuwa viongozi sababu kule hujifunza ukomavu na kukubalika na jeshi

Museveni wake komandoo na mwanajeshi aliyeiva ,Kabila mkubwa pia mwanawqe alimpeleka jeshini akawa kiongozi jeshini kabla uraisi.Kagame watoto wake hadi wa kike ni wanajeshi makomandoo walioiva waliopitia mafunzo ya kijeshi vyuo vigumu vya uhakika duniani.Mtoto wake wa kiume kiongozi mkubwa jeshini

Hawa wa kwetu watoto wa viongozi hata JKT AU MGAMBO huwa wanatoroka hawaendi wamelegea sana,

Ukiona anajitia fit kukimbia kimbia ni vimichakamchaka tu vya mazoezi ya gym!!!! lakini hamna kitu ukirusha tu kofi hewa ya kofi tu ikimpitia bila kofi lenyewe kumfikia anaanguka chini
 
Apewe wizara ya ulinzi arub shoulders na Makamanda na wapiganaji kuwapiga changa la macho.
 
Back
Top Bottom