Report Card ya Meya wa Ilala: Jerry Silaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Report Card ya Meya wa Ilala: Jerry Silaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Game Theory, Jan 6, 2012.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2012
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Mwaka ushapita sasa tunaomba wana ILALA na wana Dar na JFkwa ujumle mtuleteee report card ya huyu JERRY SILAA ambaye pia ni member wa JF humu so natumai atakuja kutupatia majibu ya maswali yetu hasa ukizingatia yeye ni meya wa wilaya tajiri kuliko zote Tanzania ambayo ni pamoja na Ikulu ambayo iko chini yake.


  [​IMG]

  Je Meya huyu alitoa ahadi zipi kwa wana ILALA

  Je ana elimu gani?

  Komsomea nini

  Kasoma wapi?

  Je kashatekeleza ngapi?

  Je yumo kwenye kamati zipi?

  Je anato access kwa wapiga kura wake?

  Je ana ofisi jimboni kwake?

  Je anayo website?

  Je anayo namba maalum ya kuwasiliana na wapiga kura wake?

  Je anayo Facebook page?

  Je anapatikana kwenye Twitter?

  Je ana fanya surgery (kukutana na kuwasikiliza ) wapiga kura wake?

  Je ame declare interests zipi kama mtumishi wa umma?

  Je analipwa mshahara kiasi gani?

  Je anachukua posho?

  Kiasi gani anachukua kwa mwezi?

  Je wana ILALA wanamaoni gani kuhusu performance yake?

  Je potential competitors wake in 2015 ni akina nani?

  Je ana maoni gani kuhusiana na blue print ya kuliendeleza jumbo la ILALA?

  Je amopokea zawadi sosote toka kwa wafanyabiashara au watu binafsi?

  Zawadi hizo ni zipi?

  Je ame declare kama amepokea hizo zawadi?

  Je private life yake ni reflection ya hao anawa wakilisha?

  Je ILALA kuna issues 5 kubwa ambazo alitakiwa kuzishughulia je ni zipi?

  Je ana shiriki kwenye shughuli za kijamii (yuko close na wapiga kura wake) auhaonekani mpaka kutokee issue yenye kumpa publicity?


  Je kwa Mtazamo wa haraka haraka JERRY SILAA atarudishwa tena na wan ILALA in2015?

  Je ni Cabinet material? If so wizara gani itamfaa?

  Rough estimates za Budget ya JERRY kuwa Meya wa ILALA ni kiasigani?
   
 2. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Kwa ufupi tu ni kwamba amepwaya sana katika wadhifa huo wa meya wa manispaa ya ilala. Na hilo limewaumiza sana vijana ambao wamekuwa wakijitahidi kudai nafasi za uongozi ili waongoze kwa mifano.

  Mapato ya manispaa ya ilala yameongezeka toka sh. 16 bilioni hadi sh. 26 bilioni, lakini hakuna shughuli yoyote ya kimaendeleo inayoonekana kufanywa kwa maslahi ya wananchi.
  Masoko ni machafu, mitaro imeziba, mitaa ni michafu, hospitali,zahanati na vituo vya afya havina madawa, vifaa tiba wala wahudumu wa kutosha hasa vilivyoko nje ya mji kama ukonga, kitunda,chanika na kwingineko. Barabara za manispaa ni mbaya sana na hazifanyiwi matengenezo yanayostahili ili zipitike muda wote wa mwaka.

  Anachofanya sasahivi kwa umakini ni kukusanya fedha za kununulia ubunge 2015! Hana muda na shughuli za maendeleo ya wananchi wa manispaa ya ilala.
   
 3. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Duh Mkuu unataka kujua hadi analipwa Mshahara kiasi gani?, ukishajua Mshahara wake itakusaidia nini/utafanya nini?
  Nadhani la msingi aeleze ameifanyia nini Ilala so far......
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Jan 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Kwani qualification ya kuwa meya wa wilaya tajiri ni ipi?
  Ukijua Mshahara wake utasaidia kitu gani kama si umbea na upashukuna?
  Ku declare interests depends on time and situation Mkuu, usitarajie utapata majibu ya haraka haraka. Hebu Mwulize Jk kama alishawahi ku declare interests zake transparently!
  Madiwani wa Ilala waliomchagua kuwa Meya ndiyo wenye panga la kumwondoa kama hajawatendea aliyopasa kuwatendea.
  Acha majungu, leta topics zenye hoja za msingi!
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Jan 6, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  huyu jamaa alikuwa 'hafai hata kuwa naibu meya'
  sasa sijui mnataka report ipi.......

  mimi nakumbuka alichokifanya toka nimsikie ni kukodi limousine na kuwasindikiza warembo wa miss ilala
  kwenda kambi ya miss tanzania huku akipigwa picha na waandishi wa habari na kufunga ofisi siku nzima kwa shughuli hiyo.....

  he is a burden kwa jamiiii....
   
