Uhamiaji vs Kigoma

McFerson

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
2,120
2,167
Wakuu salaam.

Declaration: Mimi ni Muha wa Kigoma. Nikijikita kwenye mada,suala la watu wa Kigoma kutotambuliwa na watu wa uhamiaji(MHA) kama raia halali wa Tanzania limekuwa la muda mrefu.

Ukitaka utambulisho wowote kama Mtanzania utakutana na mikwara mizito sana.

Mara ya kwanza kutaka kwenda nje ya nchi nilisumbuliwa kiasi kwamba nikajiuliza hivi kama sitambuliki Tanzania,Burudi,Congo na Rwanda je! Kigoma ni nchi nyingine?

Sikatai wanaoishi mipakani wanapata usumbufu lakini unajiuliza mbona kwa Kigoma ni too much? By the way Kigoma ndio ilipaswa kupewa hadhi Tanzania kwa kuwa Tanganyika asili ya Kigoma ndio ilizaa jina la Tanzania kwa muungano na Zanzibar.

Nipende kumalizia kwa kusema M.H.A achaneni na masuala ya roho mbaya, no Kigoma no Tanganyika and no Tanzania.
 
Wakuu salaam.

Declaration: Mimi ni Muha wa Kigoma. Nikijikita kwenye mada,suala la watu wa Kigoma kutotambuliwa na watu wa uhamiaji(MHA) kama raia halali wa Tanzania limekuwa la muda mrefu...
Hiyo cha mtoto, usiombe uwe na sura inayofanania watusi yaani mwembamba mrefu na pua ndefu ndo utasumbuka mpaka ukome utaambiwa wewe ni myarwanda hata kama ukija na wazazi wako ukawaonesha hapo bado utaambiwa wewe ni mtusi rudi kwenu Rwanda sasa unajiuliza inamaana umezaliwa bongo kimakosa?
 
Back
Top Bottom