Elections 2010 REDET & Synovate hamtaweza kuzuia mabadiliko...

Nawahurumia hawa Synovate watakuja kuaibika zaidi. Kuna ripoti kwamba wamewahi kufanya kazi (assignment) fulani -- ya kifisadi -- na kitengo cha Ikulu cha Salva. Hilo bomu linakuja maana walikuwa wanasubiriwa watoe hii. I pity them!!!


Nami niliwahi kusikia kitu kama hicho. Lakini kama kawaida hakuna chombo chochote cha dola kitashughulikia ufisadi huo ktk Ikulu.
 
Toka uchaguzi wa vyama vingi uanze 1992 sijaona mwamuko wa kisiasa kama ninaoshuhudia leo, hii ni ishara ya mabadiliko makubwa kutokea siku ya kupiga kura ambapo wananchi wote watashirikishwa kufanya utafiti tofauti na utafiti wa REDET na Synovate unaowahusisha watu 2000 tu. People will prove REDET and Synovate wrong na aibu itaenda kwa mashirika hayo. Nina kila sababu:

Kukubalika kwa vyama vya upinzani hasa vijijini tofauti na miaka ya nyuma ambapo vilikuwa vinajulikana mijini tu, wananchi kuanza kuwakataa waziwazi wabunge wasiowataka ni ishara kubwa kuwa elimu ya uraia imefika kwao.

Vyama vya upinzani vilianza maandalizi ya uchaguzi mapema refer Operation Sangara ya Chadema na Operation Zinduka ya CUF. Kwa mara ya kwanza upinzani umeweka wagombea ubunge karibu majimbo yote hivyo kuonyesha ukaribu wake kwa wananchi.

Kuweka wagombea wanaouzika hasa ujio wa Dr. Slaa ulivyowashangaza wengi hata CCM hawakutarajia kwa hiyo hawakujiandaa kupata upinzani mkubwa. Imesababisha
- CCM kuanza kutumia mbinu chafu badala ya kutangaza sera mfano kuzungumzia maisha ya ndani ya Slaa.
- CCM kulitumia jeshi la wananchi badala ya Polisi ni dhahiri wameona nguvu ya upinzani ni kubwa.

Kwa mara ya kwanza viongozi ndani ya chama tawala kupinga wazi tena mbele ya vyombo vya habari utawala na uongozi wa Kikwete eg
- Tamko la MNF-kushindwa kuchukua maamuzi magumu
- Kutengwa kwa Kikwete na wanamtandao waliomuingiza ikulu
- waasisi wa chama hicho kujitenga na kampeni na kuiachia familia ya Kikwete.

Udhaifu wa kiutendaji wa Kikwete kwa miaka mitano na udhaifu wa kiafya(inajieleza).

CCM is not united again
- makundi yanayoendelea chini kwa chini na mengine waziwazi.
- maandalizi hafifu ya kura ya maoni ya CCM imebomoa badala ya kujenga chama
- wanahujumiana wenyewe kwa wenyewe

Kuvuja mapema kwa siri za wizi wa kura, mbinu gani kina nani wako wapi tofauti na miaka iliyopita, baadhi ya TISS kuhusishwa.

Jamii na wanaharakati wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na viongozi wa dini kuhamasisha waumini wao kujitokeza kupiga kura na baadhi ya ibada kubadilishwa.
- mfano makanisa ya Kakobe kusali Jumamosi badala ya Jumapili
- baadhi ya makanisa kufupisha ibada
- baadhi ya wanaharakati kutumika kujibu matamko refer Ananilea Nkya kumjibu Nsimbo.

Kama ilivyozoeleka wapinzani kuanzisha fujo safari hii CCM ndiyo imekuwa kinara wa kuanzisha vurugu(matukio ya hivi karibuni).

Kikwete kuzikataa hadharani kura za wafanyakazi na ujio wa kizazi kipya ambacho hakikupiga kura mwaka 1995 ni ishara kitafanya mabadiliko yatokee.

Pamoja na mambo mengine, haya ni baadhi ya mambo kwa mawazo yangu na uzoefu wangu kwenye mambo ya siasa huenda mwaka huu kukatokea mabadiliko makubwa Tanzania.

Angalizo: Mabadiliko hayo yanaweza kutokea kwa njia ya sanduku la kura endapo NEC watataka iwe hivyo au madadiliko hasi kwa njia mbadala.

Naomba kutoa hoja.


Ukweli ni kuwa tayari wameshawashangaza kutokana na hali halisi walio ikuta huko ambapo hawakutegemea kuona Vuguvugu la UKOMBOZI WA Slaa halina makali kama walitegemea.............
 