 6. E

  EMMANUELEY Member

  #6
  Jan 6, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  sina hakika na utajiri wa ilala kama ni kweli kushinda TANDAHIMBA
   
 7. F

  FMuhomi Member

  #7
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Amesoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Amemaliza Mwaka 2005, Degree ya BSc. Electronics, wakati akiwa chuo amewahi kushika uongozi kama Waziri wa Mambo ya Kijamii.

  Nawasilisha
   
 8. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  ni kweli kabisa mkuu yuko bize kukusanya hela za kununua ubunge 2015. udiwani atamwachia MSAFIRI DK waliyegombea nae udwn kwa tkt ya magamba 2010.
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Jan 6, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ilala ni tajir kuliko wilaya zote?kweli?nifafanulie mdau,
   
 10. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #10
  Jan 6, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,367
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  Wana JF,

  Napenda kuweka kumbukumbu sawa ndugu zangu, Silaa mnamuadama bure pasipo sababu zozote za msingi, jana niliomba tuache unafki lakini naona chokochoko bado zinaendelea, business as usual siyo!? Sasa kama kuna mtu anataka kujua Silaa kafanya nini basi aende ofisini kwake akaombe ufafanuzi wa specific issues anazodhani ndio suluhu kwa matatizo ya wana ilala, ni aibu na fedheha kuhoji vitu vya kipuuzi kama zawadi, website, facebook ama upuuzi wa twita, hivi ni mpuuzi gani anayehoji maendeleo ya kiongozi kupitia facebook? Ni wangapi wanzojua kwamba facebook is actually there!?

  Ni watanzania wangapi wanaojua kama mamitandao haya na je ni wangapi wanayatembelea ili kuchafua wenzao, sasa kama mnadhani umeya wa Silaa umetokea facebook ama umetokana na elimu yake basi ni ujinga na kamwe mjinga haelimishiki, watu wa ilala wamemuamini na ndio maana wameamua kumchagua awe kichwa chao. Hatuwezi kuvumilia upuuzi huu usambae bila sababu za msingi, hivi na wewe Silaa tutakutetea hadi lini? Hivi kama una majibu si afadhali uwajibu hawa wafitini yaishe, kukaa kimya kwako kunatufanyz tuamini kwamba na wewe sil msafi na ni kweli upoupo tu.

  Toa ufafanuzi aisee, usidhani chokochoko hii itaishia humu na usidhani watu wanafurahia umeya wako, wenzako wanalenga kukulegeza na kukudhoofu usifikirie ubunge 2015, sasa we kenua meno utaona wanavyokuchafua, amka.

  Ni mimi
  Pangu Pakavu
  Nawasalimia.
   
