Re: Vichekesho nane vya nguvu. Enjoy... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Re: Vichekesho nane vya nguvu. Enjoy...

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Wambuzi, Jun 18, 2012.

 1. W

  Wambuzi JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Mwizi wa atm

  Jamaa aliibiwa kadi yake ya benk akaulizwa kama ameripoti polisi akajibu "sijaripoti bado, mwizi mwenyewe hamfikii matumizi kama mke wangu.

  Cheka kidogo

  Njia rahisi kusahau matatizo yako (japo kwa muda mfupi) vaa viatu vinavyokubana.

  Mlizi mbio mbio

  Tulikuwa bar moja jana mlinzi kaingia spidi, akamwambia jamaa mmoja aliyekaa kaunta, Mlinzi: Mzee gari lako limeibiwa Mzee: Umemtambua aliyeiba? Mlinzi: Hapana lakini nimeandika namba za gari hizi hapa.

  13, 13...


  Jamaa alikuwa anapita nje ya wodi ya vichaa akasikia mtu anasema, 13, 13, 13, 13, 13, 13,..... akaamua kuchungulia kwenye kitundu alichokiona ajue kuna nini, ile kuchungulia tu akamwagiwa mchanga wa machoni, sauti ikabadili ikaanza 14,14,14,14,14......

  WATAALAM

  Jamaa alikuwa anaumwa sana, mkewe akamwita daktari, alipofika akamkuta jamaa kafumba macho;
  Dokta: Huyu mbona amekwisha kufa?
  Jamaa: Sijafa bwana
  Mke: Hebu nyamaza bwana acha kubishana na wataalamu.

  Ya leo mgonjwa


  Dokta alipotembelea wodi ya mgonjwa wake aliyepata ajali. Mgonjwa akiwa amening'inizwa mikono juu akauliza "dokta ntaweza kweli kupiga kinanda nkitoka hospitali?"
  Dokta: Bila shaka utaweza, wewe ni mpiga kinanda mzuri enh?
  Mgonjwa: Hapana sijawahi kabisa bado.

  4WD


  Mwanaume alimnunulia pete ya almasi mkewe, rafiki akauliza "si ulisema anapenda gari yenye four wheel drive, mbona umenunua pete?" Mume akajibu "unadhani wapi ntapata rav4 feki?"

  Ajali ilivyotokea


  Trafiki polisi akihoji palipotokea ajali "ahaa! Sasa naanza elewa embu nielezee jinsi ajali ilivyotokea wewe ukiwa kama dereva mhusika." Dereva akajibu "hata sikumbuki nlifumba macho"

  Faini ya kukojoa

  Polisi alimdaka jamaa anakojoa pembezoni mwa ukuta.
  Polisi: Wewe unajua panakatazwa kukojoa hapa?
  Jamaa: Sasa nimebanwa nifanyaje?
  Polisi: Faini yake elfu tano.
  Jamaa akatoa noti ya elfu 10.
  Polisi: Sasa chenji tunaipataje?
  Jamaa: Tafuta chenji unipe changu.
  Polisi: Basi kojoa tena...

  Mume anaenda kazini

  Jamaa kaamka asubuhi sana Jumamosi, mvua inanyesha kang'ang'ania kuwa anaenda ofisini. Kawasha gari yake, kufika njiani hali ilikuwa mbaya kaamua kurudi. Kafika home kavua nguo kaingia tena kitandani, kamnong'oneza mkewe aliyekuwa usingizini; "Yaani hali ya hewa huko nje mbaya sana" Mke: Si ndio nimemshangaa huyu mpumbavu eti kaenda kazini...

  Hasira za mtoto

  Baba na mtoto:
  Baba: Mwanangu ukiwa na hasira unafanya nini?
  Mtoto: Naenda chooni.
  Baba: Chooni? Kufanya nini?
  Mtoto: Kusafisha.
  Baba: Halafu ndio hasira zinaisha?
  Mtoto: Ndio. Nasafisha choo kwa mswaki wako.

