REDET: Wabunge 143 hawachaguliki uchaguzi 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

REDET: Wabunge 143 hawachaguliki uchaguzi 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Apr 28, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  WABUNGE 143 kati ya 232 wanaotoka katika majimbo ya uchaguzi hawachaguliki, hivyo ni vigumu kurejea bungeni baada ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (Redet).

  Utafiti wa taasisi hiyo iliyo chini ya Idara ya Sayansi ya Siasa ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam unaonyesha asilimia 61.7 ya wabunge wa bunge la sasa hawatachaguliwa tena.

  Wakijibu swali lililoulizwa katika utafiti huo kuhusu uchaguzi mkuu ujao kama watachagua mbunge wao aliyepo sasa, asilimia 39.3 ya wananchi ndio waliosema watachagua mbunge wa sasa, wakati asilimia 61.7 ya wote waliyohojiwa walisema hawatamchagua mbunge wa sasa.

  Utafiti huo ambao ulifanywa kwa ajili ya kutafuta maoni ya wananchi kuhusu uchaguzi mkuu ujao, ulishirkisha wilaya 52 na kuhoji watu 2600 ikiwa ni watu 50 kutoka kila wilaya.

  Akisoma matokeo ya utafiti huo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Dk Bernadeta Killian alisema kuwa waliyohojiwa pia walikuwa na maoni tofauti.

  Alisema asilimia 38.3 walisema watachagua mgombea mwingine wa chama chake, asilimia 8.7walisema watachagua mgombea wa chama kingine, asilimia12.4 walisema hawajaamua bado na asilimia 2.9 walitoa majibu mengine tofauti.

  Kutokana na hali hiyo, mtafiti huyo wa Redet alisema kuwa karibu asilimia 62 ya wabunge wa sasa hawatachaguliwa tena majimboni mwao.

  Utafiti huo pia unaonyesha kuwa Rais Kikwete na chama chake cha CCM wanaendelea kushika nafasi ya juu kutokana na maoni ya wananchi hivyo kuashiria kuwa CCM itarejesha wabunge wengi na mgombea huyo wa urais atashinda kwa kishindo.

  Kwa mujibu wa utafiti huo, waliohojiwa walitakiwa kutoa maoni yao katika swali lililoulizwa kuwa mwezi Oktoba mwaka huu utafanyika Uchaguzi Mkuu, "kama uchaguzi huo ungefanyika leo wewe ungemchagua mgombea wa chama gani?"

  Asilimia 77.2 (1997) ya waliohojiwa walisema watamchagua mgombea wa urais wa CCM, asilimia 9.2 (237) ikisema itamchagua mgombea wa CUF, asilimia 4.2 (109) mgombea wa Chadema, wakati asilimia 8.7 walisema bado hawajaamua ni mgombea wa chama gani watampigia kura.

  Kwa upande wa wabunge, inaonyesha CCM itapata upinzani mkali katika baadhi ya maeneo kwa kuwa utafiti huo unaonyesha asilimia kushuka ikilinganishwa na ya urais. Asilimia 68 ya waliohojiwa walisema watachagua mgombea ubunge wa chama hicho.

  Asilimia 10.2 watachagua mgombea CUF na asilimia 8.6 watachagua mgombea wa Chadema wakati vyama vingine vikitajwa kwa idadi ndogo sana na matokeo hayo yamekuwa yakijirudia kwa asilimia hizo hata kwa madiwani.

  Kuhusu uchaguzi wa urais, wahojiwa walitakiwa kumtaja mtu mmoja ambaye wangependa awe rais. Rais wa sasa, Jakaya Mrisho Kikwete ameendelea kuwabwanga wengine waliotajwa kwa kujikusanyia asilimia 66.9.

  Kikwete amefuatiwa kwa mbali na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF aliyepata asilimia 6.7, Freeman Mbowe (3.1) na Dk. Asha Rose Migiro asilimia 0.7.

