Nilifurahi nilipoona kijana amerudi kundini, anahitajika sana kwa sasa kurudisha ile fighting mentality, game zote mbili tulizocheza japokuwa hazina maana zaidi ya maandalizi, sikuona our usaual character, vijana walijikuta wanapasiana katikati ya uwanja tu, wapinzani haswa mabeki hawakufeel presha yetu kabisa kitu ambacho sio cha kawaida.
Sijui ni nani atavyaa viatu vya Ramos na Ronaldo kwa kweli, Marcelo sio wa kumtegemea kihivyo, labda Asensio na Theo, kidogo ninaona hawa vijana wanapenda kushinda, hao wengine wanapenda kucheza tu mpira.