Reli ya standard gauge ya Rwanda na Tanzania ni kaburi la uchumi wa Tanzania

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
5,159
5,399
Ni kweli ndivyo ilivyo kadri ya maono yangu ya ndotoni usiku wa kuamkia leo.

Ninasema haya moyo wangu ukivuja machozi mazito ya huzuni kwani miaka kumi ijayo Tanzania hii itakuwa makapi na nchi ya kwanza kwa uzalishaji wa dhahabu Afrika yaweza kuwa Rwanda hapo baadaye.

Kagame si mpuuzi hadi kushinikiza suala hili chini ya utawala huu na kufanikiwa kwa asilimia 100%. Sijaona kitu chochote ambacho watanzania watanufaika nacho kwa ujenzi wa reli hiyo ambacho sasa hivi wanakikosa kwa kutokuwepo kwa reli hiyo. Msomaji yeyote akitaka kuelewa asome sentensi hii zaidi na zaidi. Ikiwa huwezi kuielewa ni bora usiendelee kusoma zaidi.

Mizigo inayosafirishwa kwa njia ya barabara na maji kwenda Rwanda bado haijaweza kufurika hadi miundo mbinu hiyo ikaelemewa na kuhitaji huu wa tatu kwa kiinchi kidogo kama Rwanda.

Mwaka fulani mkongomani mmoja aliwahi niambia kuwa batanzania banatucheka kuongoswa na huyu Joseph kabila ba bandia lakini ipo msiku nanyi batachekwa kama sisi.

Unapoingia mkataba hasa unaohusu nchi na nchi terms and conditions zitumikazo ni za kimataifa na hata kama unavunja lazima uwe umeumia.

Hata kama reli hiyo kwa kagame itatumika miaka minne tu kwake inatosha kutimiza malengo yake ya nchi.

Tumeliwa tena tumeliwa kuliko walivyoliwa wakongomani nchini mwao. JK kukataa kufungamana na kagame ilikuwa usalama kwa nchi hii. Kwanini tusijenge hiyo standard na wakenya ambako tutafaidi mengi au tujenge hiyo gauge kwa hizi reli za tazara na kati nakufufua zilizokufa eti tunakimbilia kujenga za huko kwa huyo mnyalu.

Naapa kabisa ujenzi huo ndo kaburi la uchumi Tanzania kutokana na aina ya mtu anayehitaji huduma hiyo. Jiulize anataka kusafirisha vitu gani ambavyo havisafirishiki kwa maji na barabara?.

Kwanini hakuhitaji kufanya hivyo na JK wakati wote wa utawala wake?

Kwanini aliwahi kumtukana JK kuwa anashindwa kuongoza nchi na akadai watanzania wampe bandari tu itatosha kuhudumia nchi ya Tanzania na Rwanda kwa kila kitu?.

Ni vema tuacha usaliti wa kukaa kimya ktk mambo ya msingi maana hakuna usaliti mbaya na wa hatari kama kukaa kimya.Watanzania tuseme maana hata wataalamu wa masuala ya investment sidhani kama calculations iliwapa jibu la kuaccept hiki kitu au kureject.

Wataalamu wamebaki kuongozwa na matamshi badala ya kanuni za kitaalamu ili kuweza kuamua. Ukweli inaniuma mno najua ndoto yangu hii yaweza isikubalike lakini nimekataa kuinamishwa kwa kukaa kimya maana itakuwa ni usaliti mbaya. Being silence is the most silence betrayal that kills faster.

Tafakuri njema.
 
Aisee kama haujasoma rudi shule kwa kweli khaa so unamaanisha sisi tunajenga reli sabu ya kagame? Hahaha unajua faida za reli kwa nchi? Hivi gharama za usafirishaji wa mizigo Kwa njia ya reli ni sawa na njia ya bara bara? Hahaha nacheka kwa dharau...afu sijaona hoja why iwe ndio chanzo cha kuanguka uchumi?
 
Aisee kama haujasoma rudi shule kwa kweli khaa so unamaanisha sisi tunajenga reli sabu ya kagame? Idiotic thinking hii... Hahaha unajua faida za reli kwa nchi? Hivi gharama za usafirishaji wa mizigo Kwa njia ya reli ni sawa na njia ya bara bara? Hahaha nacheka kwa dharau sababu haujielewi...afu sijaona hoja why iwe ndio chanzo cha kuanguka uchumi?