61 + 16 + 5 = 82
100 - 82 = 18


Sasa hata kama 18% watagawana wengine, ni bora zingeonyeshwa, kwani ni nyingi mno kuzipuuzia.

Ripoti yenye inasema hivi:

JK 61%
Slaa 16%
Lipumba 5%
13% hawakujibu
5% wagombea wengine
 
Nimechoshwa na matokeo ya uongo wanayotoa hawa vibaraka, nadhani hawatambui kuwa mabadiliko ni kama mvua, kama inanyesha inanyesha..Hta wakimpa 100%...mabadiliko yapo njiani...tunakuja na watalokota benyewe kwenye nyavu....
 
Kazi ya kuchakachua Matokeo imekuwa ikifanyika bila ya watu kuwa makini hata kidogo. Kwanza kabisa asilimia za JK alizopewa na REDET zimepungua kutoka 71% hadi 61%. Hili ni anguko la asilimia 10% nzima. Na kufanya tofauti ya matokeo ya kampuni mbili tofauti kuwa ni asilimia 14!!!!!!!!

Dr. Slaa amepanda kwa asilimia 4 kutoka asilimia 12.1 alizopewa na REDET hadi 16% za SYNOVATE. Haya ni mabadiliko ya karibu asilimia 25 hivi.

Prof. Lipumba amezidi kuporomoka kutoka asilimia 10 alizopewa na REDET hadi asilimia 5 za SYNOVATE. Hili ni anguko la asilimia tano nzima au 50% kwa vipimo vya kampuni mawili ya polls.

Hatujaelezwa sampling error ni kiasi gani katika polling zote hizo mbili.

Huko Kenya, SYNOVATE haijawahi kusema kuna "UNDECIDED VOTERS" na hii asilimia 18% kudai ni undecided voters inatia shuku ya JK na CCM kuwa wameyachakachua matokeo ya SYNOVATE kama walivyoyachakachua yale ya REDET.

Kwa lugha ya Kinana ni kuwa hata hizo asilimia 18 JK atabeba na hivyo kufikisha asilimia 79 au 80 ambayo ndiyo wamekuwa wakijigamba nayo.

SYNOVATE ya Tanzania siyo ile ya Kenya hata kidogo hii wamejaa mashushushu wa JK na CCM.

Hawa SYNOVATE walidai ya kuwa watatoa tathmini yao kabla ya uchaguzi sasa wiki tatu kabla ya uchaguzi purukshani hii ni ya nini? Kwa nini wanaona umuhimu wa kutupooza na yale ya REDET?

Kama haya matokeo yangelikuwa ni ya kweli mbona JK amefuta siku za mapumziko zote ndani ya CCM na amedai kufanya kampeni ni usiku na mchana?

kwa kufanya hivyo JK, ajua ukweli kuwa anaanguka lakini ahitaji dhuluma kuendela madarakani
 
Ukweli ni kuwa tayari wameshawashangaza kutokana na hali halisi walio ikuta huko ambapo hawakutegemea kuona Vuguvugu la UKOMBOZI WA Slaa halina makali kama walitegemea.............

Omar,

Tatizo lako Dr. Slaa au mabadiliko? Hakika pona ya CCM ni wizi ila uwe wa hi-tech. Siamini hapa Mambali mapokezi ninayoyapata yakiwa na ushikiano na uelewa wa Tz ijapokuwa ni km 40 toka nzega mjini.
 
Ndugu wanajamii inasikitisha sana kuona baadhi ya taasisi kama REDET NA SYNOVATE zikitoa matokeo ya tafiti za mezani,zisizo na chembe ya ukweli hata kidogo na kuziachia kwenye vyombo vya habari zikishabikiwa na baadhi ya watanzania wenye upeo mdogo(siwalaumu kwa kutokwenda shule).
Tafiti hizi zimekua zikiharibu vichwa vya wapiga kura wetu hasa wenye upeo mdogo na wapenda mageuzi.
Inabidi tujiulize nini la kufanya?
Jawabu(a)Kura za maoni za kwenye mitandao ya kijamii kama hizi za JF ambazo the real doctor amemgalagaza vibaya mno doctor wa heshima(sijui heshima gani)yafaa kabisa na huu ni muda muafaka zipelekwe magazetini wabongo wasiopita mitandaoni wazione.hii itasaidia sana kuongeza ari ya mioyo iliyoanza kufa kutokana na tafiti za mrengo1 za REDET na mwanae SYNOVATE.
Jawabu(b)Yafaa kabisa idadi ya ma fans na wanao mfollow mgombea fulani kwenye mitandao kama facebook na twitter imwagwe hadharani kwenye magazeti,radio na televisions..hii itakua bonge la counterattack kwa CHALE CHALE MIKE.....

Ndugu wanajamii majawabu che na de mnayafahamu. . . . .. . . . . Ni hayo tu!
 
