Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, amesema ikiwa mafisadi hawatadhibitiwa, iko hatari wakajiimarisha kufikia hatua ya kuiongoza nchi siku zijazo.
Wala rushwa wakubwa ni kina nani na wako wangapi? Ukiniuliza mimi nitakwambia hawazidi wanne, wanafahamika ila sitawataja kwa leo, alibainisha.
Alisema rushwa kubwa ipo nchini na tuendako ana wasiwasi kuwa wala rushwa wakubwa ndiyo watatawala nchi kupitia matakwa yao kwa nchi kuongozwa na kutawaliwa na watu wasioonekana wala kujulikana.
Ni watu wenye nguvu wanajipenyeza hadi katika vyombo vya dola, mtu anaweza kupoteza kazi kwa uamuzi wao, alisema.
Chanzo: Nipashe