RC Makalla: Leo(Desemba 8) saa 6 kamili usiku tutapiga fataki kama Ishara ya kuanza sherehe za uhuru!

Uhuru gani huo mnaotuambia leo hii taifa linalotegemea hisani ya beberu mpaka kwenye bajeti ya serikali miaka 60 baada ya kuupata?

Uhuru gani huo mnaokamata wapinzani wenu kisiasa bila kufuata sheria kwasababu tu wameenda kinyume na matakwa yenu?

Uhuru gani mnaozuia vyama vya upinzani kufanya shughuli zao kama sheria inavyotaka na kuwaacha viongozi wa CCM peke yao wazunguke nchi nzima?

Uhuru gani kwenye taifa lenye mgao wa maji na umeme kila mara? taifa lenye uhaba wa matundu ya vyoo kwenye shule zake?

Huyo mkuu wa mkoa bora akae kimya tu, huo ni uhuru wa CCM sio wa watanzania.
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amesema leo usiku wa saa 6:00 katika uwanja wa taifa zitarushwa fataki kama ishara ya kuanza sherehe za uhuru.

Wananchi msiogope bali mshangilie na kurukaruka kwa furaha, amesema.

Source: ITV habari
Wananchi watajaa pale ila yeye ataenda na V8 + posho
 
Uhuru wa amani hakika tunamshukuru Mungu kwa 100%, shida ni hili dubwasha liitwalo "Neo Colonialism" na haswa la ngozi yetu nyeusi, yani huweziamini ni kweli tunaishi kwenye nchi ya asali na maziwa kwa rasilimali za gesi, mafuta, madini, mbuga za wanyama, maziwa, bahari, ardhi yenye rutuba na mvua za kutosha kwa hali ya uchumi wa nchi yetu ulivyo baada ya miaka 60
 
Sherehe za Uhuru zienda pamoja na peace & reconciliation (maridhiano ya kitaifa) - watanzania wengi wapo magelezani wakishitakiwa kwa makosa ya kisiasa, wengine vilema, wengine wamefiwa na wapendwa wao vifo vilivyotokana na mambo ya kisiasa.

Ni muda sasa wa kukaa pamoja tuone je tunakwama wapi kama familia moja ya Tanganyika? huu si muda wa kukomoana, utemi utemi hautufikishi mbali kama taifa.

Tulitegemea DPP afute kesi zote za kisasa ili hao wananchi waachiwe bila masharti yoyote wakaungane na familia zao kusherehekea miaka hii 60 ya uhuru wa Tanganyika.

Hatuoni ufahali wowote kusherehekea sikukuu hii wakati wenzetu wanasota magelezani - haina maana kwa kweli.
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla amesema leo usiku wa saa 6:00 katika uwanja wa taifa zitarushwa fataki kama ishara ya kuanza sherehe za uhuru.

Wananchi msiogope bali mshangilie na kurukaruka kwa furaha, amesema.

Chanzo: ITV habari
Tanzania itakuwa huru siku Mkoloni CCM atakapoondoka ....!!
 
Uhuru gani huo mnaotuambia leo hii taifa linalotegemea hisani ya beberu mpaka kwenye bajeti ya serikali miaka 60 baada ya kuupata?

Uhuru gani huo mnaokamata wapinzani wenu kisiasa bila kufuata sheria kwasababu tu wameenda kinyume na matakwa yenu?...
Rukaruka kwa furaha ukisikia fataki bwashee!
 
Uhuru gani huo mnaotuambia leo hii taifa linalotegemea hisani ya beberu mpaka kwenye bajeti ya serikali miaka 60 baada ya kuupata?

Uhuru gani huo mnaokamata wapinzani wenu kisiasa bila kufuata sheria kwasababu tu wameenda kinyume na matakwa yenu?

Uhuru gani mnaozuia vyama vya upinzani kufanya shughuli zao kama sheria inavyotaka na kuwaacha viongozi wa CCM peke yao wazunguke nchi nzima?

Uhuru gani kwenye taifa lenye mgao wa maji na umeme kila mara? taifa lenye uhaba wa matundu ya vyoo kwenye shule zake?

Huyo mkuu wa mkoa bora akae kimya tu, huo ni uhuru wa CCM sio wa watanzania.
Acha kisirani wewe mzee
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla amesema leo usiku wa saa 6:00 katika uwanja wa taifa zitarushwa fataki kama ishara ya kuanza sherehe za uhuru.

Wananchi msiogope bali mshangilie na kurukaruka kwa furaha, amesema.

Chanzo: ITV habari
Tanzania haipo huru kabisa.
 
Chama chakavu..ndio kinachosherekea uhuru wake wa kuendelea kuwanyonya watanzania..60 years of misery..magojwa ujinga na umasikini plas ufisadi vinaendelea kama kaulimbiu yao.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Enzi za mwendazake kulikuwa hamna hivi vitu...sasa ulizieni basi hata bei ya hilo fataki, vikao vya procurement vilikuwa vingapi na posho kiasi gani ilitolewa mpaka kupata vocha ya kulinunua hilo fataki....ila ndio hela inarudi mtaani🤣
 
Uhuru ni wa Tanganyika,,,tusipotoshe ukweli,,mwaka 1961 hakukuwa na Tanzania.
 
Kwa nini Freedom house inasema Tanzania hatujapata uhuru wa kweli, uhuru kamili?

Uhuru gani huo mnaotuambia leo hii taifa linalotegemea hisani ya beberu mpaka kwenye bajeti ya serikali miaka 60 baada ya kuupata?

Uhuru gani huo mnaokamata wapinzani wenu kisiasa bila kufuata sheria kwasababu tu wameenda kinyume na matakwa yenu?

Uhuru gani mnaozuia vyama vya upinzani kufanya shughuli zao kama sheria inavyotaka na kuwaacha viongozi wa CCM peke yao wazunguke nchi nzima?

Uhuru gani kwenye taifa lenye mgao wa maji na umeme kila mara? taifa lenye uhaba wa matundu ya vyoo kwenye shule zake?

Huyo mkuu wa mkoa bora akae kimya tu, huo ni uhuru wa CCM sio wa watanzania.
Wacha CCM wafurahie uhuru wao wewe subiri huo uhuru kamili mbona simple tu
 
Uhuru gani huo mnaotuambia leo hii taifa linalotegemea hisani ya beberu mpaka kwenye bajeti ya serikali miaka 60 baada ya kuupata?

Uhuru gani huo mnaokamata wapinzani wenu kisiasa bila kufuata sheria kwasababu tu wameenda kinyume na matakwa yenu?

Uhuru gani mnaozuia vyama vya upinzani kufanya shughuli zao kama sheria inavyotaka na kuwaacha viongozi wa CCM peke yao wazunguke nchi nzima?

Uhuru gani kwenye taifa lenye mgao wa maji na umeme kila mara? taifa lenye uhaba wa matundu ya vyoo kwenye shule zake?

Huyo mkuu wa mkoa bora akae kimya tu, huo ni uhuru wa CCM sio wa watanzania.
AMINA
 
Back
Top Bottom