Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread

Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread

Mpira kitu cha ajabu sana, Neuer amefanya saves nyingi kweli nyingine unaona kabisa angekuwa golikipa mwingine ingekuwa goli, ila mpira wa Vinicius ukamshinda kuudaka.,
 
Fainali ingekua tamu kama Madrid wangecheza na PSG
Najua fainal haitakuwa nyepesi kwa sababu hawa Dortmund wana vijana wengi sana na wana kazi balaa..

Natamani fainal pale golini awepo Thibo,kwa sababu uwezo wake wakusoma mwendo wa mchezaji ni mkubwa sana.

However,for now tusherehekee kufika fainal expecting tunaenda kuchukua ndoo ya 15.
 
Jamaa aliona kama ameshamaliza game, ndio maana akafanya sub za kiboya vile, ninadhani aliamua kujilinda zaidi.
Mimi naona bado makocha wengi wataendelea kupokea vipigo vya dakika za jion nakushangaza hapa Bernabeu kwa sababu akili ya wadau wote wa madrid tunaamini mechi imeisha pale refa anapopuliza filimbi yakumaliza mchezo.

Ndo maana naamini kuwa "pale ambapo timu pinzani inaona imeikamata madrid katika mchezo,basi ukwel ni kuwa timu hiyo ndio imekamatwa na madrid imeilazimisha hiyo timu icheze hivyo ili madrid aweze kupata ushindi",

Matokeo ya namna hii yenye msisimko hayaji bahati mbaya wala bahati bali ndio tabia za club bora dunian namna inavyouendea mchezo nakutaka matokeo.
 
Back
Top Bottom