Review: Demographics, Population and Youth Leadership

Zaidi ya hayo uliosema hapo nadhani this will help consolidate that patriotic feeling ya wakati ule. Of course I believe the content of the course will also be adapted so as to nurture this.

there you are madame!
Let me tell you, umefika wakati tuletewe tena sera ya elimu tuijadili kisha serikali isikilize mawazo yetu. Infact we have a lot to tell and i can tell you Roulette am among the most disturbing teachers ambaye huwa siishiwi kuishauri serikali kwa maandish with valid urgument but yaani utaishia kupewa kikombe cha chai kwenye maofisi yao ukiondoka ndo basi inawekwa kwenye shelfu till death.
 
Last edited by a moderator:
But how do we prepare the youth to take the future leadership roles? By letting them rooming in the streets?
 
But how do we prepare the youth to take the future leadership roles? By letting them rooming in the streets?

That's the next question. We have discussed population growth and education (actually population growth in connection to education) which was not covered in the presentation. But the other question is how do we prepare them for Leadership?
Si umeona mwenyewe EMT anasema watu hawawahamasishi watoto ku-participate in the decision making process hata nyumbani. mfano mngine ni watu wanao pinga miaka ya uraisi ishishuke chini ya 40 wakati we are a country of under 40s. Wakisema under 40 sio marute to run a country, then they should also propose how take them to maturity because we are only growing younger, we need to adjust.
Kwanza cheki hii slide (from the presentation)
role models.png
 
View attachment 98402

Roulette nadhani watoto na vijana wana interests zao which should be recognised and respected. They have people and things which they perceive to be relevant to them. Nilipokuwa mtoto nilikuwa hivyo hivyo. Lakini umri unavyokwenda interests and perceptions zinabadilika. Inawezekana kabisa mtoto/kijana akajifunza kutoka kwa Wema kuliko kwa Naibu Spika wa bunge, maana hata mimi mzee mzima sina cha kujifunza kutoka kwa Naibu Spika kama kiongozi. Lakini kuna baadhi ya mambo ningependa kuyaongea hasa katika hoja ya kuwaanda watoto na vijana kuwa viongozi wa kesho.

Tunakoelekea kutahitaji more creativity, kuwa mjuzi kwenye teknologia, na uwezo wa kuunganisha watu na ideas. Tena kulingana na jinsi uchumi wa duania unavyoenda, watoto wa nchi kama zetu wanatakiwa kuyajua haya mambo mapema na kwa haraka zaidi. Kwa hiyo, nadhani watoto na vijana wasiandaliwe tuu kwa ajili ya leadership roles, bali kwa kila kitu ili wawe na competencies za kukabiliana na dunia inayokuja.

Kwanza, watoto waandaliwe ili wawe na tabia nzuri kama binadamu regardless of whether or not they want to be leaders (though naamini kila mtu ni leader). Hilo lenyewe ni muhimu sana. Kwa dunia ijayo itamchukua mtu miaka mingi sana kujenga reputuation, lakini hiyo reputation inaweza kuangamizwa na social media kwa siku moja tuu.

Story kama hii inasema mengi: BBC News - Paris Brown: Kent youth PCC resigns after Twitter row. Alichanguliwa na wapiga kura kama the youngest police commissioner in the United Kingdom at the age of 17. Baada ya hapo watu wakaja kuibua tweets ambazo ali-tweet wakati akiwa na umri wa miaka 14 na 16 na kumlazimisha kujiuzulu. Social media is a powerful tool for the youth, but it can also be powerless.

Siku hizi nasikia pia waajiri wengi huwa wanapitia pages za Facebook na Twitter kabla ya kuwaajiri watu. Many employers now want to know the character of potential employees. Probably kuna wengine would specifically ask for them. Kwa hiyo, watoto na vijana waelimishwe kuwa makini with what they post on social media, they may come to hunt them in future siyo kikazi bali kwenye nyanja nyingine pia. Unamkumbuka yaliyompata yule shahidi kwenye ile kesi ya Charles Taylor? Inawezekana bado Tanzania, lakini tunaelekea huko.

Pili, concept nzima ya jamii inabadilika. Siku hizi kuna online community. Watu hamjakutana lakini mko so close on the internet. Kama alivyosema mmoja "Facebook is for the people you know. Twitter [and JamiiForums] is for the people you wish you knew and Myspace is for the people you wish you NEVER met."

Kwa hiyo, watoto na vijana waelimishwe kuwa responsible katika kujenga online communities. Kwa mfano, they should not add someone as a friend simply because that person sent them a friend request. Waangalie kama kuna connection yoyote in terms of interests and what can be learned from each other. Quality rather than quantity ya friends and who you follow is much better.

