Kwa mujibu wa kitabu cha Yashari Ibrahimu alizaliwa kwa ishara ya nyota na alifichwa pangoni na babake Terah kwa miaka kumi

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,209
4,706
Wadau hamjamboni nyote?

Huu ndiyo ukweli kuhusu kuzaliwa Kwa Ibrahimu aliye baba yetu wa Imani Kwa mujibu wa kitabu cha Yashari (Jasher) 8

Ibrahimu alizaliwa na Terah kwa ishara ya nyota sawasawa na alivyozaliwa Yesu Kristo. Nyota moja kubwa ilionekana angani ikitokea upande wa Mashariki na kuzimeza nyota nyingine 4 zilizozunguka pande zote za dunia

Mfalme Nimrod aliyetawala wakati huo aliarifiwa na wataalamu wake kuhusu kuzaliwa kwa Ibrahimu na tafsiri ya ishara ya nyota hizo.

Wataalamu hao walimwambia Mfalme kuwa Ibrahimu atakuwa mtawala mkubwa atakayemiliki ardhi kubwa, watoto wengi na atakayeua wafalme wote wa Duniani.

Wataalamu hao walimshauri Mfalme Nimrod ili kujinusuru basi amuue Mtoto Ibrahimu ili KUZUIA Unabii huo kutimia

Mfalme huyo Kwa hofu aliagiza Terah alimkabidhi mtoto wake huyo kwake mara moja

Mfalme alipokabidhiwa Mtoto huyo ( aliyeamini kuwa ni Mtoto Ibrahimu) alimshika kisha kumtupa kwa nguvu kubwa ardhini akiamini amempasia kichwa na kumuua Ibrahimu

Hata hivyo huyo aliyedhaniwa kufa hakuwa Mtoto Ibrahimu bali ulikuwa ni muujiza wa Mungu ili kumnusuru Mtoto Ibrahimu

Terah alimficha Mwanae Ibrahimu na Mamaye na mjakazi wake kwenye Pango kwa muda wa miaka kumi

Ahadi ya kuua wafalme ilitimizwa na mjukuu wa Ibrahimu aendaye Kwa jina la Esau ambaye alikuja kumuua Mfalme Nimrodi

Karibuni tujadili
 
Watu wa kipindi cha manabii na mitume waliishi kwenye mazingira magumu sana.
Ebullient fikiria leo mtu ajitokeze aseme yeye ni nabii au mtume wa mungu.
Unadhani ni rahisi kumuamini?.
Sasa waza kipindi kile yesu na Muhammad wanajitokeza mbele za watu na kudai utume.sio mchezo.

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom