Wewe ni muongo.
Hujui mpira.
Mpira = biashara + championship
Timu haiwezi kukumbatia wachezaji wote hata wawe wazuri aje... Eti kisa wataleta ushindi. Kumbuka Payroll inawahusu.
Kwa akili yako, basi hakuna timu ambayo haijaingia hasara kwenye uuzaji wa wachezaji.
- Madrid aliingia hasara kumuuza Robben.
- Chelsea aliingia hasara kumuuza Debruyne
- Madrid (tena) aliingia hasara kumuuza Dimaria kisa Rodriguez
- Arsenal aliingia hasara kumuuza Gnabry
- Man United waliingia hasara kumuuza Ronaldo
- Tottenham waliingia hasara kumuuza Modric
Usiwe una copy na kupaste content za watu... Andika uchambuzi wako binafsi.
Mkuu kuna mambo mengi huwa tunazungumza kimihemko tu ila hayana uhalisia
Hakuna hasara yoyote iliyopatikanwa hapo kwa kuuzwa hao wachezaji labda kwa ishu ya Robben tu.
- De bruyne alishindwa ku develop akiwa chelsea, na huyo de bryune tunaemuona sahivi asingelipatikanwa kama angeendelea kubaki Chelsea, KDB ali develop alipokuwa Germany na ndipo alipoanzwa kuchezeshwa midfield badala nafasi yake ya awali winger. Kwa CHelsea angeendelea kubaki kuwa winger na pengine hivi sasa angelikuwa ameshasahauliwa.
- Madrid haikula hasara kumuuza Di maria mana hapakuwa na pengo lake popote, Tukumbuke kuwa nafasi ya Di maria ilishachukuliwa na Bale wakati bado Di maria akiwepo, Carlo alijiongezo na akamdevlop akawa anacheza Midifield, Ni kweli DI maria alikuwa ana uwezo mkubw akuliko Bale na James, ila kuondoka kwake hakukuiathiri timu kwa chochote. Na madrid walipiga faida ndefu kumuuza kwake.
- Ishu ya Arsenal na Gnabry ni hivo hivo kama ya KDB, Gnabry ali develop baada ya kuondoka arsenal, angeendelea kubaki pengine angeishia kuwa Carlos Vela mwengine.
- Man Utd walipata hasara kwa njia gani? a) walipata faida ndefu kwa kumuuza Ronaldo, b) Ronaldo hakuwa tayari kubaki tena kwenye timu kwa maana hata wasingemuuza angeishia kuondoka bure. c) Mafanikio na tunzo alizozipata akiwa Real usifikirie kuwa pia angelivipata akiwa Man Utd, Real MAdrid ilikuwa timu bora iliyomsaidia akapata mafanikio Bora usifikirie zile 50+ Goals angeliweza kuzifunga pale man utd au yale mataji ya Champion League yalioyjipanga angeyapata pale Man utd chini ya David Moyes na Van Gaal. huku team mates wake wakiwa akina Rashford na Evans.
- Modric asingefikia peak yake akiwa na timu kama spurs ambayo ilikuwa ikicheza mpira usioeleweka, mpaka anaondoka Spurs alishafikia kuchezeshwa forward kabisa position ambayo sio nzuri kwake na alishaondolewa kwenye midifield mana alikuwa hapigi mikasi.