Richmond kutikisa Bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Richmond kutikisa Bunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngongo, Jan 28, 2012.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  • NI HOJA BINAFSI ILIYOWASILISHWA NA JOHN MNYIKA WA UBUNGO
  Imeandikwa na Shakila Nyerere

  SAKATA la Richmond linatarajiwa kurudi upya bungeni baada ya Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika kuwasilisha hoja binafsi kuhusu utekelezaji wa Maazimio 13 yaliyobaki ya Bunge, juu ya mkataba baina ya Tanesco na kampuni hiyo ya kufua umeme wa dharura.Mnyika alisema jana katika taarifa yake kuwa lengo la hoja yake hiyo ni kutaka uamuzi wa Bunge la Tisa Mkutano wa 18 Februari, 2010 kufunga mjadala huo ubadilishwe ili hoja hiyo irudi upya bungeni.

  "Niliwasilisha hoja hiyo Ofisi za Bunge Januari 25, mwaka huu kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2007, Kanuni 54, (4) na 55 (1)," alisema Mnyika katika taarifa yake hiyo na kuongeza:

  "Ikipokewa na kujadiliwa, hoja hiyo itaongeza msukumo wa utekelezaji wa maazimio ya Bunge na hivyo kuchangia katika mapitio ya mikataba yenye kuongeza bei ya umeme na kuweka mfumo wa kulihusisha Bunge katika maandalizi ya mikataba yenye maslahi kwa taifa."

  Februari 2010, Bunge lilifunga mjadala huo baada ya Serikali kutoa taarifa ya tatu ya utekelezaji wa mapendekezo yake. Taarifa hiyo ilitanguliwa na nyingine mbili zilizowasilishwa bungeni na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Agosti 28, 2008 na Februari 11, 2009.

  Moja ya taarifa hizo ilikabidhiwa na kujadiliwa na Kamati, ambazo zililitaarifu Bunge kuwa utekelezaji wa Maazimio 10 kati ya 23 yaliyotolewa na Bunge, umefanyika hadi Februari 2009 na Maazimio 13 bado yalikuwahayajakamilika.
  Baadhi ya maazimio ambayo utekelezaji wake haujakamilika ni Azimio Na. 3, ambalo liliagiza Mkataba kati ya Tanesco na Richmond Development Company LLC (uliorithiwa na Dowans Holdings S.A.) na mingine kati ya Tanesco na IPTL, Songas, Aggreko na Alstom Power Rentals, ipitiwe upya mapema kama mikataba ya madini ilivyopitiwa upya na Serikali.

  "Iwapo Azimio hili lingetekelezwa kwa ukamilifu wake, gharama za uzalishaji Tanesco zingepungua na hivyo bei ya umeme isingepandishwa kwa kiwango kikubwa kama ilivyo sasa," alisema Mnyika.

  Maazimio mengine ambayo utekelezaji wake haujakamilika ni pamoja na lile lililotaka Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah awajibishwe kutokana na taasisi yake kushindwa kuona upungufu katika mchakato ulioipatia zabuni Richmond.

  Azimio jingine ni lile lililotaka kuwajibishwa kwa watumishi wa umma akiwemo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi, ambaye hata hivyo, hakuchukuliwa hatua yoyote hadi alipostaafu na kutowajibishwa kwa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika.

  Katika sakata hilo, Serikali pia haijatekeleza azimio la kuwajibishwa kwa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi badala yake ilieleza kuwa uchunguzi ulikuwa unaendelea dhidi yake.

  "Hoja binafsi itakapojadiliwa bungeni itawezesha Bunge na wananchi kwa ujumla kupata taarifa ya utekelezaji wa maazimio hayo 13," alisema Mnyika katika taarifa hiyo.

  Hii si mara ya kwanza kwa Mnyika kuwasilisha hoja hiyo bungeni. Aprili 13, 2011 aliiwasilisha... "Hata hivyo, niliijibu Ofisi ya Bunge kupatiwa taarifa ya utekelezaji uliofanywa na Serikali baada ya Februari, 2010 bila kupatiwa majibu hivyo nimeiwasilisha tena ili hoja husika ijadiliwe."

  "Kwa muktadha huo, hoja binafsi husika itawezesha mjadala kuhusu uamuzi husika kufunguliwa na kutoa fursa kwa jambo hilo kufikiriwa tena ili kuwezesha hatua kamili kuchukuliwa juu ya maazimio 23 ya Bunge yaliyopitishwa Februari 15, 2008 katika Mkutano wa 10 wa Bunge la Tisa."