 11. J

  Jerry Silaa Verified User

  #11
  Jan 7, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante Hossam
  Kwa faida ya wapenda maendeleo.
  Bsc Electronics & Communication UDSM 2005
  Atec II NBAA 2003
  Cert in Law UDSM 2005
  Siku mbili za kuona wananchi ,Monday & Friday
  Kata ya Gongolamboto ni mpya kwa sasa tunatumia ofisi za kata ya Ukonga.
  Website ya Council www.imc.co.tz
  Namba ya wapiga kura ipo,lakini utaratibu mzuri ni kutumia forum zilizopo kuwasilisha.
  Twitter Jerry Silaa
  Upo muda maalum wa kukutana na wapiga kura. Kwa ujumla wananchi wanawakilishwa na waheshimiwa madiwani na wenyeviti wa mitaa. Hawa they are free to see me anytime.
  Mimi sio mtumishi wa umma, ni kiongozi wa umma na ninadeclear mali na madeni chini ya Tamko kwa mujibu wa sheria ya maadili ya viongozi kila mwaka kabla ya 31st Dec.
  Sina mshahara.
  Posho 240,000 kwa mwezi na sitting allowance 60,000 kwa vikao ninavyohudhuria with a maximum ya vikao vinne kwa mwezi.
  Hayo ya Ilala watajibu wenyewe.
  Ilala ni manispaa sio jimbo na upo mango mkakati nitauweka kwenye website.
  Sheria ya umaadili ya TZ ni tofauti ya marekani na haitoi fursa ya kudeclear zawadi. Lakini mimi sio mpokeaji mzuri wa zawadi za kiofisi. Integrity yangu kwa wafanyabiashara u can reserch.
  Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya madiwani ya mwaka 1979 inamtaka udiwani kama shughuli ya kujitolea na diwani anapashwa kuwa na shughuli tofauti na nafasi nyingine za umma, udiwani hauna reflection ya lifestyle. Na kwa kuwa kiongozi wa metropolitan hakuna lifestyle utayoishi ikareflect wananchi wote.
  Ushiriki wa shughuli za umma ndio majukumu ya msingi ya kiongozi ws kisiasa. Majibu mazuri ungewauliza waigakura wa Gongolamboto na General Public, majukumu nimengi na pale muda unaporuhusu tunashiriki. Sasa kama kuna mwandishi amecover ukaiita publicity sawa, lakini na yenyewe muhimu ili watu kama nyie muone ushiriki.
  Uchaguzi wa 2015 kwa style yangu ya siasa utazungumzwa 2015. Na kwa taarifa yako siasa ya nchi hii what u have done itakupa 20-30 %.
  Bajet ya umeya : fomu lak 2, mafuta ya kuzungukia kuomba kura, simu ya logistics + 7m ya udiwani.
  Facebook Jerry Silaa
   
 12. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #12
  Jan 7, 2012
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,763
  Trophy Points: 280

  Mh. Silaa asante sana kwa majibu yako mafupi lakini yanayotia moyo na kuonyesha kwamba wewe ni kiongozi msikivu. Maana hata kujibu humu unaonyesha wewe ni mtu wa namna gani. Salute

  Mh. Kama kijana mwenzako, naomba nikiri kwamba uongozi wako una maana kubwa kwetu vijana. Utendaji wako utatufanya vijana wengi tuwe na imani katika siasa au tuikimbie tukiamini ni sehemu ya ufisadi kujineemesha. So keep up the hard work. Its never easy lakini yanawezekana.

  Nina ushauri hapa kwako na ofisi yako katika kutafuta suluhu ya mambo kadhaa.

  1. Wilaya yetu ya Ilala ni chafu ndugu yangu. Uchafu umezidi kila sehemu na rarely anybody cares. Mimi ombi langu, kwa nini usilivalie njuga hili swala mkuu? Kwanza kabisa ningeshauri uanze na wote wanaokabidhiwa tenda ya kuzoa takataka. Ofisi yako ihakikishe kwamba kila anayeomba tenda hiyo ana vifaa vya kutosha na wafanyakazi wa kutosha. Naamini na wewe umeshashuhudia magari chakavu yakiwa yanasomba taka hapa mjini, sasa unashindwa kuelewa tofauti ya uchafu na gari iliyobeba uchafu. Maana gari nyingi ni chakavu kuliko maelelezo. Hili jambo linakera na inaonekana viongozi either wana interests na haya makampuni kama shareholders au they simply dont care!

  2. Ofisi yako ihakikishe haya makampuni yanazingatia sheria za kazi kwa watumishi wao. Ni jambo la kusikitisha unakuta akina mama wakiwa wanafagia barabara za mjini hapa bila protection yoyote kwenye jua la Dar. Ni hali inayotishia usalama wa afya zao. Hili nalo livalie njuga. You will make a difference in the lives of your fellow citizens. Kampuni kama inataka tenda ya usafi ihakikishe wafanyakazi wanapewa vitendea kazi stahiki kulinda afya zao.

  3. Kuna swala la huduma za msingi kama maji, afya nk. Hebu jitahidi mkuu ujipambanue kwa kuonyesha kwamba inawezekana. Arguably matatizo ya hapa mjini ni mengi na yanahusisha cross-section ya idara. Lakini wewe waweza kufanya mengi na wananchi certainly tutakusupport.

