Matangazo ya Kamari kwenye radio zetu: Waziri mwenye dhamana chukua hatua

Kinoamiguu

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
10,526
13,013
Habari za muda wadau.

Mimi ni mdau na msikilizaji wa hizi radio za masafa marefu fm radios
Nasikiliza baadhi ya vipindi kwani vipindi vyao vingi havina maudhui niyapendayo ya habari.
Utafiti wangu nimegundua kwamba katika vipindi hivi vichache ninavyosikiliza matangazo ya KAMARI NI MENGI SANA SANA.

Matangazo yenye sifa kama yale ya tatu mzuka yameongezeka sana.
mfano radio wasafi kile kipindi cha michezo ni kamari tuu mwanzo mwisho
Radio one mpaka saa saba usiku.
kama taifa hali haiwezi kuachwa hivi kwasababu

1. Kamari itawazuia watu kutofanya kazi kwa bidii, wataamini pesa ni lelemama.
2. Kuhamasisha wizi nk

Kwakuwa radio hizi husikilizwa na makundi yote katika jamii, uwekwe utaratibu ili kulinda jamii hasa watoto wasiamini kwamba maisha ni kubeti tu na kuacha kuamini kwenye kazi.

Waziri mwenye dhamana hili lipo ndani yako.

Tulishaliweza huko nyuma na sasa tuweze tena

Asante
 
Vijana wengi wa kileo ukiwatazama vichwani wana mvi kutokana na kutegemea kupata hela kwa style hii..

Hela ya kamari inatia stress maana hujaipata tayari matatizo yako yameshaisha ukiikosa unajiongezea tena mawazo kuwaza mbona sishindi nina gundu au nimelogwa?
 
Yani wananitesa sana wakitangaza kamali nabadili na uko nao ivo ivo wanaibia watu tu
 
Habari za muda wadau.

Mimi ni mdau na msikilizaji wa hizi radio za masafa marefu fm radios
Nasikiliza baadhi ya vipindi kwani vipindi vyao vingi havina maudhui niyapendayo ya habari.
Utafiti wangu nimegundua kwamba katika vipindi hivi vichache ninavyosikiliza matangazo ya KAMARI NI MENGI SANA SANA.

Matangazo yenye sifa kama yale ya tatu mzuka yameongezeka sana.
mfano radio wasafi kile kipindi cha michezo ni kamari tuu mwanzo mwisho
Radio one mpaka saa saba usiku.
kama taifa hali haiwezi kuachwa hivi kwasababu

1. Kamari itawazuia watu kutofanya kazi kwa bidii, wataamini pesa ni lelemama.
2. Kuhamasisha wizi nk

Kwakuwa radio hizi husikilizwa na makundi yote katika jamii, uwekwe utaratibu ili kulinda jamii hasa watoto wasiamini kwamba maisha ni kubeti tu na kuacha kuamini kwenye kazi.

Waziri mwenye dhamana hili lipo ndani yako.

Tulishaliweza huko nyuma na sasa tuweze tena

Asante
Yaani inasikitisha sana, wizara husika iko kimya wakati Watanzania wanadanganywa kuwa zipo pesa za bure. Bahati mbaya sana Watanzania nao wanaamini na kushiriki kwa wingi kwenye hizo kamari.

Vv
 
Media inafuata nini raia/wasikilizaji wanataka kusikia/kuona .

Kuenea kwa matangazo ya betting company sio kosa la media, hizo kampuni zinalipa pesa nzuri tuu, ni moja ya vyanzo vya mapato kwa wamiliki wa vituo vya habari.

Suala la kuelimisha jamii Vs Mapato
hilo ni controversal......
 
ila watanzania ni wapuuzi😄 unaambiwa chota mihela wakati huo unaambiwa cheza kadri uwezavyo.
wasikilizaji wako 1 million, nusu yao wakicheza buku buku tu tayari ni 500M pesa ya bure kabisa ukiweka kodi ya serikali 18% the end justifies the means!
 
Back
Top Bottom