  Mnyika alihoji Serikali kutochukua hatua zozote hadi sasa wakati ililieleza Bunge kwamba vyombo vya dola vimekamilisha uchunguzi wake wa ndani ya nchi kuhusu suala hilo.

  "Hata hivyo, zoezi lililoendelea toka Februari, 2010 ni kufanya uchunguzi wa nje ya nchi kwa kushirikiana na vyombo vya dola vya kimataifa ambapo, mmoja umemalizika bila hatua zozote kuchukuliwa kwa wahusika katika kashfa ambayo maazimio ya Bunge yalipitishwa zaidi ya miaka mitatu iliyopita hali ambayo inaweza kusababisha hata mashahidi na ushahidi kupotea," alisema.

  Mnyika pia alihoji sababu za kutoanza kutekelezwa ipasavyo kwa azimio la 13, lililotaka Serikali izihusishe Kamati za Kudumu za Bunge kwenye hatua za awali za maandalizi ya mikataba mikubwa ya muda mrefu ya kibiashara ili kuondokana na utaratibu uliopitwa na wakati kwamba mikataba ya kibiashara ni siri hata kwa walipa kodi wenyewe.

  "Azimio hili halijaanza kutekelezwa kwa ukamilifu wake, matokeo yake ni kwamba Serikali katika kipindi cha kati ya mwaka 2008 mpaka 2011 imeendelea kuwa siri katika hatua za awali za maandalizi na pia mikataba mingi haijafanyiwa mapitio," alisema.

  Mnyika alisema azimio hilo lingetekelezwa kwa ukamilifu lingesaidia kuwa na mfumo mzuri zaidi wa maandalizi ya mikataba wakati huu na Serikali inaingia mikataba mingi ya gharama kubwa ya utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme hali ambayo imeongeza mzigo mwingine wa gharama za maisha kwa wananchi.

  Azimio Na.10 lilihusu Gavana wa Benki Kuu (BoT), pamoja na Bodi ya Wakurugenzi, wachunguze kwa makini uhalali wa malipo ya ziada ya Dola za Marekani 4,865,000 yaliyofanywa kwa Dowans Holdings S.A iliyorithi majukumu ya Richmond Development Company LLC na kuwachukulia hatua waliohusika na uzembe huo.

  "Hoja Binafsi itawezesha mjadala kufunguliwa na mambo zaidi yaliyojiri kuhusu suala hili na mengine kuweza kujulikana na hatua kuchukuliwa kwa wote waliozembea ili kuimarisha misingi ya uwajibikaji katika taifa," alisema na kueleza:
  "Masuala zaidi kuhusu maazimio mengine nitayaweka katika maelezo ya hoja ili niwasilishe katika Mkutano wa Sita wa Bunge la 10 uliopangwa kuanza Januari 31, mwaka huu," alisema.

  Alipoulizwa kuhusu hoja hiyo ya Mnyika, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah hakukataa wala kukubali badala yake akasema, "Unataka mimi nisemeje? Yeye ni leader (kiongozi) amechaguliwa na watu wengi, kwa nini tusimwamini? Mimi nafikiri kama kasema mwenyewe tumwamini tu bila hata mimi kuthibitisha."

  "Unajua ofisi yangu ina mambo mengi na kiutaratibu siwezi kulisemea kila jambo kabla ya wakati wake. Mimi napendekeza basi hilo nalo tusubiri wakati wake, ukifika, tutasema."


  Source: Mwananchi

  My take:

  John Mnyika ananivutia sana ni mwanasiasa kijana ambae ndani ya bunge na nje ya bunge kaonyesha ukomavu na uelewa mkubwa wa mambo mengi.Pamoja na mambo anayohoji John Mnyika nadhani sasa ni wakati muafaka wa Mheshimiwa Edward Ngoya Lowassa kueleza kile tusichojua waTanzania nategemea kama bado ana ndoto za uRais hii ni nafasi pekee amabayo hataiapta tena.
   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Kuna baadhi ya mambo ambayo wabunge wakijipanga vizuri hakika serekali lazima iporomoke tena.

  [1] Ni kwanini Hosea bado ni mkurugenzi wa TAKUKURU ?.

  [2] Uchunguzi wa Karamagi umefikia wapi,Je ni hatua gani zimechukuli dhidi yake mpaka sasa ?.