Reli ni mhimu lakini si lazima ijengwe lazima uangalie aspects nyingi. Huko unakojenga reli mizigo haifiki kwa sasa?. Kama inafika kwa njia gani?.

Usinitoe relini kwangu hiyo reli siyo kitu kwa nchi na lengo ingekuwa kufaidika na reli angeanza na ya Zambia ambapo nchi nyingi zinaitumia siyo hako katarafa ka Rwanda.
 
shida hawa watusi na wahutu wanagombana kila mahali huku hakuna ukabila wenu wa kujinga,kama una dhahabu au hela aliyekuzuia kununua ni nani? mnakaogopa kanchi ambako hata mkoa wa kigoma mkubwa na kama alisema JK bandari ilimshinda kwani sio kweli? banyamulenge hivi kwenu hamna forum muendelee na stori zenu za kikabila .mnatuboa sana!!!!
 
shida hawa watusi na wahutu wanagombana kila mahali wewe mla panya wa swanga huku hakuna ukabila wenu wa kujinga,kama una dhahabu au hela aliyekuzuia kununua ni nani? mnakaogopa kanchi ambako hata mkoa wa kigoma mkubwa na kama alisema JK bandari ilimshinda kwani sio kweli? banyamulenge hivi kwenu hamna forum muendelee na stori zenu za kikabila .mnatuboa sana!!!!
Kila mtu atakushangaa ukidai tz tuna ukabila.
Sijaona umejenga hoja zaidi ya lawama juu yangu kuleta uzi. Nataka ujenge hoja ya kuniaminisha kuwa tz wakabila, ya kuniaminisha kuwa JK alishindwa na huyu amefaulu, kivipi na kwa data zipi.
Jenga hoja utaeleweka.
Ukiona mtu kabla hajapost anaanza lawama kwa mtoa post ni ishara ya kukosa hoja. Leta hoja kujibu hoja yangu.
 
Kama MITAZAMO ndo kama hii hii frankly speaking bado tuna SAFARI NDEFU sana as Tanzanians kuufikia UKOMBOZI wa KIFIKRA ...
Unadhani kwa maelezo yako hayo ndo viwanda vitajengwa. Nataka ujibu hoja kwa hoja.
Niambie hiyo reli inataka ibebe kitu gani ambacho kimeshindwa kubebeka kwa njia ya barabara,maji na anga.
Huko treni it a be a nini toka Rwanda ambacho ni kizito mno hakibebeki kwa mode of transportation zilizopo.
Mbona reli ya tazara na kati zipo na miundombinu mibovu hamsemi?.
Acha kunihamisha relini mi siwezi kukaa kimya kwa matusi yako nakusubiri hapa ulete hoja ya maana siyo ooo oh ukabila, sijui mange leteni hoja acheni mambo ya udaku kwenye serious issue.

Sisi tunaumizwa nyinyi mnashangilia.
 
Kwani drc wanaumiaje kupitia kwa huyu hadi uone zangu ni hisia.
Hata wanaolia sasa huko kongo waliona ni hisia kama unavyoona wewe.
Nani amekwambia kuwa conflicts za DRC zilianzishwa na Rwanda? Umesoma historia vizuri? Matatizo ya DRC yalianza kabla hata Kagame hajafikiria kuwa kuna siku atakiwa rais..Kagame alikuja kutumia fursa ya vurugu za Congo baadae sana!
 
Unadhani kwa maelezo yako hayo ndo viwanda vitajengwa. Nataka ujibu hoja kwa hoja.
Niambie hiyo reli inataka ibebe kitu gani ambacho kimeshindwa kubebeka kwa njia ya barabara,maji na anga.
Huko treni it a be a nini toka Rwanda ambacho ni kizito mno hakibebeki kwa mode of transportation zilizopo.
Mbona reli ya tazara na kati zipo na miundombinu mibovu hamsemi?.
Acha kunihamisha relini mi siwezi kukaa kimya kwa matusi yako nakusubiri hapa ulete hoja ya maana siyo ooo oh ukabila, sijui mange leteni hoja acheni mambo ya udaku kwenye serious issue.

Sisi tunaumizwa nyinyi mnashangilia.
Treni ni cheaper kuliko hizo mode zingine za transport.cost of doing business zitakuwa chini sana na bidhaa zitakuwa bei chini hivyo kunufaisha wananchi wa kawaida.
 
Back
Top Bottom