In addition, viongozi wengi wa sasa nao wanaongezeka kwenye social media. So, badala ya watoto na vijana kuishia kuwambia tuu viongozi kwenye social media "Go go kiongozi wangu", "nakuaminia Mkuu wangu", "You're my role model", "You're always right, Mkuu wangu", "I trust you, Boss wangu", n.k., waelimishwe kuwa na tabia ya kuchangia as thought or future leaders kwenye mijadala inayoendelea social media. Wawe na tabia ya kutaka kuhoji kinachoandikwa na viongozi kwa kufuata hoja zao badala ya viongozi wenyewe.

Viongozi nao wawe na tabia ya kuwa-engage vijana kwenye social media. Nimeshaandika sana hapa juu ya tabia ya baadhi ya viongozi kutundika status au tweet na kusepa huku wakisubiri watu wa-like au wa-tweet status zao au kumwagiwa masifa. Hii inaweza kuwadumaza vijana, kwa sababu watadhani social media works just like conventional media.

Hapa ndipo social media inapokuwa powerless kwa watoto na vijana maana wanapowauliza hawa viongizi maswali, mengi hayajibiwi. Kuwa interactive means to engage people, testing their understanding, listen to them, etc, hata kama hukubaliani nao. Nilishasikia kuwa kuna watoto na vijana ambao hawasikilizwi majumbani mwao, kwa hiyo wanaona social media ni tool ya kusikilizwa. Kama na huko hawasikilizwi na wanaowaamini kuwa ni viongozi wao, then we are not doing any better for them.

Tatu, dunia inaangamizwa kwa njia mbalimbali kama uharibifu wa mazingira. Watoto na vijana waelimishwe maana ya "sustainability". Tembo wetu wanaangamia. Waelimishwe athari na impact yake kwenye maisha yao ya baadae.

Nne, siku hizi kuna information nyingi sana. Pia it is becoming easier and easier to access the information. Watoto na vijana waelimishe kuwa not all information out there is correct. Vijana wafundishwe kuwa pro-active katika kuunganisha data na kufikia conclusions za muafaka. Huko tuendako hakutakuwa tena maswali ya kujaza sehemu zilizo wazi kama vile Rais ya Tanzania ni Jakaya Kikwe__ (a) we, (b) ta (c) te. au yale maswali ya false and true.

Hakutakuwa tena na kukremisha mambo. Kwa hiyo, watoto na vijana waelimishwe kuwa na fikra tunduizi. Kwenye homework zao na hata kwenye mazungumzo ya kawaida tuu, wazazi wawe na tabia ya kuwauliza watoto maswali siyo ya kufikiri tuu bali ya kufikiri critically na ku-reason.

Kama mtoto au kijana anapenda kufuata sana habari za Wema au Diamond badala ya news za Dkt Slaa au Rais Kikwete sidhani kama kuna haja ya kumkataza kufanya hivyo. Best way ni kumshauri au kumfundisha jinsi ya kufikri critically. Inawezekana kuna mambo mazuri wanayofanya akina Wema na Diamond (of course yapo) and these kids will want to take the good ones (na kuacha mabaya yao) and build on them na kuwa artists wazuri zaidi. We need artists as well na siyo politicians tuu!

Watoto na vijana wafundishwe jinsi ya kutumia "common sense" kutatua matatizo yao madogo madogo. Siyo kila tatizo anatafuta ushauri kwa mama na baba. Tunaona sana hapa JF jinsi baadhi ya vijana wanavyoanzisha threads ambazo wengi tunaona kama jibu lipo wazi kabisa. Huko baadae waajiri hawatawa-train tena waajiriwa, bali wataajiri tuu watu ambayo tayari wanajua kufikiri na kutumia rasilimali vizuri.

Tano, tunakoelekea teknologia itaongeza ubora wa multi-tasking. Wengi tunajua kuwa multi-tasking inaongeza distraction na usahaulifu. Hapa sina maana ya kuwafundishwa watoto na vijana wa kiume kuongea huku wakipiga mswaki, though I am sure haitakuwa shida kwa Matesha wa Asprin. Lakini watoto na vijana wafundishwe jinsi ya ku-priotise mambo, jinsi ya kuwa focused na kujenga na kudumisha mahusiano na watu wengine.

Jukumu la nani? Kila mtu, kuanzia, mzazi, ndugu, rafiki, viongozi, taasisi na jamii kwa ujumla.
 
EMT and Roulette baadae nitarejea hapa manake leo kuna nondo mmeziongeza na mm sikupita kabisa huku but kabla sijalala i will come back to you. naamini we have a lot to say kwenye hii context.
 
Last edited by a moderator:
EMT, the point is not stopping them from being young, or forcing them to be interested in siasa, but it is important to know where they get their information from and who they listen to. Maybe it can be part of a communication strategy going forward?
Ona "Kigoma All Stars" and their song Nyumbani. It was a good project, and it contributes to pass on a patriotic message. In Kenya I saw a soap about youth in a campus, with a pop DJ from a radio etc, but the thread of the series is HIV awareness. See? it is important to know who our youth are, what they do, where they get info from etc.
Nurturing their leadership will then be adapred to their interest, or their talents.

