Raj kapool
JF-Expert Member
- Jun 29, 2018
- 1,557
- 2,597
Ngoma imeisha, timu imecheza vizuri inanyumbulika, kilichobaki ni pumzi tu, second half mechi nyingi tunakata moto
"Ni kocha mzuri sana kwenye upande wa saikolojia ya kuandaa wachezaji, namshindia alama 100 kwa 100. Labda kwa sababu alitokea kufundisha watoto (timu ya vijana ya Madrid), ndiyo maana anawajua vizuri wachezaji na tabia zao.Huyo ni kwenye press ya jana baada ya game yetu dhidi ya Atletico, jamaa anaonekana ana uelewa mkubwa sana wa wachezaji wake na namna anataka wawe, akipata support ya wachezaji wake, basi ana uwezekano mkubwa sana wa kufanya vizuri siku zijazo.
Kidogo kidogo tu, hakuna aliyejua kuwa jamaa yupo hivi, so atakuwa anabadilika kadri muda unavyoenda,ukizingatie pia sub zake ni kama za utambulisho, so muda sio mrefu atakuwa na full squad fit kasoro Rodrygo tu, so atakuwa na uwanja mpana wakufanya mautundu!"Ni kocha mzuri sana kwenye upande wa saikolojia ya kuandaa wachezaji, namshindia alama 100 kwa 100. Labda kwa sababu alitokea kufundisha watoto (timu ya vijana ya Madrid), ndiyo maana anawajua vizuri wachezaji na tabia zao.
Real Madrid ya sasa imechangamka; mchezaji anayepoteza mpira ndiye anakuwa wa kwanza kuanza kuzuia (counter-pressing). Hii mara ya mwisho niliiona timu ikiwa chini ya Zidane. Sasa hivi anatakiwa akomae pia kwenye upande wa mbinu (tactics), ikibidi akae na Zidane apate 'madini'. Zidane alikuwa fundi sana kwenye mabadiliko (subs); akifanya sub, ujue mpinzani amekwisha.