Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread

Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread

Fantastic assist from cr7 to Isco..[/QUOTE
Hilo goli limenikumbusha ile nguvu yetu ya counter attack na umaliziaji wa uhakika, kweli vijana wanajituma kurudisha ile hali yetu, ni Benzema tu bado anashangaa,ila nimeona hari waliyonayo vijana wetu, kidogo dogo tutarudi tena.,
[HASHTAG]#HalaMadrid[/HASHTAG]!!
 
Cr7 hana bahati kwa kweli. Anajitahidi sana ila nyavu zinagoma
Huwa inatokea kukosa bahati kuweka mpira wavuni, Ramos na yeye pia amekuwa hana bahati kweli, japokuwa anajitahidi sana kutafuta goli., mambo yakirudi kwenye mstari ndio wataanza kutupia, ila kwasasa wanatakiwa watulize akili tu.,
 
Wameiona hii comment yako. Cr 7 na Ramos wapo JF now
 
KANE ASUKUMIWA REAL MADRID

Real Madrid wanashinikizwa kumsajili nyota wa Tottenham Harry Kane na wasambazaji wa fulana Adidas, kwa mujibu wa Don Balon .
 
REAL MADRID YAWASILIANA NA COUTINHO

Real Madrid wanaamini wataweza kuipiku Barcelona katika mbio za kumsajili Philippe Coutinho, kwa mujibu wa Mundo Deportivo .
Baada ya jitihada zao kugonga mwamba kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazili majira ya joto, Barca sasa wanataka kurudi upya kwa ajili ya kiungo huyo dirisha la uhamisho litakapofunguliwa Januari. Lakini Madrid imeibuka kuwa timu nyingine ambayo anaweza kujiunga nayo nyota huyo.
 
REAL BADO WANA TUMAINI LA KUMPATA NEYMAR

Real Madrid wanapanda mbegu kumsajli Neymar siku za mbeleni licha ya Mbrazili huyo kuhamia PSG kwa uhamisho wa rekodi ya dunia miezi michache iliyopita, kwa mujibu wa Diario Gol .
Ripoti zinadai kuwa Mbrazili huyo anataka kutwaa Ballon d'Or na Ligi ya Mabingwa akiwa Paris ndani ya miaka miwili. Ikiwa hatafanikiwa kutimiza malengo haya, basi Neymar atatafuta njia ya kutokea.
Inaaminika rais wa Real amekuwa kwenye mawasiliano ya karibu na baba wa mchezaji huyo ambaye pia ni wakala wake, na amesisitiza kuwa milango ya Real Madrid itakuwa wazi kwa daima.
 
MESSI AMKATAZA AGUERO KUJIUNGA NA REAL MADRID

Lionel Messi amemshauri Mwargentina mwenzake Sergio Aguero kutojiunga na Real Madrid mwaka ujao, kwa mujibu wa Diario Gol .
Rais wa Madrid Florentino Perez amemtaja straika wa Manchester City, Aguero kuwa mchezaji sahihi na anaamini ataweza kumshawishi kujiunga na Blancos ikiwa Pep atamsajili Alexis Sanchez.
Lakini kwa mujibu wa habari Lionel Messi amemtumia ujumbe Aguero kwa njia ya WhatsApp, na amemwambia rafiki yake kipenzi na Mwargentina mwenzake kuwa ni vema abaki Manchester kwa sababu Madrid inaelekea kuporomoka na City wanazidi kuwa tishio chini ya Guardiola kwa sasa.
 
REAL MADRID YAWASILIANA NA COUTINHO

Real Madrid wanaamini wataweza kuipiku Barcelona katika mbio za kumsajili Philippe Coutinho, kwa mujibu wa Mundo Deportivo .
Baada ya jitihada zao kugonga mwamba kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazili majira ya joto, Barca sasa wanataka kurudi upya kwa ajili ya kiungo huyo dirisha la uhamisho litakapofunguliwa Januari. Lakini Madrid imeibuka kuwa timu nyingine ambayo anaweza kujiunga nayo nyota huyo.

Mundo Deportivo ni Catalan based newspaper, siamini report yoyote wanayoitoa kuhusu Real Madrid.
 
MESSI AMKATAZA AGUERO KUJIUNGA NA REAL MADRID

Lionel Messi amemshauri Mwargentina mwenzake Sergio Aguero kutojiunga na Real Madrid mwaka ujao, kwa mujibu wa Diario Gol .
Rais wa Madrid Florentino Perez amemtaja straika wa Manchester City, Aguero kuwa mchezaji sahihi na anaamini ataweza kumshawishi kujiunga na Blancos ikiwa Pep atamsajili Alexis Sanchez.
Lakini kwa mujibu wa habari Lionel Messi amemtumia ujumbe Aguero kwa njia ya WhatsApp, na amemwambia rafiki yake kipenzi na Mwargentina mwenzake kuwa ni vema abaki Manchester kwa sababu Madrid inaelekea kuporomoka na City wanazidi kuwa tishio chini ya Guardiola kwa sasa.

Sasa Agüero wa nini? Hizi habari nyingine bhana, watu wanamipango ya kuondoa Cristiano, Bale na Benzema wao, aletwe Agüero?
 
Ukame wa penati unaoitokea Real Madrid haujawahi kutokea kwa miaka 36, yatajwa kuwa sehemu ya anguko la Cr7

Kati ya sababu ambayo imeshaanza kuongelewa kama chanzo cha kutofanya vizuri kwa Real Madrid msimu huu ni ukosefu wa penati, michezo 11 ya ligi kuu La Liga Los Blancos hawajapewa penati.

Mara ya mwisho kwa Real Madrid kucheza michezo 11 bila kupewa penati ilikuwa msimu wa mwaka 1980/1981 na kuanzia hapo Real Madrid wamekuwa wakipewa penati nyingi kula msimu.

Kuanzia msimu wa mwaka 1982 Real Madrid hawajawahi kucheza mechi 11 bila penati ambapo msimu uliopita katika kipindi kama hiki tayari Real Madrid walikuwa wameshapewa pigo la penati mara mbili.

Msimu wa mwaka 2015/2016 Real Madrid almanusra wakose penati lakini walifanikiwa kupata penati moja katika michezo 11 lakini msimu wa 2014/2015 ndio waliweka rekodi kwani walipata penati 5 katika mechi 11.

Kuanzia msimu wa 2011/2012 hadi kufikia msimu wa mwaka 2014/2015 Real Madrid hawajawahi kupewa chini ya penati 4 ndani ya mechi 11 za mwanzo na wakipata penati 19 katika misimu minne mechi 11 za mwanzo.

Tangu Cristiano Ronaldo ajiunge na Real Madrid mwaka 2009 hawajawahi kukaa muda mrefu hivi bila kupata penati na sasa ukame wa mabao unaomuandama Cr7 unatajwa kusababishwa na ukame wa penati
 
The professor is back working with the ball.

DOMfZumXcAEAVOk.jpg
 
Bale kaumia tena (groin) and looks like atakua nje ya uwanja kwa mwezi ivi,sijui nani alibana uyu jamaa kwenda Utd kipindi kile walivyo komaa nae.
1d0f2b1c2d330c10601e62e68f5ed749.jpg
 
Back
Top Bottom