Rj.jpg
 
Nilikuwa na nabishana na member kwenye thread nyingine juu ya watoto waliodhurika kwenye bomu la Arusha. Although nilikuwa na-ague kuwa children are more vulnerable kwenye mikusanyiko kama ile and, thus, we need to think on whether waendelee kuhufhuria mkutano ya hadhara ya kisiasa, yeye alikuwa alikuwa ana-argue kwa ile hali kila mtu yoyote ni vulnerable.

But I still believe that children are more vulnerable hasa katika dunia ya sasa ambayo kuna a lot of information which they can access so easily. Wanaweza wasidhurike kwa bomu, lakini kwa mafano siasa za majukwaani kama zile za yule mbunge aliyekuwa anamwaga matuzi ya nguoni kwenye mkutano wa hadhara mbele ya watoto.

Kwa hiyo, kuna umuhimu wa kuwa aware where they get the information from and to whom they listen to maana hata baadhi ya peers wao hawaangali kama kuna watoto kabla ya kuzungumza.

Lakinu pamoja na hayo watoto na vijana waliemishwe juu ya ku-assess information and their sources kabla ya ku-rely and act on them. Isjie ikawa kama nilivyosoma somewhere (if it's true) msichana mmoja aliyesoma kwenye net kuwa kuolewa na mzungu na dili sana, nae akaanza kuwasaka wazungu tena wazee.

Inaweza ikawa part ya communication strategy, but bahati mbaya wazazi wengi hawajui modern technology na wengi hawataki kujua. Probably, taasisi nyingine need to step in na kuwaelimisha wote.

Ona "Kigoma All Stars" and their song Nyumbani. It was a good project, and it contributes to pass on a patriotic message. In Kenya I saw a soap about youth in a campus, with a pop DJ from a radio etc, but the thread of the series is HIV awareness. See? it is important to know who our youth are, what they do, where they get info from etc.
Nurturing their leadership will then be adapred to their interest, or their talents.

Pia kuwaelimisha kuwa accountable na kila wanachofanya. Kwa sana neno accountability ni kama halipo kabisa kwenye vichwa vya viongozi wengi na hata wazazi. Watoto na vijana nao wanajihisi hawako accountable kwa wanayofanya. They don't really care because their peer don't care anyway.
 
EMT and roulette asanteni sana kwa maelezo mazuri mliyoyatoa and here comes my urgument na nitajikita zaid kwenye tasnia ya upashanaji habari na kumuandaa kijana kuwa kiongozi.

kwanza nianze na upashanaji habari, nafikiri mtakubaliana na mimi kwamba leo hii habari sio ngumu kupatikana miongoni mwa vijana wetu hata wale ambao ni wadogo kabisa kama Gwin wangu. manake ataone kwenye tv, redio, internet etc. Habari anazozipata kijana huyu ni raw interms of hazijachaguliwa ili kuweza kupata habari sahihi zaid kwa huyu kijana na imfikie kwa wakati gani.

ngoja nitoe mfano mdogo tu wa ishu ya HIV kwa %kubwa sana over speaking ya HIV/AIDS imeongeza shauku ya kutaka kujaribu miongni mwa vijana. sipingani na elimu ya afya ya uzazi kwa kijana la hasha ila napingana na namna elimu hii inavyotolewa interms of kijana yupi hasa alipaswa kupata elimu hii, njia agani ilitumika kumpa taarifa na context iliyobebwa ni ipi ndani ya habari husika. kutokana na sensitivty ya jambo lenyewe hakuna aliyevipa kipaumbele mambo haya na matokeo yake elimu hii ikawa sasa inapatikana kila kona na mwisho kuwafanya wengi wapende kujaribu kamba kunanini huku?? (huu ni mtazamo wangu mm binafsi)

sasa tunaporudi kwenye mada je vijana wanapata habari sahihi juu ya taifa lao?? habari wanazozipata je zinafungua milango gani ya fahamu zao?? yumkini tunafungua milango ya ufisadi, ukatili, overpowering and the like miongoni mwao pasi sisi kujua hayo.

hebu EMT niambie ni gazeti limeandikwa heading kama hivi '' MANYANGUMI FISADI"hiki ndo kichwa cha habari huyu kijana anapoisoma anakutana na hoja kwamba kwenye kufanya ufisadi kuna grading wengine wakiwa mapapa na wengine manyangumi, na anapozidi kuisoma hbari vzr anagundua kwamba wote hawa ni watu ambao walikuwa viongozi ama ni viongozi wafikiri yeye atajenga imagination gani akilini mwake?? ni wazi kwamba atatamani awe kiongozi ili nayeye afisadishe awe ama nyangumi ama papa kama waliomtangulia.