  4. Swala la foleni mjini. Ningeshauri uwasiliane na idara nyingine husika muangalie namna ya ku-control haya magari yanayojazana mjini kati (CBD). Seriously najua wengi humu hawatakubaliana na mimi, lakini kutokana na miundo mbinu yetu ilivyochoka na michache..you guys should make it difficult to drive in town especially kwenye rush hours! ILA hili liende sambamba na miundo mbinu kama kuboresha public transport. Ultimately hatuwezi ku-pretend kwamba Dar itaendelea kwa mtindo huu bila kuchukua maamuzi magumu na 'unpopular'. Kama kulipisha kodi kila gari linaloingia mjini katika mida fulani fulani. Ila as I said, ufanye hivi kwa ku-invest in alternative transport mechanism.

  5. Mh. Silaa, mimi nakupongeza na naelewa kabisa uongozi wa sehemu kama Dar si lelemama. Lakini I can assure you, ni watanzania wa leo wengi wanaelewa ukifanya kazi inayonekana we can support you kufanya makubwa zaidi.

  6. JIPAMBANUE uondokane na hii sense ya 'business as usual' kwenye mambo ya msingi yanayotuhusu wakazi wa mji huu.
   
 13. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #13
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 697
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mheshimiwa Jery Slaa naomba kukuuliza swali kama mpiga kura wako..
  Mkuu
  Kuna kipindi mzee Masaburii alitaka kuvunja mkataba na yule contractor uchwara anaeendesha soko la feri kwa kua hafagii wala vyoo japo vya shimo hajaachimba nakumbuka ulikawa mkali sana eti mzee anaingia kwenye 18 zako, nadhani aligusa maslahi flani... vipi mmefikia wapi na huyu dalali wa lile soko, mmesham terminate au bado anapeta tu, Kwa faida yako pale hua napita sana kula pweza na nakuta maji machafu yanachuruzika hadi barabarani kule!!i hadi hamu ya kul octopus wangu kwa ajili bukande inapotea mzee mwezio

  Nawasilisha
   
 14. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #14
  Jan 7, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,583
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  Ipe heshima yake kaka ni Bsc. Electronics and Telecomunication.
   
 15. J

  Jerry Silaa Verified User

  #15
  Jan 8, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maganga nakushukuru sana na unaonyesha unajua unachochangia.
  Nimeelezea vizuri mpango wa usafi jana kwenye ile thread ingine, in a short time utaona mabadiliko makubwa kwenye vifaa, watumishi na mpango. Ila changamoto itabaki kwenye usimamizi. Kama unakaa ilala mzee mtusaidie kamati za mazingira za kata na mtaa ni vyombo muhimu sana vya kujua kama mkandarasi anazoa taka ipasavyo. Vilevile tunahimiza vikundi vya kijamii CBOs kujikita kwenye shughuli za usafi maana wana maslahi na maeneo yao.

  Swala la ufagizi wa barabara tunahimiza mechanization, yale mafagio hayana nguvu ya kuondoa mchanga ndio maana lami zetu si nyeusi kwa ajili ya mchanga uliojikita muda mrefu.

  Huduma za jamii afya , elimu na maji zinahitaji uwekezaji, we are almost winning kuelectronise revenue collection ili kuongeza uwezo. Nimepata mhisani aliye tayari kutupa mtambo wa kuchimba visima na hii itapunguza gharama ambayo tunaingia sasa ya 20-30 m kwa kisima mpaka approx 3-6 m kwa kisima. Kitengo cha maji tunampango wa kukifanya idara kamili ili kuwaongezwa wananchi attention.

  Kwa sasa tunangoja mradi wa DART uamze maana hakuna relevant public transport then tutafanya gharama ya kuingia mjini. Kwa sasa tumeagiza mashirika hususan NHC kujenga parking cilos tuondoe utaratibu wa kuegesha magari barabarani. Itatoa eneo kubwa zaidi kwa magari kupita.

  Kama nilivyosema tatizo la Nafasi ninayoitumikia kabla iliendeshwa kwa business as usual, pili kuna matatizo ya legal framework. Kurekebisha by law kwa urasimu mpaka iende Tamisemi mpaka mpiga chapa mkuu aichape ni mwaka. Kubadilisha mfumo na tayari kuna mkandarasi na ana mkataba ni muda mrefu, kugundua mtumishi ambaye haendi kwa kasi yangu mpaka mipango ya kumuhamisha( kwa system za nchi hii) sio muda mdogo. Na uhakika mabadiliko makubwa yataanza kuonekana kwani maandalizi yamekamilika.