  Wengine ni Salim Ahmed Salim asilimia 0.7, Dk Willibrod Slaa asilimia 0.6, Zitto Kabwe asilimia 0.6, Seif Sharrif Hamad asilimia 0.5, Dk. Ghalib Bilali asilimia 0.5 na Balozi Ali Karume 0.3.

  Aidha, utafiti huo ulihoji kuhusu utendaji kazi wa Rais Kikwete katika kipindi cha miaka mitano na kuonyesha kuwa asilimia 49 ya waliyohojiwa wanaridhishwa sana na utendaji wake, asilimia 36.5 wanaridhishwa kiasi wakati wasioridhika kabisa ni asilimia 13.1 na wasiojua kitu kuhusu suala hilo ni asilimia 1.1

  Takwimu hizi zikilinganishwa na tafiti zilizopita za Redet inaonekana kiwango cha kuridhika na utendaji kazi wa Rais Kikwete miongoni mwa wananchi kimeanza kupanda. Oktoba 2009 ilikuwa asilimia 67.4, Oktoba 2007 ilikuwa asilimia 44.4, Novemba 2008 ilikuwa asilimia 39.5 na Machi 2010 ilikuwa asilimia 49.3.

  Kuhusu imani ya wananchi kuhusu utendaji kazi wa viongozi na serikali, utafiti huo unaonyesha kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewabwaga viongozi wengine akiwemo Rais Kikwete.

  Kwa mijibu wa utafiti huo, Pinda anaongoza kwa asilimia 61.2 , akifuatiwa na Rais Kikwete mwenye asilimia 58.8 (1528).

  Wengine ni Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein aliyepata asilimia 46.8, mawaziri (25.7) madiwani (44.5) na wabunge ni 38.7 .

  From: Mwananchi Newspaper
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  REDET you are quite wrong. Hawa 143 ni wachache mno, nafikiri the figure should be more than 200. Kwani mchango gani Wabunge, hasa wale wa CCm, wameutoa kuwaendeleza wananchi wao? hawatembelei majimbo yao, na wakilazimika kutembelea kutokana na ziara za Jk au Pinda, basu huzomewa wanapopanda majukwaani.
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Hawa REDET huwa wanamuhoji nani hawa, mbona pita pita zangu mjini sijawahi kutana na watu kama hawa wakanihoji?
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  They just cook up figures, that's all!
   
 5. M

  Msindima JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2010
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135

  Hata mimi nahisi hivyo,nini haswa lengo lao? maana nimejaribu kufikiri na mpaka sasa sijaelewa lengo lao ni nini haswa.
   
 6. Shoo Gap

  Shoo Gap JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 236
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Utafiti unahitaji kuwa na sample, huwezi kulazimisha wewe uingie kwenye sample ya utafiti fulani. Ukisoma kwa makini utagundua kuwa hawakupita Wilaya zote, yumkini hata Wilaya unayoishi au ulizowahi kutembelea hazipo katika sample yao. Its just a probability.
   
 7. K

  Keil JF-Expert Member

  #7
  Apr 28, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Walitumia njia gani kupata hizo wilaya 52 ambazo wamezipitia? Siasa za Tanzania zimekaa kikanda zaidi kwa hiyo mtafiti anatakiwa kuwa makini na namna anavyochukua sample yake.

  Je, hao waliowahoji, ni wangapi wanachama/wapenzi/mashabiki wa CCM? Unaweza kukuta asilimia kubwa ya hao waliowahoji ni wapenzi na wanachama wa CCM.

  Kitu kingine ambacho REDET walitakiwa kukichunguza, kungekuwa na swali la ziada (follow-up question), kwa kufafanua kwanini wananchi hawataki ama wanataka kuwachagua wabunge waliopo mjengoni sasa hivi? Hili swali linge-make sense, maana kama Mbunge ameshindwa kutimiza ahadi zake kwa wapiga kura kulingana na Ilani ya Chama chake, kwanini watu waendelee kuchagua mbunge mwingine wa chama kile kile kilichoshindwa kutimiza ahadi zake?

  Mwisho kabisa, hivi watanzania huwa tunachagua mtu ama chama? Maana the way maswali ya REDET yalivyokuwa structured ni kana kwamba wanashindanisha vyama na siyo hoja za wagombea.
   