Leo hii kijana anapata habari kwamba kampuni fulan ya kiongozi inakwepa kulipa kodi, anaposubiri kuona matokeo yake anaona kuko kimya, wafikiri kijana huyu anagrasp nini hapo?? na yeye anajua akimbilie uongozi ili awe mkwepa kodi maisha yaende basi.

sijaona mahali popote pale ambapo habari zetu zimejikita katika kuwafungua maskio ya ndani ya vijana na kuwafanya wawe na maarifa ya kutosha juu ya nchi na mwenendo wa uchumi wa nchi hii. habari zozote zikiandikwa kwenye gazeti, makala kwenye tv nk utakuta basi zinatumika lugha ngumu sana ambazo hata kijana huyu kuelewa tu nini kinasemwa ni mtihani atlast anaopt kujinunulia udaku acheke maisha yasonge mbele.

Kuhusu kumwandaa kijana kuwa kiongozi bora hili ni tatizo sana, nilikuwa natafakari hii hoja yenu jana usiku nikaanza kuwaza toka wakati wa vijana wa Tanu. kimsingi viongozi wetu wakuu hapa nchini wawe upinzani wawe wa chama tawala walipitia kwenye kombania.

walipokuwa vijana waliandanliwa kuwa na uchungu na nchi yao, kuwa wawajibikaji, wenye heshima, wasiopenda dhuluma na kwa kufanya hivyo walikuwa na ahadi za Tanu ambazo waliziimba ili tu kujaza mioyo yao na mapenzi mema ya nchi yao na afrika kwa ujumla. sikatai hali hii iliwafanya viongozi wa kipindi ile hadi mpaka miaka ya 84 wakawa ni wawajibikaji na hata kama walikuwa na makosa ni madogo madogo sana.

hawa wa sasa hivi hatuwez kusema kitu manake they are worse, but pia sio worse ukilinganisha na tunaowakuza manake hawa tunaowakuza ndio kuzid, kwasababu hawaoni uwajibikaji kwa waliopo nao pia hawafikirii kuwa wawajibikaji,. kwasabbu hakuna mfano mzuri basi nao hawaoni sabbau ya kuwa viongozi wazuri. Leo hii muulize kijana yyte kwann hasa anataka kuwa kiongozi atakuambia ni ili apate hela basi.

sasa kama system tu imefika mahali imeonyesha wazi kwamba uongozi is all about filling your account na sio uwajibikaji, wa kuwaletea wenzio maendeleo htuwez kufika mahali. Elimu ya uraia sasa hivi ikitolewa iko tofauti kabisa na hali halisi ilivyo. sasa hivi hata chaguzi mashulen tu ili kijana awe HEADBOY/HEADGIRL lazima ahonge wenzie, kwannn manake wanajua watashiriki kwenye baadhi ya kamati na mwisho wa siku watapata pesa so hata kwao ni dili. kw ashule za bweni ndo kabisa anajua nikiwa HG/HB basi nina incentives kibao plus uhakika wa chumba kizuri cha kulala kwa nn mtu huyu asihonge?? then tunawakuza viongozi gani??
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin asante kwa mchango kwa mtazamo wako. Suala la tasnia ya habari na vijana imejadiliwa sana hapa jamvini, lakini zaidi in the context ya magazeti ya Shigongo na Clouds FM. Mojawapo ya thread za mwanzo kabisa ni thread ya Maxence Melo https://www.jamiiforums.com/celebrities-forum/1788-shigongo-chanzo-cha-kuharibika-kwa-vijana.html ambayo threads nyingi zimeumganishwa huko.

Kwanza kabisa nadhani wazazi ndiyo wenye majukumu ya kuhakikisha kuwa watoto wao wanasoma, kusikiliza na kuangalia habari zenye tija kwa watoto watoto wao. Lakini maendeleo ya teknologia yanafanya hili jukumu kuwa gumu zaidi maana kama ulivyosema siku hizi kuna aina mbalimbali za ku-access information. Kwenye post yangu ya nyuma nilishauri wazazi na jamii kuwaelimisha watoto na vijana kwa ujumla jinsi ya kuchuja habari wanazokutana kwa kuwa na fikra tunduizi na ku-reason na siyo kuamini kila wanachokisoma, wanachoangalia au kusikia.

Hata hivyo, tasnia ya habari ina jukumu la kuandika habari zenye tija na kuweka habari za kikubwa kwenye "top shelf". Unfortunately, kama ulivyosema, hata vile vyombo vya habari ambavyo tulidhani vitaandaa habari zenye tija navyo vinaandaa habari ambazo zinamtia uvivu hata mtu mzima. Waandishi wetu wa habari wamekuwa kama public relation officers vile. Wengine wanaripoti tuu habari, hakuna analysis yoyote. Ndiyo maana nilihoji somewhere "Probably hii ndiyo inasabanisha watu kukimbilia kwenye magazeti ya udaku ambayo yako more "investigative" kwenye udaku wao mpaka wanatoa na picha live wakati wa tukio?

