Habari hizi nimezisikia juu juu lakini inaonekana ni za ukweli kwa hiyo mwenye details atupatie!
Ilivyo ni kwamba, Mganga Mkuu wa wilaya moja huko Singida ameandika 24 hours notice kuachia ngazi!! Inasemekana sababu ni Mkuu wa Mkoa, Dr. Nchimbi alimweka ndani, Mganga Mkuu husika anaitwa Erick Bakuza.
Naona watu washaamua kujilipua!!
NOTE: Kuna watu wanajikita kwenye hoja zisizo na msingi kwamba, Mkuu wa MKoa alikuwa na mamlaka ya kumweka ndani kwa sababu sheria za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa zinatoa mamlaka hayo kwa RC & DC!!!
Hata hivyo, inasemekana sababu ya DMO husika kuwekwa ndani ni kutokana na kushindwa kutoa ripoti ya ugonjwa wa kipindupindu!!!!
Wakati tunaambiwa sababu ni kushindwa kutoa ripoti ya kuzuka kwa ugonjwa wa kipindupindu; sheria ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa zinatoa mamlaka hayo kwa RC & DC kutokana na nafasi zao kama walinzi wa amani na usalama kwenye maeneo yao!! Aidha, RC au DC anatumia mamlaka hayo endapo mhusika ni MHALIFU na amefanya uhalifu UNAOHATARISHA AMANI & UTULIVU!

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Singida ameamua kuachia ngazi na kuachana na kazi hiyo na kwenda kutafuta utaratibu mwingine wa maisha.
Taarifa hizo za DMO kuachia ngazi zimewashtua watumishi na wengi waliokuwa karibu naye kwa sbb walifanya nae kazi kwa upendo na ushirikiano mkubwa.
Siku chache zilizopita alianza kwa kuachia ngazi ukuu wa Idara,hata alipohimizwa kuendelea ili aweze kusaidia Idara,hakuwa tayari.
Taarifa zinadai DMO kaamua kuachia ngazi baada ya kuona "siasa" zimekuwa nyingi na kuingilia utendaji na utaalamu.Hali hiyo ilianza mwezi November mwaka jana ambapo Mkuu wa Mkoa wa Singinda Dr Rehema Nchimbi alipotofautiana na DMO kuhusu "status" ya kipindupindu ktk Wilaya ya Singida Mjini.
Tofauti hizi za kiutendaji kati ya DMO na RC ndio zinahusishwa na uamuzi huu wa DMO kubwaga manyanga na kutafuta riziki mahali pengine.Hata Mkuu wa Mkoa alipoulizwa,alikiri kutofautiana na DMO katika suala la kipindupindu Wilaya ya Singida Mjini