 8. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #8
  Apr 28, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama walivyofanya mwaka 2005, wamenza tena kufanya utafiti wao wa kipuuzi. kuna issues kibao hazina fedha za kufanyia utafiti. Hawa wanafanya utafiti wa kuwapumbaza watanzania ili mikono yao iende kinywani. Shame, shame shame on you REDET.
   
 9. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #9
  Apr 28, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nikama kupima oil wakati election ni kushusha engine.... It would be nice to have a newer generation with a 21st Century outlook (as if we will even see that..election ya 2020 na 2025 ndio labda tutaona hayo inshallah..
   
 10. jamadari

  jamadari JF-Expert Member

  #10
  Apr 28, 2010
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 295
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  [​IMG] Wananchi waapa hawatawarudisha
  [​IMG] Rais Kikwete azidi kuchanja mbuga
  [​IMG] Asilimia 77 wadai watampigia kura  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete


  Asilimia 62 ya wabunge waliopo hivi sasa madarakani, wako shakani kuchaguliwa tena katika Uchaguzi Mkuu ujao kutokana na asilimia kubwa ya wananchi kutoridhika na utendaji wao wa kazi.

  Matokeo ya utafiti uliofanywa na Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (Redet) katika wilaya 52 za mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na Zanzibar, yameonyesha kuwa asilimia 61.7 ya wananchi waliohojiwa, walisema hawatamchagua mbunge aliyepo madarakani hivi sasa.


  Utafiti huo ulifanyika Machi, mwaka huu na matokeo yake yalitangazwa jana na Mtafiti Mkuu wa Redet, Dk. Bernadeta Killian, alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.


  Alisema wananchi waliohojiwa kuhusu kutomchagua mbunge wa sasa, walitoa maoni tofauti.


  Alisema wakati asilimia 38.3 walisema watamchagua mgombea mwingine wa chama chake, asilimia 8.7, walisema watachagua mgombea wa chama kingine, asilimia 12.4 hawajaamua bado na asilimia 2.9 walitoa majibu mengineyo.


  “
  Hii inaashiria kwamba, takribani asilimia 62 ya wabunge wa sasa wanaweza wasichaguliwe hapo Oktoba,” alisema Dk. Killian.

  Alisema ukiachilia mbali wananchi hao, asilimia 39 tu ya wahojiwa wote ndio waliosema watamchagua mbunge wa sasa.


  Mtafiti Mkuu huyo alisema utafiti huo pia umeonyesha kuwa asilimia 85.8 ya wananchi waliohojiwa, wameridhika na utendaji kazi wa Rais Kikwete katika kipindi cha takriban miaka mitano ya utawala wake.


  Alisema idadi hiyo ni ya wananchi waliohojiwa, ambapo asilimia 49.3 walisema wanaridhishwa sana wakati asilimia 36.5 walisema wanaridhika kiasi, huku asilimia 13.1 wakisema hawaridhiki.


  “
  Ukijumlisha wale waliohojiwa waliosema wanaridhika sana na wanaridhika kiasi, utaona kwamba asilimia 85.8 ya wahojiwa wote wanaridhishwa na utawala wa Rais Kikwete,” alisema Dk. Killian.

  Alisema nusu ya wahojiwa waliosema wanaridhika sana ni wanawake, ambao ni asilimia 51.4, huku wanaume wakiwa ni asilimia 48.6.


  Dk. Killian kwa kulinganisha na takwimu kutoka tafiti za Redet zilizopita, inaonekana kwamba kiwango cha kuridhika na utendaji kazi wa Rais Kikwete miongoni mwa wananchi, kimeanza kupanda kutoka asilimia 67.4 (mwaka 2006) hadi asilimia 49 katika utafiti uliofanywa Machi, mwaka huu.


  Alisema katika utafiti huo, wahojiwa pia walitakiwa kutoa maoni yao kuhusu uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani.