Kuna mwandishi mmoja alishawahi kuandika haya kuhusu magazeti ya udaku lakini in the context ya jinsia. Najaribu kuliangalia hili suala kwa upandae mwingine hasa kwa akina dada vijana wengi kupenda sana magazeti ya udaku. Nini maoni yako hasa kutokana na vijana wa jinsia ya kike kutosoma yale magazeti ambayo tunadai siyo ya udaku?

MAGAZETI YA UDAKU NA JINSIA, na Bw. Privatus Karugendo wa Raia Mwema

MAGAZETI ya udaku, ama magazeti pendwa kama wenyewe wanavyotaka yaitwe duniani kote, yana sifa mbalimbali, ikiwamo kutangaza uongo na hata umbeya. Pamoja na ukweli kwamba magazeti ya aina hii nchini yanasomwa na wengi, bado tunayadharau na kufikiri kwamba yanasomwa na watu wasiokuwa makini. Kamusi ya Kiswahili sanifu inaelezea neno udaku kama tabia ya kutafuta na kutaka kujua habari za watu; kilimilimi na umbea. Kuyabatiza magazeti haya kuwa ya udaku ni lengo zima la kutoa ujumbe kwamba haya ni magazeti ya umbea na uzushi.

Je, ni kweli kwamba magazeti haya ni ya umbea na uzushi? Je, watu wengi, na hasa vijana wanapenda kusoma umbea na uzushi? Kila mahali magazeti haya yanauzwa sana. Ukweli ni kwamba magazeti ya udaku yanasomwa sana. Lakini kwa nini watu wapende kusoma umbea na uzushi?

Hoja ninayoijenga katika makala hii si kununuliwa kwa magazeti au kutonunuliwa; bali ni kutaka kumshirikisha msomaji ufunuo nilioupata juu ya magazeti ya udaku. Mimi pia nilikuwa kati ya watu waliokuwa wakiyapiga vita magazeti ya udaku. Nimeandika makala nyingi nikipinga utamaduni wa watu kuacha kusoma vitabu na magazeti makini na kukimbilia magazeti ya udaku. Niliamini kabisa kwamba wale wote wanaoyasoma magazeti ya udaku si watu makini.

Inawezekana kabisa nikawa sijafanikiwa kufahamu vizuri sababu inayowasukuma watu kusoma magazeti ya udaku; na inawezekana pia kwamba wale wanaoyaandika magazeti ya udaku wana malengo na nia tofauti na ile niliyofunuliwa. Hata hivyo, ukweli unabaki pale pale kwamba magazeti ya udaku yanaandika maswala ya jinsia kuliko magazeti tunayoyaita ni makini.

Karibia magazeti yote ya udaku kurasa zake za mbele zinapambwa na masuala ya jinsia. Mifano ya magazeti haya na habari zinayoandika ni mingi. Inahusu wanasiasa kushiriki ngono; mafumanizi, ufusika wa kupindukia na nyingine nyingi. Ingawa hapa ninatoa mfano wa habari katika magazeti machache tu, ukweli ni kwamba karibia magazeti yote ya udaku yanaandika mambo ya jinsia na yaliyo tofauti. Hakuna gazeti linalorudia yale yaliyoandikwa na gazeti jingine. Kila gazeti linajitahidi kuibua kitu kipya. Ukitaka kufahamu hali ya jinsia ilivyo katika taifa letu la Tanzania, soma magazeti ya udaku.

Wanaharakati wa kujenga vuguvugu la kumkomboa mwanamke kimapinduzi, wanaharakati wa haki za binadamu na wanaharakati wote wanaotetea usawa wa kijinsia, watakubaliana na mimi kwamba niliyoyataja hapo juu ni masuala ya jinsia. Ni nadra sana kuona magazeti makini yakibeba maswala ya jinsia kwenye kurasa za mbele. Ikitokea yakawemo ni katikati na yanapewa nafasi ndogo kinyume na yanavyofanya magazeti ya udaku.

Inawezekana kwamba habari hizo zinakuwa zimehakikiwa na kuchujwa na wamiliki au na hata Serikali. Habari nyingine zinachujwa na viongozi wa dini na zile ambazo ni nyeti zaidi zinafunikwa na kufichwa kabisa hadi Kristo atakaporudi mara ya pili! Kwa njia hii hatuwezi kujisahihisha, kwa njia hii hatuwezi kuendelea. Nchi nyingi zilizoendelea zimeheshimu na kukumbatia usawa wa kijinsia.

