Reginald Mengi: Ipo siku Mafisadi wataongoza nchi

Reginald Mengi: Ipo siku Mafisadi wataongoza nchi

Mbona kituo chako cha ITV ndicho kinachowainua mkuu au wanakulipa kwani? Wapotezee kwenye habari zako kwani watakufanya nini?
 
Nahis anamwongelea lowasa ambae ilithibitika kuwa fisadi na ni mgombea wa ccm kiti cha urais 2015 watch out ppo
 
Mwenyekiti wa makampuni ya IPP bwana Reginald Mengi amesema kwa hali ya kisiasa inavyoendelea ipo siku mafisadi wataongoza nchi kwa kuwa mpaka leo hawajachukuliwa hatua zozote za kuwakamata na kuwafungulia mashataka. Na serikali imekaa kimya

Anazungumzia siku ipi wakati hata sasa serikali inaongozwa na kusimamiwa na hao mafisadi
 
Mzee Mengi acha hizo bhana!!!! Yaani unatuchomekea mpira ili tuseme sio. Poa tu lakini.
 
mengi yupo sawa ina nae hao mafisadi ndio rafiki rake
 
Dr-Reginald-Mengi-July12-2013.jpg


Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, (aliyesimama), akizungumza kwenye majadiliano yaliyohusu utaratibu wa ulipaji kodi za serikali kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam jana.

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, amesema ikiwa mafisadi hawatadhibitiwa, iko hatari wakajiimarisha kufikia hatua ya kuiongoza nchi siku zijazo.
Dk. Mengi alitoa kauli hiyo jana kwenye kongamano la siku moja baina ya serikali, taasisi za serikali na wafanyabiashara, lililokwenda sambamba na uzinduzi wa ripoti mtazamo wa viongozi wa biashara kuhusu mazingira ya uwekezaji Tanzania mwaka 2013.
“Wala rushwa wakubwa ni kina nani na wako wangapi? Ukiniuliza mimi nitakwambia hawazidi wanne, wanafahamika ila sitawataja kwa leo,” alibainisha.
Alisema rushwa kubwa ipo nchinina tuendako ana wasiwasi kuwa wala rushwa wakubwa ndiyo watatawala nchi kupitia matakwa yao kwa nchi kuongozwa na kutawaliwa na watu wasioonekana wala kujulikana.
“Ni watu wenye nguvu wanajipenyeza hadi katika vyombo vya dola, mtu anaweza kupoteza kazi kwa uamuzi wao,” alisema.
Dk. Mengi aliongeza kuwa wapo wanaosema tatizo la rushwa litamalizwa kwa utashi wa kisiasa, lakini hauwezi kufanikiwakama hakuna utekelezaji na kutambua kuwa rushwa kubwa inateketeza Taifa.
Alisema kuna sababu nne zinazosababisha mafisadi wasishughulikiwe ikiwamo kuogopwa kwa kuwa wana nguvu za kuwadhuru wanaowashughulikia, mlolongo wa utoaji rushwa na kuna wanaonufaika na ndiyo wanaotakiwa kuwashughulikia na kukosekana kwa ujasiri wa kuwashughulikia.
Dk. Mengi alibainisha kuwa wala rushwa wakubwa hapa nchini wako wanne na wanafahamika lakini kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo kuogopwa, wameendelea kutafuna mali ya umma bila woga wowote.
Alisema ripoti ya hivi karibuni ya masuala ya rushwa iliyotolewa na Shirika la Transparence International, imeonyesha kuwa Tanzania imeshika nafasi ya 14 kwa rushwa, hali ambayo inatisha.
Alisema matokeo ya rushwa ni mabaya kwa watu maskini kwanini wizi wa kumwibia mvuja jasho.
Mengi alisema wapo wanaosema kuwa yeye (Mengi), si mwathirikawa rushwa lakini ukweli ni kwamba alipoteza miradi mikubwa miwili kutokana na kukataa kutoa rushwa.
“Sitataja kuwa miradi yangu ilipotea katika awamu ipi ya serikali, lakini sijakata tamaa na sitaogopa nitaendelea kuzungumzia na kupambana na rushwa,” alisema.
Alisema haiwezekani kuendesha nchi kwa misingi ya rushwa, hivyo ifike mahali Taifa likubali kutengana nayo na kuwatenga wala rushwa wakubwa na wadogo, lakini kuendelea kuwakumbatia Taifa litaanguka.
Alisema Taifa linakabiliwa na tatizo la uwapo wa watu wasiofahamu kitu kujinadi kuwa ndiyo wanafahamu na kuhusika katika maamuzi ya kupanga kodi kwa wafanyabiashara.
Alisema kwa sasa anafanya sala Taifa lisifike mahali mafisadi kutawala na kuachwa wafanye watakavyo.
Aidha, alisema kuna uhusiano mkubwa kati ya wala rushwa wakubwa na mtandao wa biashara ya dawa za kulevya.
Alisema biashara ya dawa za kulevya inakua na vijana ndiyo wanatumika katika biashara hiyo.
“Huwezi kutenganisha biashara ya dawa za kulevya na wala rushwa wakubwa, hawa ndiyo wafanyabiashara wa dawa za kulevya, wanawatumia vijana kufanikisha biashara zao,” alisema.
“Vijana na wasanii wetu wanatumika katika biashara hii, waliokamatwa Afrika Kusini si rahisi wawe na kiasi hicho cha fedha, bila ufadhili wa wala rushwa wakubwa, aliyewatuma si mtu mdogo bali mla rushwa mkubwa,” alisema Dk. Mengi.
Aidha, alisema vijana ndiyo tegemeo la Taifa na wateja wa bidhaa zinazouzwa na wafanyabiashara, hivyo upo wajibu mkubwa wa kupinga kwavitendo suala la rushwa.
Alisema ni lazima Watanzania wachukue hatua za kukabiliana na wala rushwa na lawama kubwa ni kwa Watanzania ambao wanashindwa kuwaunga mkono wanaopinga rushwa.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, Godfrey Simbeye, alisema ripoti iliyozinduliwa ilijikita katika kuangalia mazingira ya uwekezajiTanzania na kubainisha mambo yanayokwamisha uendeshaji na ukuaji wa biashara nchini.
Alisema wengi wa wafanyabiashara waliohojiwa waliainisha vikwazo kuwa ni ukosefu wa umeme, kiwango chakodi, rushwa na mrundikano wa kodi.