  Dk. Killian alisema asilimia 77.2 ya wahojiwa wote walisema watamchagua mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wabunge (68.0%) na madiwani (68.2%) na kufuatiwa na Chama cha Wananchi (CUF), ambapo asilimia 9.2 walisema watamchagua mgombea urais wa chama hicho, wabunge (10.2%) na madiwani (10.6%), wakati asilimia 4.2 walisema watamchagua mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wabunge (8.6%) na madiwani (7.7%).


  Alisema vyama vingine vilipata idadi ndogo sana ya wahojiwa, ambapo asilimia 0.2 walisema watamchagua mgombea wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), wabunge (0.2%) na madiwani (0.2%), NCCR-Mageuzi (urais 0.2%), wabunge (0.3%) na madiwani (0.2%); na Chama Cha Jamii (CCJ) (urais 0.0%), wabunge (0.1%) na madiwani (0.1%).


  Utafiti huo pia umeonyesha kuwa idadi kubwa ya watanzania hawaridhishwi na utendaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na waliosema kuwa hakitimizi ahadi ni asilimia (18.7) , viongozi wake hawaaminiki ni wabovu (9.4) , viongozi wake ni wala rushwa (12.1), kina migogoro (2.2), hakina sera na programu nzuri (1.8).


  Dk. Killian alisema wahojiwa wanaosema wana imani sana na wale wanaosema wana imani kiasi, Rais Kikwete anaongoza kwa kupata asilimia 89.7 akifuatiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (83.9%), wakati Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein (79.9).


  Alisema mawaziri wamepata kiwango cha chini cha wahojiwa wanaosema wana imani sana nao cha asilimia (25).


  Kuhusu uchaguzi wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, wahojiwa waliulizwa kutaja jina la mtu mmoja, ambaye wangependa kumchagua ili awe Rais wa Tanzania, kwa upande wa vyama vya upinzani, Mtafiti Mkuu huyo wa Redet alisema Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ndiye anamfuatia Rais Kikwete mwenye asilimia 66.9 kwa kuwa na asilimia (6.7) ya kukubalika akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe asilimia (3.1).


  Dk. Killian alisema majina mengine yaliyotajwa na waliohojiwa ni Dk. Asha-Rose Migiro (0.7), Dk. Salim Ahmed Salim (0.7), Dk. Wilbroad Slaa (0.6) na Zitto Kabwe (0.6), Maalim Seif Shariff Hamad (0.5), Dk. Gharib Bilal (0.5), Balozi Ali Karume (0.3), Augustine Mrema (0.1), John Malecela (0.1), Getrude Mongela (0.1) na Dk. Ali Mohamed Shein (0.1).


  Alisema wilaya, ambazo zina idadi kubwa ya watu wasioridhika na utendaji kazi wa Rais Kikwete ni Tandahimba (64), Kiteto (32), Ilala (30), Lindi vijijini (28) , Dodoma mjini (28), Karatu (28), Kasulu (29), Unguja Kaskazini A (26), Musoma vijini (26), Singida mjini (24) Tarime (24), Lushoto 22 na Biharamulo (22).


  Kuhusu maridhiano yaliyofikiwa kati ya Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad visiwani humo, utafiti unaonyesha kuwa asilimia 63 ya wananchi Zanzibar wanayaunga mkono wakati asilimia (43) ya wananchi wa bara ndio wanayaunga mkono.


  Alisema asilimia 8.8 ya wananchi wa Zanzibar walisema hawajui maridhiano hayo yanahusu kitu gani na asilimia 19 ya wabara nao walisema hawajui maridhiano hayo yanahusu nini.


  Alisema kati ya vyama vyote vya siasa, CUF na Chadema tu ndio vinaonekana kutoa ushindani katika uchaguzi mkuu hasa katika uchaguzi wa wabunge na madiwani kuliko ule wa urais.


  Dk. Kilian alisema ukusanyaji maoni ya utafiti huo ulifanyika katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani na uchambuzi ulichukuliwa kwa kutumia ngazi tatu.