  [3] Je uhalali wa malipo ya ziada RICHMOND na hatua zilizochukuliwa ?.
   
 3. M

  Makupa JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hivi nchi matatizo tuliyonayo ni Richmond tu au ni watu wanataka kujitafutia tu umaarufu wa kisiasa
   
 4. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Aeleze nini zaidi ya kile alichokieleza mbele ya mwenyekiti na wajumbe wa NEC wa chama chao!!! Au aeleze bungeni ili kuharakisha uchaguzi mkuu kabla ya 2015 na Jaji Mkuu ashikilie nchi katika kipindi cha mpito!!!
   
 5. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Yataje basi unayoyajua wewe kwa akili yako 'kubwa' unadhani yanahitaji utatuzi na kuongelewa hapa
   
 6. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nyinyi ndio mnalirudisha taifa nyuma, umesomeshwa ila huna tofauti na mtoto wa darasa la saba aliyefaulu while ajui kusoma.
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Makupa tuna mashida sana Tanzania .Sasa wewe una anza nonsens zako kwa kusema umaarufu ? Hili pia ni tatizo lishughulikiwe tukielekea kwenye mengine huko mbele .Unataka waache wakiwa na mawazo kama yako ? Ama kweli una uelewa kama wa JK
   
 8. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu Makupa kama maazimio ya bunge yangetekelezwa ipasavyo hakika matatizo mengi ya TANESCO yangekuwa historia.

   
 9. usininukuu

  usininukuu JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2012
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inanihuzunisha sana kuwa na serikali inayoshindwa kulimaliza suala moja miaka 6 kisa ushikaji;
   
 10. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  hongera sana Mnyika maana hata mimi niliwahi kule thread hapa nikihoji serikali kutekeleza maazimio ya bunge ni hiari au wanawajibika kufanya hivo huenda swali langu likapatiwa jibu!!!
   
 11. yegella

  yegella JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 3,116
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  matatizo mengine ni mdudu CCM....
   
 12. maulaga

  maulaga JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2012
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 472
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwani wewe unamaslahi gani na Richmond?
   
 13. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #13
  Jan 28, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,540
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 180
  Hakyanani huyu kijana nimempenda . Nataka ukweli wote ufunuliwe.
   
 14. HT

  HT JF-Expert Member

  #14
  Jan 28, 2012
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  binti kaa chini utulie. Uwe msikivu ati, kilinge cha watu wazima watoto wapaswa kuwa na nidhamu!
  Huwezi elewa hii kitu ila ukikua utaelewa tu binti yangu!
   
 15. c

  chama JF-Expert Member

  #15
  Jan 28, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Majibu yake ni rahisi sana! Viongozi waandamizi wa serikali ni wahusika wakubwa akiwamo Hosea mwenyewe, suala la nani amchunguze nani halipo.

  Chama
  Gongo la Mboto DSM
   
 16. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #16
  Jan 28, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  ngoja tuone
   
 17. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #17
  Jan 28, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,694
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  No stone will be left unturned.
   
 18. KIGENE

  KIGENE JF-Expert Member

  #18
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,066
  Likes Received: 203
  Trophy Points: 160
  Ukiona mtu kama huyu kwenye karne hii ya dot com hawezi kuelewa hoja iliyoelezwa kinagaubaga bado anahoji utumbo unaridhika kwamba jerumani alikuwa na uhalali yakuwatia mijeledi watu wa aina yako miaka hiyo

  Si tu wewe na wote wenye mawazo kama wewe ni tatizo bali ni janga la kitaifa.
   
 19. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #19
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Siku zote mie huwa nasema Mnyika ana akili km za embe dodo. Hili suala liliisha fungwa na Bunge sasa kwa akili za embe dodo anajitafutia umaarufu wakulazimisha. Jimboni ubungo hajafanya lolote mpaka sasa zaidi ya maandamano. Na anaevutiwa na huyu kwa kweli nae ana akili za embe dodo.

  Na hii hoja yake tupo hapa haiwezi kupita hata kwa bunduki

   
 20. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #20
  Jan 30, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu GeniusBrain,

  Ni kweli hili swala lilishafungwa lakini maazimio ya bunge hayajatekelezwa !.Mheshimiwa John Mnyika ana haki ya kuhoji sababu za kutotekelezwa maazimio ya bunge.   
Loading...