  Mgonjwa na Dokta


  Mgonjwa: Dokta nimekuja nahisi ninaumwa Malaria na kifua.
  Dokta: Sasa ushajua unaumwa nini hapa umefuata nini kwangu?
  Mgonjwa: Sasa si nimekuja kwa dokta.
  Dokta: Wanaojua kuwa wanaumwa kama wewe wanapitiliza maabara.

  Pilau la bachela


  Bachela mmoja aliyekua akiishi kwa muda mrefu peke yake kwenye nyumba aliyopanga siku moja alitaka kupika pilau kwa mara ya kwanza. Sasa asijue nini kinachobadilisha rangi ya wali kuwa rangi ya brown, yeye akapika kama kawaida (wali) kisha wakati wa kula akavaa miwani yenye rangi ambayo ukiuangalia wali unauona kama pilau wakati anakula.

  Mwizi na chizi

  Mwizi kaiba TV na kuanza kukimbia nayo, kumbe ile nyumba mlikuwa na chizi, akaanza kumkimbiza yule mwizi. Kila mwizi akiongeza mbio chizi nae huyo, mwishowe mwizi akasalimu amri na kusimama, yule chizi akamsogelea na kumwambia.. Daah umesahau remote hii hapa mwizi kafleti.

  Chemsha bongo

  Baba akimuuliza chemsha bongo mwanae anayesoma shule ya chekechea "haya niambie kitu gani hakiwezi kuliwa wakati wa breakfast?" Mtoto akajibu "hiyo mbona rahisi baba, si lunch na dinner"
   
 2. Badu

  Badu JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 364
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Teh! Teh! Teh! Teh! Teh!
   
 3. sister

  sister JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,025
  Likes Received: 3,929
  Trophy Points: 280
  Acha tucheke..........kwikwikwi.
   
 4. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,148
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Nashukuru wameee, nimecheka
   
 5. W

  Wambuzi JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Pamoja sana ndugu yangu Jumapili Waheed
   
 6. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,760
  Trophy Points: 280
  Sikutegemea kucheka hivi kwa siku ya leo.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 7. Domowazi

  Domowazi JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asee ngoja nicheke...
   
 8. b

  bigbumper Member

  #8
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hahahahaha mngejua nachocheka
   
 9. N

  Neylu JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,650
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hahahaaaaaa...Kwa kweli mimi umenichekesha sana..Nilikuwa nacheka mwanzo mpaka mwisho...Safi sana.
   
 10. Kilahunja

  Kilahunja JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 1,497
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Uyo mtoto wa kusafisha choo kwa mswak wa dadii yake ni noumah..kwikwikwi
   
 11. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2012
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  mbona hujaweka vichekesho?
   
 12. kijembeee

  kijembeee JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 411
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  utachekaje kama bandama lako mchina?
  vya kuchesha hucheki,unacheka tu kwa kufata mkumbo
  the storiz are funy
   
 13. KML

  KML JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 863
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  jamaa we noma nimecheka sana na watu wa oficn hapa
  hahahahahahaha...
   
 14. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Rahaaaaaaaa umenipa!!!!!$$$
   
 15. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #15
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  dadii alikuwa hasikii tofauti akitumia mswaki uliosafisha choo?
   
 16. Swts

  Swts JF-Expert Member

  #16
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 3,072
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Hahahah ama kweli,usishindane na doctor
   
 17. Sabry001

  Sabry001 JF-Expert Member

  #17
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,064
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  kidogo ntapike! Nnavowachapaga watoto itabidi mswaki nianze kutembea nao. Teh!
   
 18. W

  Wambuzi JF-Expert Member

  #18
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  we hujaviona eenh meno ngiri??? endelea kusubiri mkuu
   
 19. mimixoxo

  mimixoxo Member

  #19
  Jun 20, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hahahahaha nimeipenda hiyo ya faini ya kukojoa na mgonjwa na doctor. Nice ones.
   
 20. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #20
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  ............ile ya kubanwa na viatu ! Chukulia unatembea kwa mguu huna pesa ya taxi wala ya Daladala ! Usipimeee!
   
Loading...