Magazeti tunayoyaita makini yanaandika habari za siasa, za wanasiasa na matukio yanayowahusu wanasiasa hasa katika kurasa zile za mbele. Haina maana kwamba haya nayo si muhimu katika jamii. Ila ni kwamba magazeti yale tunayoyaita makini hayazingatii habari za jinsia.

Pia waandishi wa magazeti haya tofauti na ilivyo kwa magazeti ya udaku, hawajitumi kutafuta habari kwenye vyanzo mbali mbali. Mara nyingi wanajikita kwenye vyanzo vya kiserikali; kusubiri pale Maelezo au kusubiri mikutano ya viongozi wakuu na waandishi wa habari. Pia wamejenga utamaduni wa kutafuta habari za matukio mbali mbali kama vile vifo, kupigwa, kubakwa kutoka kwa makamanda wa polisi wa wilaya na mikoa. Matokeo yake ni kwamba, haya magazeti yetu makini, ukisoma mmoja huna haja ya kusoma jingine. Wakati mwingine unakuta karibia magazeti yote yana habari ile ile kwenye kurasa za mbele.

Hata ukisoma kurasa za ndani unakuta habari zinafanana. Kwa wale wanaosikiliza mapitio ya magazeti kwenye runinga watakubaliana na hoja yangu maana anayeyapitia magazeti akishasoma habari za gazeti linalotangulia, anabaki kusema; " habari hii imejirudia karibia katika magazeti yote". Jambo hili linaeleweka vizuri, maana magazeti haya vyanzo vyao vya habari ni vilevile. Hawatafuti habari, wanasubiri kuletewa habari. Wanasubiri kuambiwa ni lipi la kuandika na ni lipi la kuacha. Kwa njia hii wanajikuta wanayaweka maswala ya jinsia pembeni.

Magazeti ya udaku hata yote yakitoka siku mmoja, ni vigumu yawe na habari zinazofanana. Waandishi wao wanatafuta habari. Hawategemei kupata habari kutoka maelezo au kusubiri mikutano ya waandishi wa habari na viongozi au watu maarufu katika taifa letu. Wanaingia ndani ya jamii na kutafuta habari zinazogusa maisha ya watu. Wanaibua mambo mengi ya jinsia. Wanaibua ukatili majumbani, wanaibua vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji wanavyofanyiwa wanawake na watoto, wanaibua matendo ya udanganyifu katika ndoa, wanaibua rushwa ya ngono, kwa ufupi wanaibua mambo yote yanayokwenda kinyume na maadili.

Ni kiasi gani yale yote yanayoibuliwa na magazeti ya udaku yanafanyiwa kazi ni swali la kujiuliza. Ni kiasi gani yanayoibuliwa yana ukweli pia ni swali la kujiuliza. Je, mashirika ya kutetea haki za binadamu, mashirika ya harakati za kujenga vuguvugu la kumkomboa mwanamke kimapinduzi ni kiasi gani wanatumia habari za udaku kuimarisha mapambano yao na mfumo dume? Je, na wanaharakati wanayanyanyapaa magazeti ya udaku? Wanayanyanyapaa magazeti yanayoandika na kuibua maswala ya jinsia?

Swali jingine, ambalo nimeligusia mwanzo mwa makala hii ni kiasi gani wamiliki na wahariri wa magazeti ya udaku wanafahamu umuhimu wa habari wanazoziandika? Ni kweli kwamba wanaandika habari hizi kuibua maswala ya kijinsia au imetokea tu bahati mbaya wakati wakiwa kwenye harakati za kutafuta fedha? Au walifanya utafiti na kudungua kwamba vijana wengi wanapenda kusoma habari zinazoelezea mahusiano ya mwanamke na mwanaume? Habari za mapenzi, habari za ngono na mambo yote yanayofanana na hayo? Vijana ni wengi – hivyo soko ni kubwa?

Je, wanaadika kuuza magazeti yao? Ili wapate fedha na kuwa matajiri? Kuwa matajiri kuisaidia jamii au kuwa matajiri kwa faida yao na familia zao? Au wanaandika kufundisha jamii? Wanaandika kuibua maswala ya jinsia kwa lengo la kusambaratisha mfumo dume ili kuleta usawa wa kijinsia? Wanaandika kwa vile wao ni wanaharakati? Au nao pamoja na kuandika majumbani kwao wanaendeleza mfumo dume?

Kuna haja ya kuyaangalia magazeti ya udaku kwa mtizamo mpya! Hata kama wanaoyaandaa wana malengo mengine, lakini yale wanayoyaibua kuna haja ya kuyafuatilia; kuna haja ya kufanya utafiti zaidi ili kubaini ukweli. Kwa njia hii tunaweza kutoa mchango mkubwa katika kujenga jamii inayoheshimu haki za binadamu na kuzingatia usawa wa jinsia.