   
 16. J

  Jerry Silaa Verified User

  #16
  Jan 8, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa sasa hiyo kozi inaitwa hivyo, ingawa sisi tulisoma course za Telecomunication Engineering lakini Degree program iliitwa Bsc Electronics science and communication.
   
 17. J

  Jerry Silaa Verified User

  #17
  Jan 8, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa kuna issue tatu,
  Moja ni sheria na taratibu, mfano mimi nikuambie utoke humu JF! Dispite na ulichofanya lakini sina legal authority ya kukufukuza. Dr Masaburi yawezekana alukuwa na hoja za msingi ila utaratibu alotumia sio. Na nisingependa mfanyabiashara yoyote anayefanya biashara na IMC afanye in harmony na si kutishiwa termination bila kuzingatia huo mkataba unaelekezaje kuhusu termination. Maamuzi ya kisiasa yakivunja mkataba matokeo yake mmeyaona Dowans.

  Pili ni issue ya performance,
  Pale ferry kuna changamoto zake ambazo lazma tuziaddress kabla hatujaweza kidhati kupima perfomance ya mfanya usafi. Soko lile kwa utaratibu wa sasa wa kutaka mkurugenzi alisimamie ni ngumu, tumeunda bylaw ya service boards ili kulisogezea attention.

  Tatu issue ya interest haipo, yupo waziri mmoja aliniambia anaogopa kusukuma mambo eti ataambiwa ana interest. Ilala is a 91B sh council kama ingekuwa interest yapo maeneo makubwa mengi tu nisingefika kwa mfagizi wa feri. Kikubwa ni kuhakikisha mambo yanaendeshwa in harmony


   
 18. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #18
  Jan 8, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  mkuu inasemekana kuhusu upokeaji wa zawadi upo juu na ndio maana wanafunzi wa KAMPALA UNIVERSITY MPAKA LEO MMEWAPOTEZEA WW NA SERIKALI YAKO JAPO WAMEOMBA SANA MSAADA WAKO KTK UFUMBUZI WA MATATIZO YAO NA CHUO ICHO CHA MAGUMASHI.....
  LAkn mmekuwa kimya kwa kuwa kuna percent flani flani mnapata ili kuzibwa midomo....
  Kama si kweli je huelewi kinachoendelea pale chuoni ....
   
 19. c

  chama JF-Expert Member

  #19
  Jan 8, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mstahiki Meya;

  Rushwa, ukiritimba na ubadhirifu ni moja kati ya matatizo makubwa yanayozikabili manispaa na halmashauri nyingi Tanzania. Kwa ujumla Ilala inakabiliwa na matatizo makubwa kiutendaji, rushwa na ubadhirifu, je wewe ukiwa kama meya una mikakati gani ya kuifanya Ilala iwe kioo cha ufanisi? Pamoja na kuwa na ufanisi kwenye ukusanyaji wa mapato Ilala ni nini kinakwamisha shughuli za miradi ya maendeleo? Nimeona umeweka mkakati mkubwa kwenye ukusanyaji wa mapato kwenye nyanja za elimu na afya lakini hujaongelea kuboresha huduma za elimu na afya. Kuhusu uchimbaji wa visima hili ndio suluhisho pekee uliloona? Hii karne ya 21 ni lazima uende na wakati. Visima ni sulihisho la muda mfupi tu; kama meya lazima uwe na mipango ya muda mrefu kuondoa kero ya maji, la mwisho ni hizi tuhuma za ngono kama zipo zifanyie kazi; unahudumia jamii haileti picha nzuri kwa kiongozi, na inaweza kuchangia kuanguka kwako kisiasa.

  Chama
  Gongo la Mboto DSM
   
 20. O

  Ogah JF-Expert Member

  #20
  Jan 8, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mh Jerry Slaa

  Karibu sana.

  Una mikakati gani ya kushughulikia suala la mafuriko ndani ya wilaya yako na zaidi ukishirikiana na Mameya wa wilaya zingine.........hili ni tatizo sugu ambalo viongozi walio wengi Ilala wanalichukulia kama business as usual...........kuna kipindi ulitembelea US (please correct me if I'm wrong) nilitegemea suala la mafuriko ni suala ambalo ulitakiwa/unatakiwa ku-share the experience kutoka kwa wenzako wa nchi zingine........
   
Loading...