Relaxer ipi nzuri kwa nywele fupi?

Veronica7598

JF-Expert Member
Jan 2, 2017
361
408
Habari wadau
Naomba mnijuze ni dawa ipi ya nywele nzuri, inaweza nifaa kwa hizi nywele zangu fupi?

Nikisema fupi sio fupi sna nasuka mpaka nywele sita, ila tatizo kipilipili kimezidi nataka nizilainishe kwa relaxer yoyote then niendelee kusuka. Maana ni nyingi na zimekatika sna mbele na nyuma hata ukisuka unakuta za mbele zinasimama.

Msaada kwa wataalam plz
 
Texturizer sio ndio itafaa zaidi?
Kama hii hapa chini.
Kwa nywele fupi halafu kama zimekatika ukiweka relaxer kabisa inaweza kuwa too strong.
Hata relaxer ya watoto ni nzuri zaidi kwa nywele zilizokatika.


1490353787938.jpg
 
Kuna mafuta pia mazuri yanalainisha nywele, yanakuza nywele na kuzuia kukatika bila kuweka dawa.. Ukihitaji Mafuta hayo kuyaona na kujua bei yake njoo watsap kwa namba hii 0672416294
 
Kama bado haujaweka Dawa, nakushauri usizianze Hizo dawa japo ndo maamuzi yako yalipofikia.
Nakwambia hivi Labda kwasaabu haujajua madhara yake hasa hasa kwa nywele ambazo kwa wakati huo ziko weak Yaani zinakatika.
Dawa itasababisha nywele yako iwe hatarini zaidi kukatika kwa kuidhoofisha.
Nashauri ununue hair moisturizing cream/lotion for natural hair,pia ufanye deep conditioning with deep conditioner for natural hair,Unaweza kufanya hii hata Nyumbani kwako,alafu upake leave in conditioner Pamoja na hair moisturizer,Unaweza kutumia leave in conditioner Kama moisturizer pia zikiwa bado zina ubichi wa maji, malizia na mafuta.jitahidi hivi kila uoshapo nywele utaona mabadiliko makubwa.
The best kwenye maamuzi yako.
 
Back
Top Bottom