Wakiandika juu ya fumanizi, tukio hili lifuatiliwe. Wakiandika juu ya ukatili majumbani, kwa vile wanatoa majina ya watu na wakati mwingine maeneo ya tukio, ni vyema matukIo haya yafuatiliwe kwa karibu. Wakiandika juu ya rushwa ya ngono, jambo hili lifuatiliwe. Wakiandika juu ya wabunge wetu kuwa na nyumba ndogo kule Dodoma, kuwasafirisha watoto wadogo hadi Dodoma ili kufanya nao vitendo vya ngono, jambo hili lifuatiliwe ili waheshimiwa wetu wawajibishwe na kusaidiwa kuyabadilisha maisha yao.

Wakiandika juu ya waheshimiwa wabunge kununua dawa za kuongeza nguvu za kiume kwa wingi wakati wa vikao vya Bunge, jambo hili lifuatiliwe – kwa nini wabunge wetu wahitaji nguvu za ziada kufanya tendo la ngono wakati wako mbali na familia zao? Bungeni wanahitaji nguvu za kufanya ngono au nguvu za kufikiri na kufanya kazi? Lolote litakalo andikwa na udaku lifuatiliwe, hasa kama linaibua habari za jinsia.

Chanzo: Raia Mwema - Magazeti ya udaku na jinsia
 
Last edited by a moderator:
Roulette nadhani watoto na vijana wana interests zao which should be recognised and respected. They have people and things which they perceive to be relevant to them. Nilipokuwa mtoto nilikuwa hivyo hivyo. Lakini umri unavyokwenda interests and perceptions zinabadilika. Inawezekana kabisa mtoto/kijana akajifunza kutoka kwa Wema kuliko kwa Naibu Spika wa bunge, maana hata mimi mzee mzima sina cha kujifunza kutoka kwa Naibu Spika kama kiongozi. Lakini kuna baadhi ya mambo ningependa kuyaongea hasa katika hoja ya kuwaanda watoto na vijana kuwa viongozi wa kesho.

Tunakoelekea kutahitaji more creativity, kuwa mjuzi kwenye teknologia, na uwezo wa kuunganisha watu na ideas. Tena kulingana na jinsi uchumi wa duania unavyoenda, watoto wa nchi kama zetu wanatakiwa kuyajua haya mambo mapema na kwa haraka zaidi. Kwa hiyo, nadhani watoto na vijana wasiandaliwe tuu kwa ajili ya leadership roles, bali kwa kila kitu ili wawe na competencies za kukabiliana na dunia inayokuja.

Kwanza, watoto waandaliwe ili wawe na tabia nzuri kama binadamu regardless of whether or not they want to be leaders (though naamini kila mtu ni leader). Hilo lenyewe ni muhimu sana. Kwa dunia ijayo itamchukua mtu miaka mingi sana kujenga reputuation, lakini hiyo reputation inaweza kuangamizwa na social media kwa siku moja tuu.

Story kama hii inasema mengi: BBC News - Paris Brown: Kent youth PCC resigns after Twitter row. Alichanguliwa na wapiga kura kama the youngest police commissioner in the United Kingdom at the age of 17. Baada ya hapo watu wakaja kuibua tweets ambazo ali-tweet wakati akiwa na umri wa miaka 14 na 16 na kumlazimisha kujiuzulu. Social media is a powerful tool for the youth, but it can also be powerless.

Siku hizi nasikia pia waajiri wengi huwa wanapitia pages za Facebook na Twitter kabla ya kuwaajiri watu. Many employers now want to know the character of potential employees. Probably kuna wengine would specifically ask for them. Kwa hiyo, watoto na vijana waelimishwe kuwa makini with what they post on social media, they may come to hunt them in future siyo kikazi bali kwenye nyanja nyingine pia. Unamkumbuka yaliyompata yule shahidi kwenye ile kesi ya Charles Taylor? Inawezekana bado Tanzania, lakini tunaelekea huko.

Pili, concept nzima ya jamii inabadilika. Siku hizi kuna online community. Watu hamjakutana lakini mko so close on the internet. Kama alivyosema mmoja “Facebook is for the people you know. Twitter [and JamiiForums] is for the people you wish you knew and Myspace is for the people you wish you NEVER met.”

Kwa hiyo, watoto na vijana waelimishwe kuwa responsible katika kujenga online communities. Kwa mfano, they should not add someone as a friend simply because that person sent them a friend request. Waangalie kama kuna connection yoyote in terms of interests and what can be learned from each other. Quality rather than quantity ya friends and who you follow is much better.

In addition, viongozi wengi wa sasa nao wanaongezeka kwenye social media. So, badala ya watoto na vijana kuishia kuwambia tuu viongozi kwenye social media “Go go kiongozi wangu”, “nakuaminia Mkuu wangu”, “You’re my role model”, "You're always right, Mkuu wangu", "I trust you, Boss wangu", n.k., waelimishwe kuwa na tabia ya kuchangia as thought or future leaders kwenye mijadala inayoendelea social media. Wawe na tabia ya kutaka kuhoji kinachoandikwa na viongozi kwa kufuata hoja zao badala ya viongozi wenyewe.

