MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,225
- 50,368
- Imepewa jina Madaraka Express, ile aliyojenga mkoloni zaidi ya miaka 100 iliyopita iliitwa Lunatic Express
- Ya abiria itabeba watu 1,200 kwa mpigo
- Inter-city itasafiri kwa masaa manne Nairobi-Mombasa bila kusimama
- Inter-county itasafiri kwa masaa matano baina ya Nairobi na Mombasa ambapo kuna vituo 9 katikati
- Kasi yake ni 120km/h
- Umbali ni 472km
- Nauli ni Ksh700 (TZS 15,000)
- Itagharimu Kshs 50,000 kusafirisha kontena, awali iligharimu Kshs 100,000 kusafirisha kwa malori, hivyo gharama imepunguzwa kwa nusu, tunasubiri Waganda, Wanyarwanda na batoto ba Kongo DRC kuwaza upya
- Jana imezinduliwa ya mizigo, leo rais anazindua ya abiria na atasafiri nayo hadi Nairobi kutokea Mombasa.
=====
Kenya imezindua reli mpya kati ya mji wa Mombasa hadi Nairobi ikiwa ni miezi 18 mapema.
Reli hiyo iliotengezwa kupitia ufadhili wa shilingi bilioni 3.2 kutoka serikali ya China ndio mradi mkubwa wa miundo msingi kuwahi kutekelezwa na serikali tangu taifa hilo lijipatie uhuru wake.
Mradi huo umechukua takriban miaka mitatu na nusu kwa kutumia teknolojia ya ujenzi wa reli ya China kukamilika.
Ni reli ya kwanza katika kipindi cha karne moja.
Safari ya kutoka Mombasa kuelekea Nairobi na treni ya kisasa itachukua saa nne na nusu ikilinganishwa na saa tisa kwa kutumia basi na saa 12 kwa kutumia treni ya zamani.
Nauli ya watu watakaokalia viti vya kawaida ni shilingi 900 huku wale watakaosafiri kwa kutumia business class wakilipa shilingi 3,000.
Rais Uhuru Kenyatta alisema wakati wa uzinduzi wa reli hiyo ambayo imeanzishwa mwamko mpya katika historia ya Kenya.
''Historia ilianzwa miaka122 iliopita wakati Waingereza waliokuwa wametawala taifa hili walipoanzisha treni hiyo iliokuwa haijulikani inakokwenda na kupewa jina Lunatic Express
''Leo licha ya kukosolewa pakubwa tunasherehekea Madaraka Express {ikitajwa baada ya siku ambayo Wakenya walijipatia uhuru wao kikamilifu} badala ya Lunatic Express.
Gharama ya mradi huo imekosolewa na upinzani ambao unasema mradi huo umeigharimu Kenya fedha nyingi mno.
Vilevile wamemshutumu rais Kenyatta kwa kuomba fedha kutoka China bila mpango.
Serikali nayo inasema kuwa ni sharti iwekeze katika miundo msingi ili kuvutia wawekezaji.