Redio zetu bado zinarusha matangazo ya vifo ili iweje?

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,055
Nimeshangaa kusikia Radio One bado inaendelea na kipindi cha matangazo ya vifo hadi leo.. Kipindi kilichoanza zaidi ya miaka 20 iliyopita..

Naambiwa hii ilianza na Radio Tanzania (sasa TBC) enzi hizo na ilisaidia sana kufikisha taarifa za misiba kwa walio mbali..

Kiukweli sioni tija yake. Labda mnieleweshe.. Kwa zamani sawa inaeleweka sekta ya mawasiliano na usambazaji taarifa ulitegemea zaidi radio na barua za mkono kwa mkono.. Lakini zama hizi?

Ningeelewa kama redio hizi zingeboresha kipindi hicho kwa kukaribisha ndugu, jamaa na marafiki kuenzi wapendwa wao kama kumbukumbu (death anniversaries)..

Au ndio old is gold? Pengine ni culture ya redio hizi kongwe inatunzwa idumu?
 
Natumaini lengo ni kufikisha taarifa kwa wale ndugu wasio na mawasiliano na ndugu zao...
Nakumbuka hata ukoo wetu ulishawai kurusha tangazo miaka kama miwili hivi imepita lengo lilikuwa wapate taarifa wale ndugu waliiondoka kwenye familia bila taarifa na hawajulikani wapo wapi.

Sasa sijajua malengo ya wengine..
 
Sijui mleta Post anasemaje?
 
Matangazo ya vifo lengo ni habari ya msiba kuwafikia ndugu,jamaa na marafiki,

Mfiwa/Wafiwa wanaweza wasiwe na mawasiliano ya kila wanayetaka habari zimfikie popote walipo,pia unaweza kua na mawasiliano ya mtu ila akawa hayupo hewani kwa muda mrefu kwa sababu mbali mbali,

Sina uhakika kama matangazo ya vifo hulipiwa ila kama wahusika hulipia basi wacha Radio ziendelee tu na huo utaratibu coz sidhani kama kuna mtu ana athirika na utaratibu huo,

Hata wewe mleta mada siku umeme ukikatika utaenda pia Dukani kununua Mshumaa.
 
Nimeshangaa kusikia Radio One bado inaendelea na kipindi cha matangazo ya vifo hadi leo.. Kipindi kilichoanza zaidi ya miaka 20 iliyopita..

Naambiwa hii ilianza na Radio Tanzania (sasa TBC) enzi hizo na ilisaidia sana kufikisha taarifa za misiba kwa walio mbali..

Kiukweli sioni tija yake. Labda mnieleweshe.. Kwa zamani sawa inaeleweka sekta ya mawasiliano na usambazaji taarifa ulitegemea zaidi radio na barua za mkono kwa mkono.. Lakini zama hizi?

Ningeelewa kama redio hizi zingeboresha kipindi hicho kwa kukaribisha ndugu, jamaa na marafiki kuenzi wapendwa wao kama kumbukumbu (death anniversaries)..

Au ndio old is gold? Pengine ni culture ya redio hizi kongwe inatunzwa idumu?

Si bora hata wanaotangaza matangazo ya vifo angalau hilo ni jambo la muhimu. Kuna wale wanaotuma salamu mi ndio hua siwaelewi kabisa! Mtu anapiga simu redioni eti "napenda kutuma salamu kwa mpenzi wangu Edita" yuko wapi..? "Huyu hapa niko nae"
 
Alafu 90% ya matangazo ya vifo Radio One yanahusu ndugu zangu wa mkoa wa Kilimanjaro,,, sijui ni kwann!????

Fatilieni hili mtanambia 😀
 
Nimeshangaa kusikia Radio One bado inaendelea na kipindi cha matangazo ya vifo hadi leo.. Kipindi kilichoanza zaidi ya miaka 20 iliyopita..

Naambiwa hii ilianza na Radio Tanzania (sasa TBC) enzi hizo na ilisaidia sana kufikisha taarifa za misiba kwa walio mbali..

Kiukweli sioni tija yake. Labda mnieleweshe.. Kwa zamani sawa inaeleweka sekta ya mawasiliano na usambazaji taarifa ulitegemea zaidi radio na barua za mkono kwa mkono.. Lakini zama hizi?

Ningeelewa kama redio hizi zingeboresha kipindi hicho kwa kukaribisha ndugu, jamaa na marafiki kuenzi wapendwa wao kama kumbukumbu (death anniversaries)..

Au ndio old is gold? Pengine ni culture ya redio hizi kongwe inatunzwa idumu?
Matangazo ya vifo Ni matangazo ya biashara kwa sababu yanalipiwa. Hivyo kuwepo au kutokuwepo kwake kunategemeana na maamuzi ya soko , hapa naongelea wale wanaohitaji na walio tayari kulipia huduma hiyo , ambapo Ni mwendawazimu peke yake anaeweza kukataa pesa ya mteja kwa kigezo kwamba huduma imepitwa na wakati.
Pengine wanaokwenda kutuma matangazo haya ndio wako nyuma ya wakati , adhawaiz ndo wanaopaswa kujibu swali hili , na Wala si vituo vya redio..
 
Watu wasipopeleka matangazo ya vifo, matangazo hayo hayatakuwepo.
TBC yalikufa matangazo sababu watu walikua hawapeleki Tena.
Na hata ivo, matangazo ya vifo ya radio one 90% wanaotangazwa/tangaziwa Ni wachagga. Ikiwa na maana wachagga wamebak na utamadun huo, na lengo Ni kuhabarisha umma juu ya kifo Cha mhusika ili wengi wajue
 
Si bora hata wanaotangaza matangazo ya vifo angalau hilo ni jambo la muhimu. Kuna wale wanaotuma salamu mi ndio hua siwaelewi kabisa! Mtu anapiga simu redioni eti "napenda kutuma salamu kwa mpenzi wangu Edita" yuko wapi..? "Huyu hapa niko nae"
Ndo hivyo watu wanataka tufate uvumbuzi wa zamani na kizazi cha zamani ukiwaletea kipya wanasema unataka kutuua labda vitoke vipaji nje ndo vije kutumika huku kwa kulazimisha kwa high class na wale wengi low class tunaiga kwa shingo upande Kama simu zilivyokuja.
 
Back
Top Bottom