johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,915
- 141,879
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amevunja mkataba wa ujenzi wa jengo la halmashauri ya Busokelo mkoani Mbeya kati ya serikali na kampuni ya JWTZ Mzinga.
Chalamila amesema ujenzi huo ulioanza mwaka 2018 umekuwa ukisuasua hivyo pamoja na kwamba wajenzi hao ni chombo cha dola hawezi kuwavumilia. Amewataka halmashauri ya Busokelo kutafuta mkandarasi mwingine haraka na ujenzi uendelee mara moja.
Naye msimamizi wa ujenzi huo kutoka jeshini Mzinga Kanali Jackson amesema ujenzi huo umekuwa ukisuasua kwa sababu halmashauri hiyo imekuwa ikitoa fedha kwa kuchelewa sana na hakukuwa na namna ya kuendelea na ujenzi wakati fedha hakuna.
Source Eatv habari!
Maendeleo hayana vyama