CHANZO: NIPASHE
 
Hii ni siri iliyowazi. Inavyoelekea siku hiyo haiko mbali. Tungoje 2015 tuone.
 
Mzee Mengi binafsi huwa nakuheshimu. Ila hapa sasa heshima yangu kwako imeanza kupungua kabisa. Wacha Unafiki simama hazarani kama siku za nyuma uliposimama bila woga na kututajia Mafisadi PAPA akiwemo MANJI.

Usimumunye maneno wataje hao mafisadi unao wahisi kuwa kuna siku wanaweza kutawala nchi. Si useme tu wazi kuwa Unamzungumzia LOWASSA kwani ndie tunaona akijitahidi Misikitini na Makanisani kujisafisha ili aweze kuwa rais 2015 huku wakati ni FISADI PAPA!!
Mkuu hivi ile kesi manji aliyokuwa anamdai mengi shilingi 1 iliishaje? anaogopa kuwataja mzee!
 
Mwenyekiti wa makampuni ya IPP bwana Reginald Mengi amesema kwa hali ya kisiasa inavyoendelea ipo siku mafisadi wataongoza nchi kwa kuwa mpaka leo hawajachukuliwa hatua zozote za kuwakamata na kuwafungulia mashataka. Na serikali imekaa kimya

Najua anamaanisha wafadhili wakuu wa lowassa ambao no rostam, manji na
 
Huyu mzee mbona hata yeye anatuhuma za ufisadi alizoshushiwa na Rostam Aziz na mpaka leo hajazitolea ufafanuzi au kuzikanusha? Mimim naona hawa watu wanajuana sisi tubaki kuwatazama tu. Hapa najua ni yale yale mambo ya fisadi Papa na Fisadi Nyangumi yameingia episode 2.
 
Mengi naona ameishiwa hoja.
Mafisadi watawale mara ngapi?
Kwan hao anaowajua si watawala au aliyosema ni mapapa wa ufisadi wanainfluence gani kwenye serikali.hawaongozi?
Acha uhuni Mengi.
 
Mwenyekiti wa makampuni ya IPP bwana Reginald Mengi amesema kwa hali ya kisiasa inavyoendelea ipo siku mafisadi wataongoza nchi kwa kuwa mpaka leo hawajachukuliwa hatua zozote za kuwakamata na kuwafungulia mashataka. Na serikali imekaa kimya

Mengi amesema kweli lakini amekuwa mjanja kusema wazi. Ukweli ni kuwa nchi hii hata sasa inaongozwa na mafisadi na bado wanataka kuendelea kuongoza kwa kila hali ili kulinda maslahi yao. Si unaona wanavyozunguka makanisani, misikitini, kwa wamachinga, vyuoni na mashuleni? Hii yote ni katika harakati za kurithishana madaraka ili waliopo juu wawe na ulinzi baada ya kuondoka. Kwakuwa wana nguvu kubwa ya pesa hakuna wa kuwazuia. Wakisha waweka viongozi wa dini kwapani, vijana kwapani, wanafunzi kwapani, wakulima kwapani na wafanya biashara ambao kwa sehemu kubwa ndio walio uongozini kwa sasa unategemea nini? Well said Mengi na ni wazi umeshajiongezea maadui kwa maneno yako hayo ya kweli!
 
Mafisadi tayari wanaongoza labda anazungumzia sijaua anazungumzia mafisadi wanamna gani au wale papa, mbona lakini na hao wanaoongoza ni mafisadi papa pia
 
Back
Top Bottom