Re: OBOTE AMEME (BONDIA MTANZANIA)

masssaiboi

JF-Expert Member
Feb 10, 2009
636
132
Nimetoka kuangalia pambano la bondia mtanzania aitwaye Obote Ameme na kijana mdogo wa kizungu, pambano limefanyika nchini Uswiss na lilikuwa linaonyeshwa na kituo cha Sky sports hapa UK. Lilikuwa ni pambano la utangulizi kabla ya pambano la Bingwa Klitchiko na lilikuwa la raundi nne.

Kwa kweli jamaa amejitaidi kwa kiasi chake lakini ukilinganisha na mtoto aliyekuwa anacheza naye wala hamfikii kabisa. Katika suala la ufundi wa kupigana bado yuko nyuma sana kwani muda mwingi alikuwa anajikunjamania tu.
Pia alikuwa na msaidizi mmoja tu ukilinganisha na mwenzie aliyekuwa na watatu, nilichosikia kutoka kwa huyo mshkaji ktk raundi zote nne ni pale alipomwambia maneno haya tu ''mbavu hizo mbavu hizo, we unaweka gadi tu atakuumiza mwenzio''
Mie simlaumu huyu bondia ila lawama ni kwa wanasiasa wetu kwa kushindwa kuendeleza vipaji, jamaa alivyoonekana ni kama vile hakuwa na msaada wowote kutoka wizara husika na mara zote walipokuwa wanaitaja Tanzania nilijisikia vibaya sana tu.
 
Huyo ni bondia wa kulipwa ama wa ridhaa?

Huyu jamaa ni pro, naona mleta mada anaangukia kwenye kundi la walewale ambao wanataka kuilaumu serekali kwenye kila jambo. Angekuwa wa ridhaa, tungekuwa na haki ya kuishambulia serekali.
 
Mie sijawahi kumsikia ila awe pro au amateur lakini hali ilikuwa siyo nzuri kabisa.
 
tupe matokeo ya pambanao lake. na je wewe ulimsaidiaje?
 
stats zake as a boxer ni mbovu.

OBOtE AMEME STATS

39 wins, 21 Losses that is an average boxer. Halafu angalia stats zake ame loose na maboxer wote aliopigana nao wanaotoka nchi zingine.
Interesting kapigana na Rogers Mtagwa.

Kina Matumla wameishia wapi? Of boxers I would expect to do well ni hao.
 
Jamaa mwenyewe anaonekana kama Mnywa juice la Tende.....

url
 
Matokeo ya pambano ilo ni kwamba jamaa alipigwa raund zote, Mtoto alikuwa anarusha vitu vilivyoenda shule ila kilichomsaidia mshkaji wetu asiende chini ni kwasababu ya ugumu, mcheki kwenye picha utaona mwenyewe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom