Hoja ya Richmond imeendelea kuzua mjadala katika Serikali na Bunge. Hoja ya kutaka mjadala huo kufunguliwa imetawala katika vikao vya kamati ya wabunge wa chama hicho pamoja na kamati ya uongozi wa bunge. Kila upande kati ya makundi mawili lile la makamanda wa ufisadi na la watuhumiwa wa ufisadi inazungumzia hoja hiyo huku Spika wa Bunge akikwepa katika mkutano wake na waandishi wa habari jana kuzungumzia kwa undani suala hilo. Hoja hii pamoja na suala la nyongeza ya posho, kurejeshwa kwa sheria ya mabadiliko ya katiba na utekelezaji wa maazimio ya bunge juu ya wizara ya nishati na madini zinatarajiwa kuleta mijadala mikali katika mkutano wa bunge unaoendelea.
PM
Mbona kule Dodoma kwenye kikao cha NEC Lowassa aliumwaga ukweli na JK akawa anatikisa kichwa ikiwa ni ishara ya kukubali? Ok, je ni kwanini JK alishindwa/kashindwa kumjibu Captain Lowassa?lowassa anatapa tapa tu,hii kitu haitamsaidia kama anavyodhani..sana sana atazidi kujivua nguo na makyembe anaonekana kuwa fiti sasa maana lengo lilikua asiwepo hoja itakaporudi bungeni!
Mkuu Aweda, kuna kitu naona kama sio sawa pengine wadau wanaweza kufafanua. Kama utakumbuka watuhumiwa wa Richmond wamekuwa wanataka sana swala Richmond lirudi tena bungeni lakini juhudi zao hakifuka mahali. Sasa Mnyika ana ajua chochote kuhusu jitihada hizo? Something is not right. Umakini unahitajika maana upo uwezekano watu wakajipenyeza kwenye hii hoja binafsi.Excellent move Mnyika.
Acha irudi maana inaweza isaidie kufungua yale ambayo Mwakyembe alishindwa kuyatoa hadharani na yanahatarisha uhai wake sasa.
mm nalifikiri ndani ya Ukumbi wa Bunge kumbe kwenye twitter, facebook yake mwaga zaidi ameweka wapi?
Suala la Richmond kurudi bungeni, naliona kwa mtazamo tofauti kidogo.
Kwanza imelenga kumsafisha EL, Kwasababu zipo tetesi kuwa toka awali mama Makinda aliposhawishiwa na kundi la EL kugombea uspika, nia ilikuwa ni kumpata mtu atakayeirudisha Richmond bungeni ili sitta , mwakiyembe na kundi lao waonekane walichemsha ktk kulitia taifa hasara, kuleta migogoro isiyoisha ndani ya chama na serikali n.k.
Pili nachelea kusema kuwa Mnyika katumwa!!, ama kwakujua au kwakutokujua. nitaeleza.
Ikiwa katumwa akiwa anajua. Hii huenda ni dhamira ya chama chake (chadema). Kuwa, kimemtuma apeleke hoja hiyo ya Richmond bungeni ili EL asafishwe ili chadema ijihakikishie ushindi 2015 endapo ccm itampitisha El, kwakuwa wamekuwa wakiamini kuwa nguvu ya El kwa Umama ni ndogo ukilinganisha na nguvu ya cdm.
Pia upo uwezekano wa mnyika kutumwa bila ya yeye (mnyika) kujijua kwamba katumwa. El ni mtu anayefanya siasa za kiwango cha juu sana, ana mtandao mpana sana vijana kwa wazee, ndani ya chama chake na ndani ya vyama vya ushindani (upinzani), hivyo ni rahisi hoja hii ya Richmond kufikishwa kwa mnyika kupitia kwa marafiki zake (mnyika) au hata yeye mwenyewe kwa namna moja au nyingine bila Mnyika kulitambua hilo.
Naamini hoja hii ya Richmond kurudishwa bungeni, haikosi mkono wa mafisadi. Naamini hoja hii ilifikishwa kwa Mnyika bila ya yeye kujua, akidhani hoja imeletwa na wazalendo wenzake. Lakini yote kheri coz it is just a political strategy for both political party!!.