Ukweli ni kuwa tayari wameshawashangaza kutokana na hali halisi walio ikuta huko ambapo hawakutegemea kuona Vuguvugu la UKOMBOZI WA Slaa halina makali kama walitegemea.............
Kwani REDET na Synovate walienda kufanya utafiti kujua nguvu ya Slaa au nguvu ya wananchi(peoples power). Basi kama ndivyo walivyofanya kulingana na mawazo yako wamekosea sana Slaa hana nguvu ila nguvu iko kwa wananchi na ndiyo maana nasema nguvu ya wananchi itawashangaza, na mind you that wamefanya utafiti wa watu 2000 tu kati ya mil. 40.
 
Sasa kama sample space yako inainclude mostly wenyeviti wa serikali za mitaa na wajumbe wa nyumba kumi watu lazima wanagake
 
Toka uchaguzi wa vyama vingi uanze 1992 sijaona mwamuko wa kisiasa kama ninaoshuhudia leo, hii ni ishara ya mabadiliko makubwa kutokea siku ya kupiga kura ambapo wananchi wote watashirikishwa kufanya utafiti tofauti na utafiti wa REDET na Synovate unaowahusisha watu 2000 tu. People will prove REDET and Synovate wrong na aibu itaenda kwa mashirika hayo. Nina kila sababu:

Tatizo ndugu yangu ni kuwa NEC ndiyo wamenunuliwa ila wasimamie uchakachuaji wa matokeo yale yatakayopelekwa Dar kutoka mikoani yatakuwa yamekwishachezewa na mashushushu ambao wamesambazwa nchi nzima.

Unapoona uchaguzi huu kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii wapigakura wanazuiwa na NEC kuwa mita 200 kutoka kwenye vituo vyao ufahamu ya kuwa ipo njama nzito ya kuchakachua matokeo kwa kuwanunua mawakala wa Chadema.

Vyama vya upinzani kuishinikiza NEC kurudisha haki ya wapiga kura kuthibiti vituo vyao ndiyo jiba pekee la hii sakata
 
Facebook kuna pages hizi
Dr. Willibrord Slaa(imeandikwa hivyo)- fans-11,477
JAKAYA MRISHO KIKWETE FOR 2010- fans 5,023
Jakaya Kikwete- 15,243
My president is Dr Willbrod Slaa- fans 354
Hiyo ya Slaa ya kwanza iko active na nadhani inakuwa controlled na mwenyewe(au muhusika sio mtu baki).
Hiyo ni kutoka facebook nimeiwakilisha.
 
Repoti mpya ya synovate inayoonyesha jk anakubalika kwa 61%, na ile ya redet inayoonyesha 72% lengo limekuwa moja,

ripoti hizi zimetolewa kwa kufuatana, lengo likiwa kuchanganya psychologia ya wapiga kura kuonyesha kuwa jk anaongozo

kwa mtazamo wangu, naona hizi taasisi mbili zipo chini ya mkono mmoja wa mafisadi, na lengo lao ni moja.
 
SYNOVATE waliahidi matokeo ya utafiti wao wangeliyatoa siku chache kabla ya uchaguzi sasa wiki tatu ndiyo siku chache kabla ya uchaguzi?

Inaelekea kabisa kunashinikizo la Jk na CCM kuyapigatafu matokeo ya REDET kwa kuonyesha yanaungwa mkono na SYNOVATE.

Hii SYNOVATE ya Tanzania siyo sawasawa na ila ya Kenya ambayo ina maadili na hadhi inayoeleweka
 
:llama:sasa kama kuna mtu ana connection na watu wa magazetini hizi takwimu inabidi watz wazione yani vitu vimwagwe in public...slaa for 2010!
 
Bila ya Chadema kujipanga upya CCM wenzio wamekwisha kupika matokeo yao na wanajaribu kupima tutayapokeaje?

Wametugeuza kuwa "guinea pigs."


MAY GOD FORBID
 
wadau, hii ni njia moja ccm, wanayotaka kutumia kuchakachua, kura, tunachotakiwa ni kuelimisha ndugu zetu kuhusu, mapungufu ya huu utafiti wa redeti na synovate.
 
Hii SYNOVATE ya Tanzania siyo sawasawa na ila ya Kenya ambayo ina maadili na hadhi inayoeleweka [/B said:
[/QUOTE

money power vs peoples power
 
Lawama haziwezi kutusaidia.Hawa jamaa wanafanya kazi kwa maelekezo ya CCM.Hivi Watanzania,hususan wana JF tumeshindwa kabisa kuendesha opinion poll ya kitaalamu badala ya kuwategemea wachakachuaji wa REDET na Synovate?
 
Back
Top Bottom