Viongozi nao wawe na tabia ya kuwa-engage vijana kwenye social media. Nimeshaandika sana hapa juu ya tabia ya baadhi ya viongozi kutundika status au tweet na kusepa huku wakisubiri watu wa-like au wa-tweet status zao au kumwagiwa masifa. Hii inaweza kuwadumaza vijana, kwa sababu watadhani social media works just like conventional media.

Hapa ndipo social media inapokuwa powerless kwa watoto na vijana maana wanapowauliza hawa viongizi maswali, mengi hayajibiwi. Kuwa interactive means to engage people, testing their understanding, listen to them, etc, hata kama hukubaliani nao. Nilishasikia kuwa kuna watoto na vijana ambao hawasikilizwi majumbani mwao, kwa hiyo wanaona social media ni tool ya kusikilizwa. Kama na huko hawasikilizwi na wanaowaamini kuwa ni viongozi wao, then we are not doing any better for them.

Tatu, dunia inaangamizwa kwa njia mbalimbali kama uharibifu wa mazingira. Watoto na vijana waelimishwe maana ya “sustainability”. Tembo wetu wanaangamia. Waelimishwe athari na impact yake kwenye maisha yao ya baadae.

Nne, siku hizi kuna information nyingi sana. Pia it is becoming easier and easier to access the information. Watoto na vijana waelimishe kuwa not all information out there is correct. Vijana wafundishwe kuwa pro-active katika kuunganisha data na kufikia conclusions za muafaka. Huko tuendako hakutakuwa tena maswali ya kujaza sehemu zilizo wazi kama vile Rais ya Tanzania ni Jakaya Kikwe__ (a) we, (b) ta (c) te. au yale maswali ya false and true.

Hakutakuwa tena na kukremisha mambo. Kwa hiyo, watoto na vijana waelimishwe kuwa na fikra tunduizi. Kwenye homework zao na hata kwenye mazungumzo ya kawaida tuu, wazazi wawe na tabia ya kuwauliza watoto maswali siyo ya kufikiri tuu bali ya kufikiri critically na ku-reason.

Kama mtoto au kijana anapenda kufuata sana habari za Wema au Diamond badala ya news za Dkt Slaa au Rais Kikwete sidhani kama kuna haja ya kumkataza kufanya hivyo. Best way ni kumshauri au kumfundisha jinsi ya kufikri critically. Inawezekana kuna mambo mazuri wanayofanya akina Wema na Diamond (of course yapo) and these kids will want to take the good ones (na kuacha mabaya yao) and build on them na kuwa artists wazuri zaidi. We need artists as well na siyo politicians tuu!

Watoto na vijana wafundishwe jinsi ya kutumia “common sense” kutatua matatizo yao madogo madogo. Siyo kila tatizo anatafuta ushauri kwa mama na baba. Tunaona sana hapa JF jinsi baadhi ya vijana wanavyoanzisha threads ambazo wengi tunaona kama jibu lipo wazi kabisa. Huko baadae waajiri hawatawa-train tena waajiriwa, bali wataajiri tuu watu ambayo tayari wanajua kufikiri na kutumia rasilimali vizuri.

Tano, tunakoelekea teknologia itaongeza ubora wa multi-tasking. Wengi tunajua kuwa multi-tasking inaongeza distraction na usahaulifu. Hapa sina maana ya kuwafundishwa watoto na vijana wa kiume kuongea huku wakipiga mswaki, though I am sure haitakuwa shida kwa Matesha wa Asprin. Lakini watoto na vijana wafundishwe jinsi ya ku-priotise mambo, jinsi ya kuwa focused na kujenga na kudumisha mahusiano na watu wengine.

Jukumu la nani? Kila mtu, kuanzia, mzazi, ndugu, rafiki, viongozi, taasisi na jamii kwa ujumla.

well mkuu EMT ata wahenga wanasema samaki mkunje angali mbichi..
 
EMT, the point is not stopping them from being young, or forcing them to be interested in siasa, but it is important to know where they get their information from and who they listen to. Maybe it can be part of a communication strategy going forward?
Ona "Kigoma All Stars" and their song Nyumbani. It was a good project, and it contributes to pass on a patriotic message. In Kenya I saw a soap about youth in a campus, with a pop DJ from a radio etc, but the thread of the series is HIV awareness. See? it is important to know who our youth are, what they do, where they get info from etc.
Nurturing their leadership will then be adapred to their interest, or their talents.

View attachment 98498

hii katuni inakufanya ufikie zaidi ya kurahisisha unachokifikiri..
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom