Kuwa Daktari huchukua miaka mitano ya shule pamoja na mwaka mmoja wa internship hapo ndo unakuwa daktari wa kawaida but ukitaka kuwa na heshima ya udaktri, ongenza miaka mitatu ya residency jumla inakuwa miaka tisa na kwa ma DMO walio wengi wamesoma miaka 9 na wengine wapo hapa tunasoma nao. Kwa kifupi inaudhi na inatia hasira nisome miaka tisa halafu mwanasiasa tu hata shule hana anakuja kukuweka ndani kwa umaarufu wa kisiasa na kutafuta sifa za kijinga! Eti nilitaka apate akili! Kati ya yeye na Dr nani mwenye akili? Naunga mkono uamuzi wa Dr kujiuzulu.