Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,445
- 3,403
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema "Kuanzia leo, baada ya tamko langu leo, usiku wa leo na kuendelea hakuna 'Panya Road' atasalimika katika mkoa wa Dar, oparesheni inayoanza usiku wa leo si salama kwa 'Panya Road', oparesheni inayoanza leo inaenda kuua uti wa mgongo wa mtandao mzima wa 'Panya Road"
Ameongeza "Niwasihi wazazi kwamba operesheni hii haitowaacha watoto wao wahalifu, kama mzazi ulizoea kupata zawadi kwa mtoto, TV bila kujua kipato chake, akudanganye 'amebeti', kawatafuteni watoto wenu kwenye vituo vya Polisi kuanzia kesho"
Amesisitiza "Kila Wilaya kwa mikoa ya Kipolisi, kutoa taarifa za kila siku za Operesheni ondoa 'Panya Road' na kudhibiti uhalifu katika mkoa wa Dar es Salaam kila siku, toeni taarifa tusipotoa taarifa watazitoa taarifa mbaya"
Ameyasema hayo siku moja baada ya kundi hilo la uvamizi kuvamia na kujeruhi watu 19 katika Maenel ya Mtongani, Kunduchi mkoani humo