RC Makalla: DSM ina upungufu wa Maji wa Lita milioni 70 kwa siku sawa na 26%, Wananchi tumieni maji kwa uangalifu!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,975
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amesema kutokana na kuchelewa kwa mvua za vuli maji katika mto Ruvu yamepungua na kusababisha upungufu wa lita milioni 70 sawa na 26%

Makalla amewataka wakazi wa jiji la Dar es salaam kutumia maji kwa uangalifu wakati tukisubiri mvua zitakazojaza mto.

======

RC MAKALLA ASIMAMISHA ZOEZI LA UBOMOAJI ULIOFANYIKA MBWENI/BUNJU.

- Aunda timu ya Wataalamu wa ardhi kumaliza Mgogoro.

- Awataka wananchi wawe watulivu Na watoe ushirikiano ili eneo hilo lipimwe kwa mujibu wa sheria Za mipango miji.

- Wananchi wakiri wao ni wavamizi Na wameiomba serikali ikilipima eneo wao wauziwe Viwanja vidogo ambavyo watamudu gharama.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesimamisha zoezi la Bomoabomoa kwa Wananchi waliovamia eneo la Serikali mpakani mwa Mbweni na Bunju A mpaka pale muafaka wa pamoja utakapopatikana.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo alipowatembelea Wananchi hao akiwa na Viongozi mbalimbali na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa ambao November 22 mwaka huu nyumba zao zilibomolewa.

Kutokana na Hali hiyo RC Makalla ametuma timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Halmashauri ya Kinondoni, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Viongozi wa Wananchi hao ili kupata Suluhu ya pamoja ya kumaliza Mgogoro huo.

Kwa upande wao Wavamizi wa eneo hilo akiwemo SALUM HASHIM wamekiri kufanya kosa kuvamia maeneo hayo na kuizuia Serikali kufanya zoezi la Upimaji ambapo wameiomba Serikali kuwatazama kwa jicho la tatu.
 
😁😁😁
B0Jj.jpg
 
Hii ni aibu serikali haina mpango wowote zaidi ya kusubiri maji ya mvua
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amesema kutokana na kuchelewa kwa mvua za vuli maji katika mto Ruvu yamepungua na kusababisha upungufu wa lita milioni 70 sawa na 26%

Makalla amewataka wakazi wa jiji la Dar es salaam kutumia maji kwa uangalifu wakati tukisubiri mvua zitakazojaza mto.

Source: ITV habari
 
Mbona huo upungufu hatujawahi kuuona kwa miaka 6 iliyopita?
Kuna maeneo matatu ambayo Mama Samia asicheze nayo nayo Ni maji,umeme na chakula

Hayo maeneo yaweza angusha CCM na watu kuingia barabarani kwa maandamano na vurugu

Mama Samia hayo maeneo usikubali yayumbe Tena waonye watendaji wako wasilete panic kwenye hayo maeneo kwenye public ita cost serikali yako
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amesema kutokana na kuchelewa kwa mvua za vuli maji katika mto Ruvu yamepungua na kusababisha upungufu wa lita milioni 70 sawa na 26%

Makalla amewataka wakazi wa jiji la Dar es salaam kutumia maji kwa uangalifu wakati tukisubiri mvua zitakazojaza mto.

Source: ITV habari

Kwani yule mchina kaanza tena ku test mitambo yake? Si tuliambiwa yeye ndiye alikuwa chanzo?

IMG_20211121_091817_559.jpg
 
CCM na uongozi walionao huu msimu baada ya kifo cha baba ni uongozi wa aibu sana. Naona laana inaitafuna ccm taratibu.....itakufa kibudu. Yaani mkoa ambao umepitiwa na bahari ya hindi, bahari iliyojaa maji tele..wananchi wanatangaziwa ukame mkubwa na ukosefu wa maji hii ni hatari. Naona wanamtafuta ibirisi shetani kwa nguvu zao zote, wanautaka ukame japo ibirisi anawakimbia bado wanamfuata tu...hii laana mbaya sana
 
RC MAKALLA: UKAME NDIO CHANZO CHA UPUNGUFU WA MAJI.

- Asema mvua za Vuli zimechelewa ambazo huanza mwezi Oktoba na upungufu wa maji ni lita 70 Milioni kwa siku.

- Apongeza operesheni ya wachepushaji maji imeongeza kiasi lakini upungufu Upo mpaka mvua zinyeshe.

- Awataka Wananchi kutumia maji vizuri na kutunza vyanzo vya maji.

- Kilichotolea Ni mabadiliko ya Tabia Nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema Mgao wa maji Jijini humo utaendelea kuwepo mpaka pale Mvua zitakapoanza kunyesha na kuongeza kina Cha maji kwenye vyanzo vya maji Ruvu Chini na Ruvu Juu ambavyo kwa Sasa vina upungufu wa maji.

RC Makalla amesema hayo wakati wa ziara ya kutembelea Vyanzo vya Maji vya Ruvu Juu na Ruvu Chini akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Watendaji wa DAWASA iliyolenga kujionea na kujiridhisha Hali ya Maji kwenye vyanzo hivyo.

Akizungumza katika ziara hiyo RC Makalla amesema baada ya Maelekezo yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa yamesaidia uwepo wa Ongezeko la Lita Milioni 200 kutoka Lita Milioni 65 na kufanya upungufu wa Lita Milioni 70 kwa Ruvu Chini.

Aidha RC Makalla amesema upande wa Ruvu Juu Hali sio mbaya Sana Kutokana na uzalishaji wa maji kuendelea kuwa Lita Milioni 196 kwa siku.

Kutoka na Hilo RC Makalla ametoa wito kwa Wananchi kutumia Maji vizuri na kuendelea kutunza vyanzo vya maji huku akipongeza jitiada zinazofanywa na Wizara ya Maji na DAWASA.

Hata hivyo RC Makalla amesema mahitaji ya Maji kwa Mkoa wa Dar es salaam kwa siku ni Lita Milioni 540 na uzalishaji Lita Milioni 520 na asilimia kubwa ya Maji hayo yanategemea kunyesha kwa mvua lakini Kukosekana kwa mvua za Vuli kwa takribani miezi miwili Sasa imesababisha upungufu wa maji.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema Mamlaka hiyo inaendelea kufanya kila jitiada kuhakikisha kila Mwananchi anapata Huda ya Maji licha ya kuwepo kwa Mgao.

Kwa mujibu wa DAWASA, Mtambo wa Maji Ruvu Juu unazalisha Lita Milioni 196 kwa siku na Mtambo wa Maji Ruvu Chini unazalisha Lita Milioni 270 kwa siku lakini Kutokana na upungufu wa maji kwa Sasa
 
Upumbavu mtupu! Miaka 60 ya uhuru jiji kubwa kama Dar halina reservoir ya uhakika ya kutosheleza hata miaka mitatu ya ukame? Halafu kuna mazuzu watashangilia. Akili sifuri.
Hiyo mika 60 popilation ya watu ili stuck au imeongezeka?
Hiyo reservior iko wapi? Na kwamba miaka uote iko full na inahudumia jiji na kwa ongezekeko la watu bila shida?
 
Back
Top Bottom