  Alitaja ngazi hizo kuwa ni wilaya, vijiji/mitaa na wahojiwa na kwamba katika kila ngazi sampuli ilipatikana kwa kutumia mtindo wa sampuli nasibu  CHANZO: NIPASHE
   
 11. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #11
  Apr 28, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kinachonistaajabisha ni kwamba wakati inaonyesha kwamba karibu 2/3 ya Wabunge wana dalili ya kutoswa kwa Wananchi kutoridhishwa na utendaji wao lakini wanamfagilia Kikwete! Sijui kwa lipi alilolifanya hadi astahili kubaki madarakani. Maana kama 2/3 ya wabunge walishindwa kazi katika awamu inayokwisha basi Kikwete pia alishindwa kazi kama kuna lolote alilolifanya hebu tuambiwe tulifahamu.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Apr 28, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Mara nyingi nabishana na watu wanaosema kuwa vijijini watu wanahitaji elimu zaidi ili wapige kura kutoichagua CCM; lakini nimekuwa nikielezea kuwa hati hivi sasa ukiondoa Moshi Mjini majimbo mengine yote yanayoshikiliwa na wapinzani ni ya vijijini! Na kama REDET inaweza kudokeza ukweli angalia hili:

  Ukiondoa Ilala, Dodoma Mjini na Singida mjini.. ni maeneo ya vijijini ndio wamemshtukia Kikwete!!!
   
 13. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #13
  Apr 28, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  [​IMG] Wananchi waapa hawatawarudisha
  [​IMG] Rais Kikwete azidi kuchanja mbuga
  [​IMG] Asilimia 77 wadai watampigia kura  [​IMG]huyu jamaa kuna uwezekano anawatumia hawa redet, maana wamejaa mizengwe zaidi, wanajaribu kutulisha upumbavu watanzania, tuwe makini na kampeni 'vishoka'
   
 14. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nimegundua kumbe tatizo siyo kukusanya data ni wanaotoa Data analysis wana ajenda zao tayari kichwani, hebu angalia hii........
  Wanaoridhishwa 49.3%
  Wanaoridhika kiasi 36.5%...this is ambiguous hypothesis....
  Wasioridhika 13.1%

  Nawauliza REDET; hawa mnaosema wameridhika kiasi mmekipimaje hicho kiasi, je kama ni kiasi cha karibu na kutoridhishwa kabisa inakuwaje basi mmekichanganya na wanaoridhika mkaacha kuchanganya na wasioridhishwa kabisa? hii kama si siasa ni kitu gani, kama REDET mnafanya hivyo kuwafurahisha mabosi wenu basi hakuna haja ya kutoa matokeo yenu kwenye public wapelekeeni huko huko maofisini.

  Ninachowashauri REDET wanapotoa matokeo ya tafiti zao kwenye public wawe wakweli wasifikiri wote ni vilaza katika research huwezi kusema kwa vile haya mayai ni mabovu kidogo nayachanganya na mazima, heri kutofanya utafiti kuliko kupotosha matokeo ya utafiti, ni bora REDET mmebobea kwenye tafiti za siasa kama mngekuwa kwenye medical research mngeshaua watu.
   
 15. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #15
  Apr 29, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Very funny, research imefanyiwa ofsini kwao tu
  Is it true kuwa wana ukweli wowote????
   
 16. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #16
  Apr 29, 2010
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wangetueleza waliotoa maoni kwa njia gani? simu, internet, tv viewers, radio listeners au wapita njia?
  Au wananchi wa rika gani? watoto, vijana au wazee?
   
 17. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #17
  Apr 29, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nyie hamuwafahamu hawa red heart? (REDET) wajinga hawa na hivi vi research vyao vinavyofanyika karibu na chaguzi zote za dunia ya danganyika ili kutayarisha njia ya kuibia!
  Ni wasomi wajinga hawa. Utadhani hawakwenda shule vile.
  Mbona hata hivyo sijawahi kuwaona kwenye anga zangu? Twataka data zao za research ziwe wazi wazi wasizitoe kijuu juu hivi kama vile wanawapa wajinga wenzao.
   
Loading...