johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,968
- 141,976
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amesema kutokana na kuchelewa kwa mvua za vuli maji katika mto Ruvu yamepungua na kusababisha upungufu wa lita milioni 70 sawa na 26%
Makalla amewataka wakazi wa jiji la Dar es salaam kutumia maji kwa uangalifu wakati tukisubiri mvua zitakazojaza mto.
======
RC MAKALLA ASIMAMISHA ZOEZI LA UBOMOAJI ULIOFANYIKA MBWENI/BUNJU.
- Aunda timu ya Wataalamu wa ardhi kumaliza Mgogoro.
- Awataka wananchi wawe watulivu Na watoe ushirikiano ili eneo hilo lipimwe kwa mujibu wa sheria Za mipango miji.
- Wananchi wakiri wao ni wavamizi Na wameiomba serikali ikilipima eneo wao wauziwe Viwanja vidogo ambavyo watamudu gharama.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesimamisha zoezi la Bomoabomoa kwa Wananchi waliovamia eneo la Serikali mpakani mwa Mbweni na Bunju A mpaka pale muafaka wa pamoja utakapopatikana.
RC Makalla ametoa maelekezo hayo alipowatembelea Wananchi hao akiwa na Viongozi mbalimbali na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa ambao November 22 mwaka huu nyumba zao zilibomolewa.
Kutokana na Hali hiyo RC Makalla ametuma timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Halmashauri ya Kinondoni, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Viongozi wa Wananchi hao ili kupata Suluhu ya pamoja ya kumaliza Mgogoro huo.
Kwa upande wao Wavamizi wa eneo hilo akiwemo SALUM HASHIM wamekiri kufanya kosa kuvamia maeneo hayo na kuizuia Serikali kufanya zoezi la Upimaji ambapo wameiomba Serikali kuwatazama kwa jicho la tatu.