ze-dudu
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 18,428
- 24,145
Importantisimo' 878.
Zilikuwa siku 878 'muhimu sana' (Importantisimo) kwa Madridistas. Zilikuwa siku ambazo kila mmoja alifurahia maisha. Kila dakika zilikuwa murua. Utra Sul au Grada wote tulifurahia uwapo wako.
Lakini sasa tunaanza maisha bila ZINEDINE ZIDANE. Ulipoahidi mabadiliko kuanzia Juni mwaka huu, niliamini kuwa utasajili wachezaji wapya. Lakini hadi unaondoka hakuna 'Galactico' aliyesajiliwa. Ikiwa na maana umemwonesha Florentino Perez kuwa inawezekana.
Perez alichonga kinyago ambacho kimemletea mafanikio ya kutosha bila matanuzi sokoni. Unaondoka bila kumsajili 'kipenzi' chako Eden Hazard. Unaondoka katika kipindi ambacho unasema huna la kuwashawishi tena wachezaji.
Ni kweli wamefanya kila kitu kwa ajili yako na umewasaidia kushinda kila kitu ndani ya siku 878. Ulikataa kuajiri kocha msaidizi mwenye jina kubwa.
Badala yake ukawachukua washikaji zako wa utotoni, Hamidou Msaidie na David Bettoni. Hofu niliyokuwa nayo msimu huu juu ya kuondoka kwako, imedhihirika. Pengine nilikuwa kama kunguru mwoga lakini nilichokiona kimetokea.
Zizzou umeondoka katika kipindi kitamu ambacho bado tuna mashamshamu ya ubingwa. Bado tunawashwa washwa kutamba na kuringa.
Sina mashaka kuwa kuna jina umelidokeza kwa Perez, lakini inafaa pia kumpa timu RAUL GONZALEZ, SANTIAGO SOLARI au GUTIEREZ 'GUTI? Sijui... lakini inawezekana.
Asante sana na kwaheri ZINEDINE ZIDANE. Ulikuwa 'Importantisimo".